Mkuu tunazungumzia ujumla wa mambo, wewe uliyoyataja ni yale madogo madogo
Nimekaa TRA toka saa 3 hadi saa 4:30 pale Samora hawan network nilitaka ku renew leseni yangu ya udereva. Hata sasa nimempigia dogo nilimwacha pale bado hakuna network. So nchi hii bado sana pamoja na pambio zote mnazoimba.
 
Hata mimi nakuunga kidole cha kati
 
Kabla Ya Magufuli Pale Hospital Ya Mkoa Wa Ruvuma Nikifika Mapokezi Card Nilikua Nalipia Tsh. 1000. Baada Ya Kuja Serikali Ya Awamu Ya Tano Saizi Card Hiyo Hiyo Nalipia Elfu Tano.

Hongera Sana Serikali Ya Awamu ya Tano Kwa Kutujari Wanyonge.
 
Ni kweli mtoa mada, binafsi ninafanya kazi za ziada ambazo awali sikutaraji kuzisimamia mwenyewe. Muhimu tu ajenge mifumo na taasis imara tukianza na katiba bora, na kusimamia na kuiheshimu.Atakuwa kiongozi bora zaidi katika historia ya taifa letu.
 
Upo sahihi Mkuu
Tuendelee kumuunga mkono mh Rais Kwa uchapa kazi
Ni kweli mtoa mada, binafsi ninafanya kazi za ziada ambazo awali sikutaraji kuzisimamia mwenyewe. Muhimu tu ajenge mifumo na taasis imara tukianza na katiba bora, na kusimamia na kuiheshimu.Atakuwa kiongozi bora zaidi katika historia ya taifa letu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…