Maduka ya Dawa yaliyo nje ya mageti ya Hospitali za Serikali huwa na dawa muda wote lakini ndani ya Hospitali husika hamna dawa

Aisee
 
Hebu ileza maduka ya nje yanakuwaje chanzo cha ukozefu wa dawa hospitali. Serikalo inasema mama ni bure Lakini hivyo vitu vya bure huwa serikali yenyewe haivileti sasa kosa la nani kwa mfano

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu..hapa umeongea point nzuri..ambayo inaitaji mjadala mpana..kutolewa dawa bure na upatikanaji usio na mashaka wa hizo dawa za bure kwenye hivi vituo vyetu vya afya..kwa maoni yangu hii ni changamoto kubwa sana kwa vituo vingi vya afya kuweza kuendesha kazi zao za kila siku kwa ufanisi..
 
Nchi hii imejaa wapumbavu. Luckily mimi siyo Daktari.

Walahi, mimi ningekuwa Daktari ningekuwa nawaandikia hawa watu fawa yoyote.

Maana inaonekana wanachotaka ni Dawa tu. Nyamabafff
 
Mtoa mada Muongo kichizi hata kipindi cha magufuli hali ni ile ile tuliuguza sana temeke pale...tena usiku ndo kabisa hakuna huduma 2019 hata gloves zilikua dili hospital za serikali
Wakati wa Magufuli Basket Fund haikutoka hata 100 mbovu, hospitali zilipitia kipindi kigumu sana.

Unfortunately hakuna mjuaji yeyote aliyebinua kimdomo kuongea🤣🤣🤣
 
Huu ndio ukweli but mchungu
 
Usiwalaum wanakuambia ukachukue dawa kiliman pharmacy watalum wenye jukum la kuakikisha dawa inapatikan katkka hospital hao wenye pharmacy nje wanatusaidia sana sema kila mmoja anasema kwa utashi wake utakuta pharmacy wana dawa nzur currently lkin hospital za umma wana dawa za kawaida oldest kwa ntumiaj wa bima dawa nzan malalamiko yetu kiini cheke ni wasiotumia bima all in all uzembe wa wakuu wa hospital za umma kuanzia mganga mkuu mpharamacia na uhab wa dawa msd ndio wenye maduka bianfs wanatumia kma fursa big up kwao wanatusadia sana kwenye dharura

Sent from my SM-G965U using JamiiForums mobile app
 
Mbona kwenye Hospital binafsi hukuti haya maduka ya dawa yamewekwa nje ya mageti yao?
Huruhusiwi kuandika dawa nje na orodha ya dawa zinazopatikana kwenye hospitali binafsi, ukikaidi mwisho wa mwezi utauona mchungu.
 
Mbowe vip hali yake mkuu?
 
Issue ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya ni changamoto ya nchi nzima, ukifuatilia vizuri utaona malalamiko yanafanana.

Nafikiri sera, na miongozo ya upatikanaji wa dawa iliyopo haifai kwa sababu imeshindwa kutatua kero za wananchi,

Wenye dhamana wanapaswa kuangalia suala hili upya kwa macho matatu.
 
Acha kupotosha, hali ilikuwa ile ile hata kwenye hiyo awamu ya tano. Niliuguza sana madogo hospitali ya Wilaya ya Meru, kipindi cha awamu ya tano...dawa nyingi za maana ulikuwa unaenda Tengeru kutafuta pharmacy binafsi ukikosa inabidi uende mpaka USA river
 

Kabla ya malalamiko yoyote twende tukajifunze mfumo wa ununuzi wa dawa na vifaa tiba kwenye hospital zetu na control system yake. Ni nani anahysika na mnyororo mzima. Bajeti ni kiasi gani na inatolewa kiasi gani?

Msisikie hoyahoya huko nje na kusema ilikuwa hali nzuri, bali watu walizimwa kusema. Ulikuwa unawekewa kaa la moto mdomoni lakini unatakiwa useme ni mkate.

Tutafakari pia kwenye:
1: Elimu
2: Afya
3: Ujenzi
4: Sheria
5: Kilimo
6: Biashara ie Bank
7: Mawasiliano ie. Simu

Ni wapi serikali inafanya na kuishinda sekta binafsi kwa ujumla kwenye nchi hii? Haya mambo yanahitaji kushirikiana na kwekeana mazingira mwafaka.

Vitu vya serikali huwa vinaelea hapo kati kutokana na kubeba jukumu la kutoa huduma zaidi kuliko biashara hivyo kuhitaji imput kubwa. Je serikali inaweza kusustain huo mzigo?? Hapo unahitaji mfumo imara na si mtu imara.

Watu walioko kwenye hizo sekta hawajitumi ipasavyo. Kwani hawategemei moja kwa moja malipo toka pale walipo.
Ni wafanyakazi wangapi wa serikali wana objectives na zinakuwa reviewed kila mwisho wa mwaka na kuulizwa utimizaji wake na kuweka mpya au ndo ile theoretical OPRAS.

Je uliwapa vitendea kazi?
BRN ilifia wapi?? Hata utekelezaji wake ulionekana mzigo kwa serikali kutokana na hitaji lake.

Maduka ya dawa nje ya hospitali ni ya kushukuru, kwa kuwa yanasuppliment deficit kwenye institution hizo. Ukitaka ujue umuhimu wake yafunge yote kwa mwezi mmoja tu.

Kuna wakati watoa huduma ya afya wanagawiana gloves na kukaa nazo mifukoni kutokana na uchache wake, si kwa kupenda. Fikiria mama mmoja anaweza kuhitaji kupimwa mara nne kabla ya kujifungua. Nawe umepewa gloves kumi kwa siku???

Tunasema huduma bure kwa watoto chini ya miaka mitano na wazee, uliza hospitali inayopeleka idadi ya hao watu wanaopata huduma bure na kupewa bujeti yake ili kufidia deficit yake kila mwezi na kupewa hela hiyo kama utaipata. Hili ndilo linalofanya ukifika dirishani unaambiwa kanunue hii dawa ya mtoto au mzee.
 
ni hospital gani hiyo? Ni vyema ungeitaja
Almost zote !! Sometimes tuwe wakweli, maana wengine hawapendi kukubali ukweli, hii issue ni kama cancer ya nchi, kuna kipindi hupungua makali kidogo lakini IPO palepale !! Au nasema uongo bandugu ??!
 
Huruhusiwi kuandika dawa nje na orodha ya dawa zinazopatikana kwenye hospitali binafsi, ukikaidi mwisho wa mwezi utauona mchungu.
Siyo kwamba huruhusiwi kuandika.

Ila ukiandika Dawa ambazo hazipo store ya hospitali maana yake mgonjwa akanunue ndio utapata lawama kama hizi.

Kwahiyo, inadhauriwa Umwandikie mgonjwa Dawa zilizopo store ili kukwepa lawama kama hizi.
 
Huu msamiati mpya, diblo ndo nani naye huyu!
 
Dunia ya sasa hivi ukipenda vya bure na dezo utaishi maisha magumu mno.
Ni kweli mkuu ila pia dunia ya sasa usipojitambua ukawa na ujinga mwingi unaweza ukalipishwa kiingilio na mkeo kwenye nyumba yako ambayo umeinjenga mwenyewe.

Huwezi kulipa kodi na tozo halafu ulipie na huduma ambazo kimsingi zilitakiwa ziboreshwe na kodi ambazo umelipia.

Serikali haiombwi kuboresha huduma kwa hisani ni wajibu wake kuboresha ila kwa wajinga wajinga wanaweza kuhisi kuwa eti kutoa rushwa ni lazima ili upewe huduma.
 
Chifu Hangaya alipoingia madarakani kwenye zile ziara za kwanza kwanza alikutana na Baraza la Maaskofu katoliki, nakumbuka moja ya changamoto walizomweleza ni kuwa "kutokana na serikali kuboresha huduma za afya sasa hivi hospitali zao hawapati wateja na wamefikia kiwangi cha kushindwa kuwalipa watumishi wao mishahara" wakaomba waondolewe Kodi kwenye huduma za afya nk!

Muda huu Hangaya alikutana nao tena akawaukiza vipi wateja wanapatikana? Nadhani watamwambia "Asante mama kwa kutuongezea wateja!" maana yake ni kwamba huduma za afya kwenye hospitali na vituo vya umma zinaekekea kufa kabisa, ni suala la muda tu!
 
Hata wakati wa jpm mfumo ulikuwa huu huu
Dawa hospital hakuna ila maduka ya dawa nje
Zipo!
Nchi ngumu hii kuanzia juu mpaka chini

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…