Maeneo matatu yenye baridi zaidi Tanzania with facts

Maeneo matatu yenye baridi zaidi Tanzania with facts

1.Iringa- Mjini & Mufindi-Mpangatazara
2.Njombe mjini+vijijini kidogo
3.Mbeya-Tukuyu
4.Morogoro-Mahenge
5.Arusha

Mimi ni mzaliwa wa Arusha tena milimani.
Kuna sehemu pia Arusha kuna winter ila bado list naomba ifuatwe kama mstaafu.
 
Huko Makete jamaa wanaamka asubuhi kujiokotea ndege pori; yaani ndege wanapigwa na barsfu wanazima mpaka jua liwake.
Kila sebule Kuna chupa ya chsi ya moto, inanywewa muda wote.
Hatari sana!
 
Kwa yeyote aliyefika mufindi atakoa ushuhuda
Mufindi kuna joto sana hadi tunavuna chai tukiwa ndani ya vesti. Baridi ni Makete. Upepo uko Makambako. Manyunyu ya baridi yako Njombe. Jua kali liko Iringa mjini.
 
Nikienda makete siogi mpaka siku naondoka..!! 😹😹

Niliwahi kwenda church bila kuoga aisee..!!
 
Kamwene.
 

Attachments

  • 3623C1B2-DDBA-497D-9F97-CFE3ECE95B73.jpeg
    3623C1B2-DDBA-497D-9F97-CFE3ECE95B73.jpeg
    74.3 KB · Views: 36
Huko Makete jamaa wanaamka asubuhi kujiokotea ndege pori; yaani ndege wanapigwa na barsfu wanazima mpaka jua liwake.
Kila sebule Kuna chupa ya chsi ya moto, inanywewa muda wote.
Hatari sana!

Tulikwenda Lupila, Makete, kwenye maziko. Si unajua msibani watu mnalala nje, Ilibidi tuchome magogo tukakesha tunaota moto. Hatukuona jua siku nzima, ukungu mtupu. Tuliambiwa na mwenyeji kuna kipindi waalimu huwa wanaanza vipindi saa tatu, kuruhusu watoto waote moto, wachome mawe madogo madogo waingie nayo darasani kupasha mikono ili washike kalamu waandike. 😊
 
Back
Top Bottom