Ungekuwa unajituma ungeona ugumu wenyewe, sababu bado unalishwa ni ngumu kuelewa
 
Nyingi kati ya hizo ni awamu ya nne jamani zilikamilika akiwa waziri wa ujenzi.Achane hizo mambo as if hayakufanyika huko nyuma.
 
Waungwana.

Mimi huwa nafanya mazungumzo sana na bodaboda, wapiga kiwi, akina mama ntilie, madereva wa uba, wazee na vijana mbalimbali kila nipatapo mwanya.

Swali langu huwa: Mnamuonaje Rais Magufuli?

Majibu
Magufuli ni jembe. Yule mzee ni noma na nusu yani ukileta mchezo anatumbua. Sasa hivi tunaheshimiwa na nidhamu imetamalaki. Dah! mzee kajenga barabara na shule bure. Sisi machinga na mamantilie hatunyanyaswi tena.

Majibu hayo ukiyapima yanaweza yasiwe ya kitaalam kivile lakini yanaashiria kukubalika kwa Magufuli na CCM. Nendeni kawahojini hawa watu. Msibweteke na hamasa mitandaoni. Hojini mpate majibu mapemaaaa ili msihangaike kutaabishwa kuingia barabarani kwa kigezo cha kuibiwa kura ilihali Upinzani hauuziki.

Msidanganywe bure. Afande Muroto alipata kuonya. Msipende kuchakaa.
 
Hao wanaiga mfano wa wajumbe. Wakiwa nje wanasifia ila kwenye kura hawakupi. Sasa hivi watu watafuata mfano wa wajumbe. Usiwe na wasiwasi.
 
Amefanya vizuri sana kwingine lakini kwa watumishi wake pale hajafanya kitu.
 
Na nashangaaa nguvu inayotumika kumsifia naona kama ni umbumbumbu tu sababu kama ni ujenz wa miundombinu hata huku nyuma imejengwa Leo hii unajenga barabara alafu afya , elimu , ajira vyote hoi kwaiyo tusifie kwa lip?
 
Hakuna cha msingi kilicho fanywa na ccm kwa watanzania zaidi ya kutuongezea ujinga na umasikini wa kutupwa
 
Rushwa bado, ila pamoja na hayo mazuri bado ameharibu kwenye demokrasia, bunge live, tunataka vyeti vya bashite na shutuma zake za ufisadi na uvamizi zifanyiwe kazi
Huu ni mwezi wa August hakuna kilichofanyiwa kazi ktk mapungufu yote uliyo yataja
 
Inafika mahali unashindwa kuelewa watanzania wanataka nini hasa?

Kama ni maendeleo yanaonekana kwa macho, tena hayana vyama pande zote za nchi watu wameneemeka.

Huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu imeboreshwa mara dufu, miundombinu ndio usiseme.

Treni ya Moshi - Arusha imerejea, ndege kadhalika meli na vivuko vimehuishwa.

Ninapotafakari watu hawa wanataka wafanyiwe nini nakumbuka maneno ya baba wa taifa mwalimu Nyerere kwamba ili nchi iendelee inahitaji Ardhi, Watu, Siasa safi na Uongozi bora.

Watanzania tunafeli wapi hadi kukumbatia siasa za kishabiki?

Au kuna watu wameamuwa kuwa na fikra za kipinzani tu? Maana hata shetani hapingi kila jema liletwalo na Mungu.

Niishie hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…