Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2021
Basi atakuwa amejenga fundi Michael, kuna watu leo wameamua hawataki tu kusikia kuna mema ya Hayati Magufuli.
Maiti zinaokotwa mtu ruvu, coco beach , wasiojulikana , case za uhujumu uchumi , kubambikiziwa case , kufilisiwa , korosho, mbaazi,mahindi , kahawa, samaki

Siwez kua mnafiki, hakuna jema
 
Nimefarijika kuona kwa mara ya kwanza umekuwa na maoni chanya kwa marehemu JPM.
Vituo vya afya vya kata vilianza kujengwa tangu 2013 na sehemu nyingi zilikuwa hazina wahudumu hivyo vituo vilikuwa havitumiki kata nyingi vituo vilikuwepo ila havijaanza kutumika vingine vilikuwa havijakamilika tuache kutukuza mtu hadi tunakuwa waongo. Hayo yalifanywa na kikwete , magufuli kaja kuvifungua.
 
Vituo vya afya vya kata vilianza kujengwa tangu 2013 na sehemu nyingi zilikuwa hazina wahudumu hivyo vituo vilikuwa havitumiki kata nyingi vituo vilikuwepo ila havijaanza kutumika vingine vilikuwa havijakamilika tuache kutukuza mtu hadi tunakuwa waongo. Hayo yalifanywa na kikwete , magufuli kaja kuvifungua.
Huu Uzi unakua Uzi bora mno

JK alikua mtu sana , alichofanya kwenye shule za kata kahamishia vituo vya afya kata hivyo hivyo
 
tatizo sio mradi ulipangwa mda gan. Kwa Tanzania ilivyo wanaweza kupanga mradi mwaka huu na ela ikaombwa ila itekeezaji ukawa zero.

Sisi wa mara tutamkumbuka kwa kuweza kumalizia hospital ya kwangwa iliyoanza ujenz wake toka enzi za Nyerere (japo sio kwa 100%)
Hospital ya kwangwa iko hatua gani?

Si ndio inatakiwa kuwa hospital ya rufaa ya mkoa.
 
Mradi wa kuuwa vyama vya upizani (lengo ilikua ukamilike kabla ya 2020) umefikia hatua gani?
Nafikiri huu mradi, ni mmoja ya miradi aliyo ifanikisha sanaaaa.

Wewe mpaka Mwamba aliye tangazo kuwa ndani ya massaa 24 atakuwa Waziri Mkuu anayakimbia matokeo na madeni yote ya wasimamizi wa vituo.

Mbunge wa Nkasi oyeeeeeee. Covid 19 oyeeeeeee.
 
Tatizo la Magufuli, alidhani atakuwa Rais wa Tanzania milele miradi mingi utadhani aliambiwa hawatakuja watu wengine kufanya haya mambo ni kupokezana vijiti unajikuna unapoweza unaachia wengine nao wataendeleza hakujifunza kuwa alianza kuyafanya Nyerere na hakuweza kumaliza.
Kwa hiyo miradi mingi kwako kero? Dah! Hii nchi ina wachawi wengi aisee...
 
Sisi wa Uswazi ndani ndani...
Barabara ya lami gomz to Moshi bar yenye taa na mitaro yake...Mradi wa maji kisarawe to gomz, toka 1994 tunahamia gomz hatukuwahi kua na maji ya bomba, chuma kimeingia in 4yrs mimaji km yote...

Na Flyover yetu ya Tazara, hii watu wanaosema ni ya JK nadhani ni vyema ht waka google kuangalia ilianza lini na ikaisha lini, sisi wakazi wa maeno hayo ndo tunaijua zaidi msitusemee tafadhali(Mipango sio matumizi, wewe demu wako akipewa mimba na mtu mwingine huyo mtoto anakuaje wa kwako?)
Mkuu heshima yako..!

Hapa umevunja ukimya.
 
Kufufua mashirika ya Umma kama TTCL, Airtel kurudi serikalini, Reli ya Dar-Moshi nk.

Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni!
 
Back
Top Bottom