Nimepata fursa ya kuzunguka mikoa kadhaa mambo yamebadilika san,kila nilikopita watu wapo bize kweli kweli vijana kwa wazee
Huko shambani ndio usiseme kila kijiji unapita unakuta makundi kwa makundi wanaotesha mazao
Ile tabia ya watu kukaa bar saa moja asubuhi kwa kisingizio cha kutoa hangover hakuna tena, hangover inatolewa baada ya kazi
Toka Magufuli aingie madarakani sioni tena vijana wakikaa vijiweni na kucheza bao Muda wa kupambana
Huyu ndio Rais tuliyemlilia sisi Watanzania amebadilisha mtazamo wa Watanzania wengi mno wamekuwa wabunifu
Kabla ya Magufuli vijana waliokuwa wanaenda chuo walikuwa wakipata pesa za mkopo zinaishia kuzitapanya lkn sasa vijana wanaenda chuo wakipata mkopo hutunza pesa ili wajiajiri baada ya kumaliza chuo
Vijana wengi wasomi wamebadilika sana kimtazamo wabahili kweli kweli wanawaza maendeleo
Kumbe tulikuwa tunahitaji mtu mwenye uthubutu tu kubadilisha mind set za vijana
Ahsante Magufuli umetubadilisha wengi Endelea hivyo hivyo tuwe wachangamfu kwenye fursa kama wanigeria