Mishahara waliongezwa kipindi kilee ndio wanaufanyia kazi sasa, kipindi kile walikula mishahara ya bure.[emoji2960][emoji2960][emoji2960], maisha magumu kwa asiejituma kupiga kazi, mimi mbeba mizigo hapa sokoni mbona maisha kawaida tuu. Hapo kwa WASTAAFU vyeti feki na wafanyakazi hewa waliAthiri ila imani tunayo patakaa sawa.[emoji39][emoji39][emoji39]
Mimi huwa nafanya mazungumzo sana na bodaboda, wapiga kiwi, akina mama ntilie, madereva wa uba, wazee na vijana mbalimbali kila nipatapo mwanya.
Swali langu huwa: Mnamuonaje Rais Magufuli?
Majibu
Magufuli ni jembe. Yule mzee ni noma na nusu yani ukileta mchezo anatumbua. Sasa hivi tunaheshimiwa na nidhamu imetamalaki. Dah! mzee kajenga barabara na shule bure. Sisi machinga na mamantilie hatunyanyaswi tena.
Majibu hayo ukiyapima yanaweza yasiwe ya kitaalam kivile lakini yanaashiria kukubalika kwa Magufuli na CCM. Nendeni kawahojini hawa watu. Msibweteke na hamasa mitandaoni. Hojini mpate majibu mapemaaaa ili msihangaike kutaabishwa kuingia barabarani kwa kigezo cha kuibiwa kura ilihali Upinzani hauuziki.
Na nashangaaa nguvu inayotumika kumsifia naona kama ni umbumbumbu tu sababu kama ni ujenz wa miundombinu hata huku nyuma imejengwa Leo hii unajenga barabara alafu afya , elimu , ajira vyote hoi kwaiyo tusifie kwa lip?
Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.
Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.
Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.
Mpaka sasa kafanya haya;
Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------
Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;
Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba
Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.
Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.
Miradi Mikubwa ya Maji :
Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga
============ emie emie posted: Kwa kweli Rais wetu kafanya makubwa sanaa..
Kila upitapo sasa hivi ni ujenzi unaendelea...Dar es Salaam kila kona Barabara ya Tandale-Sinza- Mawasiliano inajengwa
Madaraja yanajengwa
Upanuzi wa barabara kuu ya Ubungo hadi chalinze unafanywa
Daraja Kilombero miaka yote wapigaji walikuwa wanakula hela za wananchi kuwavusha ila sasa limejengwa
Flyovers zinajengwa
Miradi ya umeme inajengwa na miradi mingi ni kwa hela za watanzania wenyewe
Miaka yote maeneo ya Mbezi na kimara walikuwa hawapati maji japo yanapita njia hiyo hiyo lakini sasa maji yamefika mbezi, na bado wanaendelea kutandaza mabomba ili kupeleka maji. Awali waliokuwa wanakula hela za wananchi ni wenye miradi ya kuuza maji kwa magari. Ila sasa wananchi wamekombolewa.
Utendaji kazi umeimarika, sasa hivi kila mmoja anaona cheo akipewa ni kama kakalia kaa la moto..Yale mambo ya kupiga hela na kukaa ofisini kupiga usingizi yameisha watu ni kazi la sivyo unawajibishwa.
Madawa sasa yanapatikana hospitali, ile hali ya madawa ya hospitali yanapelekwa katika Pharmas binafsi imeisha.
Hospitali sasa za serikali ukienda mgonjwa anajaliwa sio kama ilivyokuwa awali.
Taasisi za serikali wafanyakazi wamekuwa wanawajibika ....hakika nidhamu imeimarika.
Kwa sasa taasisi za serikali zinajiendesha kibiasara bali si kihasara kama ilivyokuwa awali, ilikuwa ni ulaji tuu wa hela, upigaji dili, taasisi zinakufa, hakuna gawio kwa serikali, ila sasa zinatoa gawio...Hakika kila kitu ni usimamizi imara, ukicheka na kima utavuna mabua.
Awali watu walikuwa wanaulilia uongozi, hata wasio kuwa na elimu walikuwa wanagombea kupata uongozi, sasa uongozi umekuwa mgumu sababu kama wewe si muwajibikaji una ndoto za kupiga tuu, hupati nafasi, Uongozi umekuwa una hadhi kwa sasa.
Binafsi nimefurahishwa na kasi ya Rais Dkt. Magufuli. Naamini wapo pia wengi wanaoungana nami katika furaha hii. Rais Magufuli ameanza kwa kasi ambayo kama ataimaintain, Tanzania haimalizi miaka mitano itakuwa tayari ni nchi yenye kipato cha kati. Hata hivyo wapo baadhi yetu ambao wanakejeli...
Rushwa bado, ila pamoja na hayo mazuri bado ameharibu kwenye demokrasia, bunge live, tunataka vyeti vya bashite na shutuma zake za ufisadi na uvamizi zifanyiwe kazi
Inafika mahali unashindwa kuelewa watanzania wanataka nini hasa?
Kama ni maendeleo yanaonekana kwa macho, tena hayana vyama pande zote za nchi watu wameneemeka.
Huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu imeboreshwa mara dufu, miundombinu ndio usiseme.
Treni ya Moshi - Arusha imerejea, ndege kadhalika meli na vivuko vimehuishwa.
Ninapotafakari watu hawa wanataka wafanyiwe nini nakumbuka maneno ya baba wa taifa mwalimu Nyerere kwamba ili nchi iendelee inahitaji Ardhi, Watu, Siasa safi na Uongozi bora.
Watanzania tunafeli wapi hadi kukumbatia siasa za kishabiki?
Au kuna watu wameamuwa kuwa na fikra za kipinzani tu? Maana hata shetani hapingi kila jema liletwalo na Mungu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.