Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Baridi yao kidogo tatizo upepoMafinga baridi ni mwaka mzima. Hakuna msimu.
Kwa hiyo kamasi linadondoka mwaka mzima?Mafinga baridi ni mwaka mzima. Hakuna msimu.
Mbona umepasahau na Manzese Dar es Salaam na kwenyewe kuna Baridi hakuna Mfano.Kwema Wadau!
Mwaka huu DSM kumekuwa na Hali ya hewa ya baridi ambayo imenikumbusha Maeneo yenye hatari kubwa Kwa upande wa baridi.
Watu wengi ambao hawajazunguka hii nchi wanafikiri Arusha na Moshi pekee ndio yenye baridi ya kufa mtu, Kama nawe ni mmoja wapo basi umekosea kabisa, yapo Maeneo ukifika unaweza kukimbia siku hiyohiyo.
Maeneo hayo ni Kama ifuatavyo;
1. Njombe!
Kwa Tanzania hakuna kama Njombe, ukianzia Makete, ludewa, Makambako, huko ukienda ujipange.
Huko ni baridi mwanzo mwisho😃😃.
Yaani ukifika msimu wa baridi ndio Hali unazidi kuwa ngumu.
Arusha na Moshi hapa wakasome Kwanza, Kwanza baridi Yao ni yamsimu, ingawaje yapo baadhi ya Maeneo Kama Rombo huko nako kuna baridi lakini haifikii hayo Maeneo hapo.
Nyumba zote za Maeneo ya Mkoa wa njombe na Iringa zina madirisha ya vioo na Dari za mbao kuepusha baridi kuingia lakini bado utaisikia tuu na lazima ufunike Yale mablanket makubwa.
2. Iringa, hasa wilaya Mufindi, Mafinga.
Mafinga na Makambaku ni pua na mdomo, Hali ya hewa zinafanana. Baridi mwanzo mwisho. Yaani miezi yote 12 baridi lipo, sema kuna kipindi linapungua lakini kipindi cha kiangazi baridi lake ni Sawa na kipindi cha baridi la baadhi ya mikoa Kama Pwani, na Dar, Dodoma, Singida, tabora n.k
3. Arusha.
Wakati mwingine watu waarusha baridi Lao wanadhani ndio linaongoza Tanzania lakini kimsingi sivyo, wao wanaweza kushika nafasi ya tatu wakichuana na Kilimanjaro.
4. Kilimanjaro, hasa Maeneo ya Moshi, Rombo, Moshi vijijini, Hai, Usangi, Chome, Suji, Tae n.k
Baridi la Maeneo ya marangu ukipanda Mlima Kilimanjaro nalo ni Kali, lakini haliumizi Kama lile baridi la Mafinga, au njombe huko.
5. Tanga, Lushoto.
Milima ya usambara imechangia Kwa kiasi kikubwa kuifanya wilaya ya lushoto na Maeneo ya karibu yanayozunguka Maeneo hayo.
6. Mbeya, Maeneo ya Mbeya Mjini, Rungwe, na Tukuyu kuelekea Kyela,
Baridi la Mbeya ni Kali ingawaje linamsimu wake..
7. Ruvuma
Ukaribu wa Songea na mkoa wa njombe ni Kama ilivyo Kwa ukaribu wa Moshi na Arusha.
Sehemu hizo Kwa hapa Tanzania kama unataka kujua nini maana ya baridi basi fika sehemu hizo, ingawaje yapo Maeneo mengine ya Mikoa Kama Morogoro Kama Turiani, na Maeneo ya Singer na Rukwa.
Nawasilisha
Sumbawanga mara zote pana baridi kali kuliko MbeyaSumbawanga nako baridi si haba.
Ukimwi unajitakia mwenyewe ila baridi hauikwepi ukiwa "Nzombe".Tatizo Njombe Ukimwi ndio nyumbani kwake,ngono kila sekunde.
Ati nini makete?Njombe mjini baridi ni miezi yote tofauti na Mafinga na Makete na Arusha ambapo baridi ni kwa msimu.
Sio panga lililonyeshewa mvua. Panga lilonyeshewa hata sio la baridi. Panga lilololala nje ndio hatari.Huku Meru kuna baridi kiasi kwamba ukilala na mwanamke mwembamba utadhani umelala na panga lililonyeshewa mvua
😆Sio panga lililonyeshewa mvua. Panga lilonyeshewa hata sio la baridi. Panga lilololala nje ndio hatari.
Joto halipo Dar tu
Hata Moro Kuna mazao kibao yanalimwa na yanawahi kukomaa sababu ya joto.
Mimi nipo Njombe na kila siku naoga maji ya baridi. Asubuhi hii nimeoga maji ya baridi najisikia vizuri sana. Ni kujiendekeza tu kuoga maji ya motoBaridi ya Njombe ukitaka Kuoga maji unachemsha Maji ya moto halafu unachemsha Mengine ya Vuguvugu kwa ajiri ya kupoozea ndio uoge sasa....😂😂
NjombeNimeishi Mufindi, Mbeya na Arusha,
Kuhusu Njombe na Mufindi wala sina shaka ndizo sehemu zinazoongozoea kwa baridi.
Baridi ya Mbeya ikifika mwezi wa 6 huwa ni kali kiasi kuliko ya Arusha.
List iwe hivi
1.Njombe
2.Iringa
3.Mbeya
4.Arusha
Naunga mkono hoja wilaya ya NEWALA-MTWARA ni hatari sana, sijui imekuwaje kule kuwe na baridi vile afu Mtwara kuwe na joto.Singida na Newala ziingie kwenye hiyo orodha aise