Sina maneno mengi
Ila kwa haraka haraka naona watanzania wengi hasa walionyimwa elimu wanavyomshabikia Magufuli na kuhisi ataweza kuifanya Tanzania kama nchi moja wapo zenye maendeleo Africa ambayo itafanana na baadhi ya nchi za ulaya
Mmepigwa fix suala la makinikia mkadanganywa kwamba fedha tutakazolipwa na barrick zinatosha kwa kila mtanzania kununua Noah mkashangilia
Hivi kwa viongozi wa kiafrica mnadhani wanaweza kubadilisha nchi zao zikawa kama ulaya? Wengi wamejawa na uchu wa madaraka ,ubabe,nongwa,visasi na fitna ,hawataki kuwaunganisha watu wao wakafanya mambo ya msingi kwa maendeleo ya nchi
Ndo mana waafrica tuna umaskini wa kutupwa kutokana na tabia mbovu,ulaghai,ubinafsi na undugulization wa viongozi wa africa
Wale waSouth mnawaona wana maendeleo ya viwanda,majengo na miundombinu mizuri ya barabara, reli n.k ni kutokana na makaburu kuitwala south na kuona ni potential kwao wakaijenga,katoka Mzee madiba mzalendo kaingia Thabo mbeki kazingua,kaja Zuma ndo hawamtaki kabisaaaa
Sasa hapa Bongo sijaona kiongozi mzalendo wote ni kutafuta kiki kama kweli kiongozi mkuu ni mzalendo aweke katiba mpya itakayoruhusu kunyonga rais akizingua wakati wa utawala wake,iruhusu bunge limkatae rais na kumwondoa madarakani,iwepo katiba ya kufukuza wabunge wote wazembe yani wananchi wawe na mamlaka ya kumfukuza kazi mbunge wao,iwepo katiba ya kupunguza madaraka ya rais,iwepo katiba ya kutengua kauli za rais juu ya maamuzi Fulani
Nchi zote zilizoendelea zina katiba za namna hii so wabongo kuanza kumshabikia JPM eti ni mzalendo upuuzi kwa katiba hii mbovu,kwa elimu na ujinga wa watanzania ni upuuzi ,bado tunasafari ndefu hatuwezi kumshabikia mtu ambae ana kinga hata akivurunda kwake poa tu.
NB: Nakaribisha povu na kukosolewa