Maduka ya Dawa yaliyo nje ya mageti ya Hospitali za Serikali huwa na dawa muda wote lakini ndani ya Hospitali husika hamna dawa

Siyo kwamba huruhusiwi kuandika.

Ila ukiandika Dawa ambazo hazipo store ya hospitali maana yake mgonjwa akanunue ndio utapata lawama kama hizi.

Kwahiyo, inadhauriwa Umwandikie mgonjwa Dawa zilizopo store ili kukwepa lawama kama hizi.
Hivi huwa tatizo ni nini kwenye ishu ya dawa? Kwamba serikali haina pesa ama ni vile sio kipaumbele?

Maana serikali inaweza agiza Land Cruiser hata 700 za 150M mpaka 200M!

Hivi kwa billion 100 ni dawa kiasi gani zinaweza nunuliwa?

Yani mie nikipewa hii nchi naweza nikaiendesha kwa namna ya tofauti sana! Its high time matatizo madogo madogo yanatakiwa yaishe haya.
 
Hata wakati wa jpm mfumo ulikuwa huu huu
Dawa hospital hakuna ila maduka ya dawa nje
Zipo!
Nchi ngumu hii kuanzia juu mpaka chini

Ova
Na sio kwamba dawa hamna ila ni hujuma tu zinafanyika! Hata ununue dawa kontena 100 lazma watatengeneza deficit tu kuwa dawa hamna au zimeisha ili ukanunue duka la nje ya hospitali!
 
Kumbe sheria ilimzuia? Si mnasema alikuwa hafuati sheria?

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mabavicha kuna wakati huwa mnajikaanga kwa mafuta yenu wenyewe!
 
Tatizo kubwa lipo kwenye budgeting.

Unaweza kuaguza dawa za magonjwa fulani kulingana na takwimu zako. Halafu ghafla ukapata idadi kubwa sana ya wagonjwa husika kuliko kiasi cha dawa ulichonacho.

Na ukiagiza tena huwa inachukua muda mrefu kuleta.

Vile vile unaweza ukaagiza dawa na usiletewe kiwango ulichoomba.

Pia, vituo vya afya vimewekewa ceiling ya bajeti.

Huwezi kupanga bajeti (ikiwemo ya dawa ) zaidi ya kuwango ulichowekewa.

Na hii ceiling inatokana na takwimu kutoka kituo husika.
 
Maybe ila wenye pharmacy nje wao wanawezaje kuwa na range kubwa ya dawa?
 
Watu wa famasi hawafuati taratibu zozote za manunuzi. Mzigo ukiisha unaagizwa.

Mambo ya serikali hayaendi hivyo.

Drug editing ya nguvu huwa inafanyika. Unaweza kufungwa.
Duh basi serikali yenyewe kumbe inafeli
 
Maybe ila wenye pharmacy nje wao wanawezaje kuwa na range kubwa ya dawa?
Tena kwa wakati wote, hata nesi anaefanya kazi serikalini ukimwambia nataka dawa fulani kesho anakuletea unampa hela yake, lakini ukienda huko Hospital kesho yake dawa ile ile hakuna unaandikiwa.
Inavyooenekana ni kuwa kila mtu anakula kulingana na urefu wa kamba yake,na usimamizi mbovu
 
Yani inashangaza na hao madaktari wanaoandika hizo dawa wao kwanini wasimshauri mtu wa bohari kwamba alete varieties za dawa! Yani kwanini iwe Paracetamol tu na sio Aspirin, Diclopar,Ibuprofen?

Yani kwanini dawa iwe aina moja tu!
 
Na
Watu wa famasi hawafuati taratibu zozote za manunuzi. Mzigo ukiisha unaagizwa.

Mambo ya serikali hayaendi hivyo.

Drug editing ya nguvu huwa inafanyika. Unaweza kufungwa.
Inakuwaje miaka yote tangu uhuru serikali inashindwa kudili na swala muhimu kama hilo ambalo linahusu afya ya binadamu? Je mbona Hospital binafsi mara nyingi hukosi dawa? Ifike mahali sasa Hospital za serikali ziwe ndo kimbilio la wananchi kutokana huduma bora zitolewazo
 
Duh basi serikali yenyewe kumbe inafeli
Mkuu, mambo ya serikali unaweza kudhani yanakisewa ila ukiwa kwenye mfumo ndio utajua kwanini yako hivyo yalivyo.

Kwanza kwa mfumo wa Afya ulivyo, vituo havina CEOs wala wahasibu.

Na vinaongozwa na na Waganga kama CEOs.

Siku hizi kila kituo cha afya kina Account bank, na pesa zote za CHF, NHIF, basket fund na User fees ( cost sharing ) huwa zinaingia kwenye akaunti husika.

Hawa maCEOs wa vituo ndio watungaji wa Mpango wa bajeti, na tatizo wengi hawajui huwa wanaandika andika tu ilimradi wameshinikizwa na Makatibu wa Afya.

Mimi kuna kakituo nipo, huwa tunapata user fees kama 7M kwa mwaka lakini tumebajeti mpaka tunakunywa chai na mikate, manesi wanapata vitambaa na pesa za uniform pamoja na extra duties.

Ila kuna kituo kikubwa tu, huwa wanapata mpaka 15M kwa mwaka lakini wana maisha magumu sana kutokana na ukilaza wa CEO wao( Daktari ).

Ili upunguze tatizo hili inabidi uwe makini sana na takwimu ili ukiagiza dawa au kupanga bajeti usiwe na DEFICIT.
 
Dah usimamizi hapo sasa naelewa, kila mtu ana utashi wake kwenye kusimamia rasilimali
 
Wewe unajua ndani ya mwaka mzima familia yenu mtaugua nini na wangapi ?

Mambo huwa yanafanyika kwa makisio tu.

Je, ukikadiria kuwa kwa mwaka huu wa 2022/23 tunatarajia kupata wagonjwa wa pressure 500 halafu ghafla ukapata 800 hujapungukiwa na dawa hapo?

Au unadhani mifumo ya serikali dawa zikiisha unapoga tu simu mzigo unaletwa🤣
 
Ulicho sema ni sahihi kabisa ila kutaka kutuamisha ya kwamba kipindi cha JPM hili tatizo halikuwepo ni kundekeza siasa uchwara na propaganda ambazo hazita saidia kutatua tatizo.
Ifikie hatua Wtz tukubali ya kwamba taifa letu lina mfumo mbovu wa kiutawala na kiuwajibikaji na sio kumlaumu mtu mmoja.
 
Hapo umeongelea Point sasa! Mjadala unafungwa
 
Hebu jaribu kueleweka kwa kuijibu hoja ya KUKOSEKANA dawa...
 
Fungua na wewe hizo ni fursa kama fursa zingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…