Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2021
Kitu ambacho kinaipa asilimia kubwa ccm mpaka sasa ni kuwekeza nguvu zao kuwakabili chadema tu
Hapo nawapa asilimia 50 kwa kuwatumia police tunaowalipa kwa kodi zetu
Lakini kiuhalisia hakuna ahadi hata moja iliyofanywa au kutimizwa na ccm

Tanzania ni ile ile aliotuachia jakaya kikwete

Haijapiga hatua yoyote
Cdm ni chaka la ukabila na ukanda. Toa takwimu labda tutakuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RAIS Dk John Pombe Magufuli anaendelea kutekeleza kwa kasi ahadi zake alizowaahidi wananchi wa Tanzania wakati akiwaomba kura wakati wa kampeni mwaka 2015.

Katika mkoa wa Kigoma moja ya ahadi zake kwa wananchi wa Mji mdogo wa Nguruka wilayani Uvinza, Rais Magufuli aliwaahidi wananchi hao kuwa ataitatua shida ya maji ya muda mrefu inayowakabili.

Rais Magufuli aliwahakikishia wananchi hao kuwa kupitia mto Malagarasi ambao ni jirani tu na mji huo (Kilomita 18 kutoka mji wa Nguruka) atawajengea mradi mkubwa wa maji ambayo yatatumika katika Wilaya yote ya Uvinza na maeneo jirani.

Hatimaye leo Rais Magufuli ameitekeleza ahadi yake na kuweka jiwe la msingi la mradi huo mkubwa kabisa katika miradi iliyopo mkoani Kigoma. Kwamujibu wa Rais Magufuli mradi huo utakamilika Desemba 31, 2017 na kuanza kuwahudumia wananchi ambao wana hamu kubwa ya kuona mradi huo ukianza kuwapatia maji.

Hizi ni juhudi za Rais za kuhakikisha kuwa wananchi wa Tanzania wanafaidika na rasilimali za nchi yao ambapo amefanikiwa kulinda rasilimali za nchi na kupambana bila kuchoka na wabadhirifu wa mali za umma, wala rushwa na mafisadi.

d61cad703c3cf95bb370738df32f1442.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili ni nywele kila mtu ana zake; nani alikuambia kwamba mahakama ya mafisadi inajengwa? Hiyo ni division tu ya mahakama kuu ya Tanzania na kumbuka mahakama siyo majengo, mahakama inaweza kuendeshea shughuli zake hata hotelini.
Whether physically built ama not, nani keshahukumiwa tangia utumbuaji majipu uanze??
 
Haiwezekani kuongelea mafanikio wakati anaua upinzani na anatumia kila njia kuhakikisha demokrasia haipo Tanzania. Vipi tutaongelea mafanikio wakati ni chama chake kimetufikisha hapa na mafissadi wakubwa na wavunjaji sheria na katiba wamo kwenye chama chake. Hatuwezi kuongelea mafanikioa wakati ameweka watu wake wa karibu kuwa ndio watendaji wakuu serikalini. Ni kichekesho kuongelea mafanikio kwani kipimo cha mafanikio ni kiyu gani.
 
Tuonacho ni makelele, majigambo, vitisho, ubabe dhidi ya upinzani. Sijaona hasa kitu kilichofanywa na the over decorated Magu mpaka sasa. Kwa misifa anayo mwagiwa tulitegemea tuwe tunaona vitu vikubwa proportionally.

Nieleweke hivi pamoja na madudu mengi, kikwete alituachia udom, Nelson Mandela, daraja la kigambon, nk. Huyu zaidi ya kupiga kampen akizunguka kila sehemu nini kafanya mpaka sasa. ?
 
Tumeshakuwa dona kantri.

Deni la taifa ni 50tr, akeshia tunawadai 420Tr. Tumebakiza chenji kama 370tr. Bajeti yetu ni kama. Trilion 30 tu kwa mwaka.,

So bajeti imelipiwa kwa miaka 10 na chenjii imebaki kama trilioni 70. Hizi sasa tutaanza kukopesha vinchi vidogo vidogo vyenye madeni afrika, ulaya na asia.
Hapo bado hatujakusanya kodi na hatujaenda kwa wezi wengine wa madini kudai kilicho chetu!

Achana na Ngosha kabisa! Ana ndoto za hatari!

Mkwamo upo kwenye uhalisia tu! Je trilioni 420 zitakuja?
 
Kafanya vingi mkuu, tena vizuri sana lakini pia kuna mabaya amefanya tena vibaya sana. Kwa mazuri yake tumpe sifa ila kwa mabaya yake tuendelee kumsema bila woga.
 
Huwezi kuona kama hufatilii kinachoendelea wizara nyingi,na sekta kibao.Halafu hata angefanya nini kama ni mmoja wa Anti-JPM huwezi kuona,November 2015 mpaka July 2017 ni miezi 20 tu sawa na mwaka mmoja na miezi 8 tu.Mwaka mmoja na miezi nane ya JK namaanisha November 2005 hadi July 2007 ilikuwa inakaribia kulipuka skendo kubwa sana nchini RICHMOND kinara akiwa E.N.L waziri mkuu wa zamani,kipindi hicho akiwa kwenye PEAK MODE ya wizi wa mali za umma.Jambo ambalo halitokei mwaka huu wala mwaka kesho awamu hii.Ukilinganisha linganisha kwa style hiyo,kingine ukishinda humu kwenye propaganda huwezi ona kinachofanywa na serikali hii.
 
kulifanya kabila LA kisukuma kuwa ndo wenye nchi kabila zingine kuhamishiwa kenya
 
Back
Top Bottom