Kwema Wadau!
Mwaka huu DSM kumekuwa na Hali ya hewa ya baridi ambayo imenikumbusha Maeneo yenye hatari kubwa Kwa upande wa baridi.
Watu wengi ambao hawajazunguka hii nchi wanafikiri Arusha na Moshi pekee ndio yenye baridi ya kufa mtu, Kama nawe ni mmoja wapo basi umekosea kabisa, yapo Maeneo ukifika unaweza kukimbia siku hiyohiyo.
Maeneo hayo ni Kama ifuatavyo;
1. Njombe!
Kwa Tanzania hakuna kama Njombe, ukianzia Makete, ludewa, Makambako, huko ukienda ujipange.
Huko ni baridi mwanzo mwisho[emoji2][emoji2].
Yaani ukifika msimu wa baridi ndio Hali unazidi kuwa ngumu.
Arusha na Moshi hapa wakasome Kwanza, Kwanza baridi Yao ni yamsimu, ingawaje yapo baadhi ya Maeneo Kama Rombo huko nako kuna baridi lakini haifikii hayo Maeneo hapo.
Nyumba zote za Maeneo ya Mkoa wa njombe na Iringa zina madirisha ya vioo na Dari za mbao kuepusha baridi kuingia lakini bado utaisikia tuu na lazima ufunike Yale mablanket makubwa.
2. Iringa, hasa wilaya Mufindi, Mafinga.
Mafinga na Makambaku ni pua na mdomo, Hali ya hewa zinafanana. Baridi mwanzo mwisho. Yaani miezi yote 12 baridi lipo, sema kuna kipindi linapungua lakini kipindi cha kiangazi baridi lake ni Sawa na kipindi cha baridi la baadhi ya mikoa Kama Pwani, na Dar, Dodoma, Singida, tabora n.k
3. Arusha.
Wakati mwingine watu waarusha baridi Lao wanadhani ndio linaongoza Tanzania lakini kimsingi sivyo, wao wanaweza kushika nafasi ya tatu wakichuana na Kilimanjaro.
4. Kilimanjaro, hasa Maeneo ya Moshi, Rombo, Moshi vijijini, Hai, Usangi, Chome, Suji, Tae n.k
Baridi la Maeneo ya marangu ukipanda Mlima Kilimanjaro nalo ni Kali, lakini haliumizi Kama lile baridi la Mafinga, au njombe huko.
5. Tanga, Lushoto.
Milima ya usambara imechangia Kwa kiasi kikubwa kuifanya wilaya ya lushoto na Maeneo ya karibu yanayozunguka Maeneo hayo.
6. Mbeya, Maeneo ya Mbeya Mjini, Rungwe, na Tukuyu kuelekea Kyela,
Baridi la Mbeya ni Kali ingawaje linamsimu wake..
7. Ruvuma
Ukaribu wa Songea na mkoa wa njombe ni Kama ilivyo Kwa ukaribu wa Moshi na Arusha.
Sehemu hizo Kwa hapa Tanzania kama unataka kujua nini maana ya baridi basi fika sehemu hizo, ingawaje yapo Maeneo mengine ya Mikoa Kama Morogoro Kama Turiani, na Maeneo ya Singer na Rukwa.
Nawasilisha