Maeneo yenye baridi la kufa mtu Tanzania

Maeneo yenye baridi la kufa mtu Tanzania

Kwema Wadau!

Mwaka huu DSM kumekuwa na Hali ya hewa ya baridi ambayo imenikumbusha Maeneo yenye hatari kubwa Kwa upande wa baridi.
Watu wengi ambao hawajazunguka hii nchi wanafikiri Arusha na Moshi pekee ndio yenye baridi ya kufa mtu, Kama nawe ni mmoja wapo basi umekosea kabisa, yapo Maeneo ukifika unaweza kukimbia siku hiyohiyo.

Maeneo hayo ni Kama ifuatavyo;

1. Njombe!
Kwa Tanzania hakuna kama Njombe, ukianzia Makete, ludewa, Makambako, huko ukienda ujipange.
Huko ni baridi mwanzo mwisho😃😃.
Yaani ukifika msimu wa baridi ndio Hali unazidi kuwa ngumu.

Arusha na Moshi hapa wakasome Kwanza, Kwanza baridi Yao ni yamsimu, ingawaje yapo baadhi ya Maeneo Kama Rombo huko nako kuna baridi lakini haifikii hayo Maeneo hapo.

Nyumba zote za Maeneo ya Mkoa wa njombe na Iringa zina madirisha ya vioo na Dari za mbao kuepusha baridi kuingia lakini bado utaisikia tuu na lazima ufunike Yale mablanket makubwa.

2. Iringa, hasa wilaya Mufindi, Mafinga.
Mafinga na Makambaku ni pua na mdomo, Hali ya hewa zinafanana. Baridi mwanzo mwisho. Yaani miezi yote 12 baridi lipo, sema kuna kipindi linapungua lakini kipindi cha kiangazi baridi lake ni Sawa na kipindi cha baridi la baadhi ya mikoa Kama Pwani, na Dar, Dodoma, Singida, tabora n.k

3. Arusha.
Wakati mwingine watu waarusha baridi Lao wanadhani ndio linaongoza Tanzania lakini kimsingi sivyo, wao wanaweza kushika nafasi ya tatu wakichuana na Kilimanjaro.

4. Kilimanjaro, hasa Maeneo ya Moshi, Rombo, Moshi vijijini, Hai, Usangi, Chome, Suji, Tae n.k
Baridi la Maeneo ya marangu ukipanda Mlima Kilimanjaro nalo ni Kali, lakini haliumizi Kama lile baridi la Mafinga, au njombe huko.

5. Tanga, Lushoto.
Milima ya usambara imechangia Kwa kiasi kikubwa kuifanya wilaya ya lushoto na Maeneo ya karibu yanayozunguka Maeneo hayo.

6. Mbeya, Maeneo ya Mbeya Mjini, Rungwe, na Tukuyu kuelekea Kyela,
Baridi la Mbeya ni Kali ingawaje linamsimu wake..

7. Ruvuma
Ukaribu wa Songea na mkoa wa njombe ni Kama ilivyo Kwa ukaribu wa Moshi na Arusha.

Sehemu hizo Kwa hapa Tanzania kama unataka kujua nini maana ya baridi basi fika sehemu hizo, ingawaje yapo Maeneo mengine ya Mikoa Kama Morogoro Kama Turiani, na Maeneo ya Singer na Rukwa.

Nawasilisha
Makambo ni Njombe,ongezea mkoa wa Songwe na Rukwa
 
Arusha huwezi ishindanisha na Mbeya. MBEYA weka Kundi moja na IRINGA. Hao ndo wanaelewana. Kule tukuyu kuna mwaka ilikuwa inaanguka snow. Mi nliwahi enda Mbeya mwaka flani kuamka asubuhi mimea imekauka kwa baridi... Acheni kabisa kuifananisha na Arusha. Mbeya yake Iringa.
 
Hata kimahesabu Iringa haiwezi kuwa na baridi kuzidi Mbeya ambayo ipo juu zaidi kutoka usawa wa bahari. Pia baridi inapungua kama utakaribia ziwa . Mfano Manda , Lupingu na maeneo mengine karibu na ziwa kuna joto. Ndio mana baridi kali sana mbeya laiki linapungua ukilifuata ziwa
Uko sahihi hata Kyela kuna joto Tukuyu baridi
 
Umasikini nao ni shida tu kuna Heater ya kutumia maji ya moto inayotumia Methane inayotokana na kinyesi cha Ng'ombe.

Ulanzi haushindi Mbege kwenye kutoa Baridi.
 
Uko sahihi hata Kyela kuna joto Tukuyu baridi
Yaaa mkuu nimeaa huko Ludewa,njombe , iringa hadi mbeya. Mfano ukitoka pale Mlangali ukiwa unaenda Manda utaona kama joto linaongezeka na mazao yanayo limwa pwani yanakubali na huko mfano mihogo mpunga mikorosho, na minazi na miembe. Wakati mwembe au mnazi utadumaa kwa njombe au Makambako.

Kipimo chepesi cha kujua kiwango cha joto we tazama mazao na miti yanayopatikana hapo.
 
We jamaa huijui baridi ya sgd aisee nenda sehemu moja inaitwa mitundu itigi utajua upo ndani ya friji
 
Inasemekana makambako ukiingia baa kila meza inakuwa na jiko la mkaa kwa chini yake likiwa na moto
 
Njombe leo inasoma nyuzi 4.....
Acha uongo mzee.
Screenshot_20220704-000857_Google.jpg
 
Nilisoma Magamba secondary Lushoto baridi la kule ni hatari zaidi la Mbeya
 
Najiuliza hiyo baridi ya Arusha mbona huwa siihisi ! au ngozi yangu ina kasoro
 
Fuatilia vizuri wazungu wanapenda kuishi wapi. Dar ES Salaam joto kali sana mzungu hawezi kuishi hapo. Kama anaishi ni kwa sababu tu ya kazi. Wazungu wanapenda kuishi sehemu zenye baridi
Ungetoa mfano kama arusha na moshi.

Ndio mana hata misheni zao walizipeleka sana maeneo ya baridi..mana wanapenda ubaridi baridi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Sehemu zenye bardi ni
1.Njombe hasa makete
2.Ruvuma hasa mbinga
3. Mufindi iringa
4.Mbeya
5. Rukwa eg Sumbawanga
6. Arusha & na baadhi ya maeneo ya Kilimanjaro eg Rombo, Sanya juu
7. Rushoto
Rushoto ndo wapi
 
Tatizo Njombe Ukimwi ndio nyumbani kwake,ngono kila sekunde.
Wacha wajidabulie mbususu na migegegdo kama kufa kupo tuu.
Sii tunasema kifo chetu kilishandikwa basi shida ya nini wao walishandikiwa kufa kwa ngoma so wacha waenjoy tunda
 
Back
Top Bottom