jacob mhina
New Member
- Aug 5, 2018
- 1
- 0
Lazima use critic sio unajipendekeza tu!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mmmmh..!Nakumbuka kuna Mheshimiwa wakati anatoka Madarakani Alisema kwa utani Mengine Nayaanza mimi ila atae kuja kumalizia ndie atakae sifiwa..Kwa hiyo Naomba nae umpe Heshima yake tu kwa kuanzisha mbio.[emoji35] [emoji35]![]()
Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.
Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.
Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.
Mpaka sasa kafanya haya;
Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------
Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;
Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba
Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.
Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.
Miradi Mikubwa ya Maji :
Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga
za marhaniUna hakika? 2020 Magufuli atapata 80% ya kura zote kwa hivyo jiandae kuhama.:[emoji2]
Kwa kweli amefanya makubwa kwa DSM MZA naona yeye ni raisi wa huko. Mimi naishi Kibondo sijaona hiyo barabara iliyojengwa kuunganisha KIBONDO KIGOMA KALIUA PENGINE IMEJENGWA KIMOYOMOYO/kisiasa Lakini kiuhalisia haipo![]()
Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.
Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.
Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.
Mpaka sasa kafanya haya;
Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------
Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;
Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba
Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.
Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.
Miradi Mikubwa ya Maji :
Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga
Prof ni mara ya tatu sasa unaDipu lakini line iko busy,ipo siku atapokea!
Si kweli. Hana mahusano mazuri na wapinzani. Anachuki mbaya dhidi ya wapinzani. Anavisasi na kutaka maendeleo ya harakaharaka kwa kutegemea nguvu zake mwenyeweTangu mwaka 1992 tulipoanza siasa za vyama vingi, Tanzania hakujawahi kuwapo kwa mshikamano wa vyama vya siasa, kila chama na mambo yake isipokuwa UKAWA tu ndiyo iliyokuwa karibu na mshikamano dhidi ya CCM. Uhasama baina ya Vyama vya upinzani na CCM umekuwapo miaka yote!
Afadhali Magufuli ameteua viongozi wa kutoka Upinzani pia: Kafulia, Mkumbo na Mngwila siyo wana CCM!.
In fact Magufuli ana uhusiano mzuri sana na wapinzani hadi anawateua katika serikali yake; hakuna serikali iliyowahi kuwa na wateule wa kutoka Upinzani ila hii tu. Inawezekana anapoteua kutoka wapinzania basi wale wasiopata kuteuliwa wanachukia sana na kudaia anawagawa. hebu angalia: Slaa, Mkumbo, Mrema, Mghwila, na sasa Kafulia wote hao waliteuliwa wakiwa siyo wana CCM! Sijui wewe unataka ushirkiano wa namna gani kama siyo kiutendaji. Anapowaziba midomo ya uwongo hao wapinzani basi wanachukia na kudai hashirikiani nao; mnataka awakubalie kwa kwa huo uwongo na uzushi wa kila siku. Majuzi tu wamesikiaka wakizusha eti trilioni 1.5 zimepotea wakati CAG hajaziona je wao waliziona katika mahesbau yapi; ndio wanaokagua vitabu vya serikali au ni CAG?Si kweli. Hana mahusano mazuri na wapinzani. Anachuki mbaya dhidi ya wapinzani. Anavisasi na kutaka maendeleo ya harakaharaka kwa kutegemea nguvu zake mwenyewe
Si kweli kwamba anamahusiano mazuri na WAPINZANI. Ana mahusiano mabaya sana. Kwanza hataki challenge yoyote ile kutoka sehemu yoyote ile. Halitakii mema taifa kwenye mambo ya umoja na mshikamano wa kitaifa na kimataifa.In fact Magufuli ana uhusiano mzuri sana na wapinzani hadi anawateua katika serikali yake; hakuna serikali iliyowahi kuwa na wateule wa kutoka Upinzani ila hii tu. Inawezekana anapoteua kutoka wapinzania basi wale wasiopata kuteuliwa wanachukia sana na kudaia anawagawa. hebu angalia: Slaa, Mkumbo, Mrema, Mghwila, na sasa Kafulia wote hao waliteuliwa wakiwa siyo wana CCM! Sijui wewe unataka ushirkiano wa namna gani kama siyo kiutendaji. Anapowaziba midomo ya uwongo hao wapinzani basi wanachukia na kudai hashirikiani nao; mnataka awakubalie kwa kwa huo uwongo na uzushi wa kila siku. Majuzi tu wamesikiaka wakizusha eti trilioni 1.5 zimepotea wakati CAG hajaziona je wao waliziona katika mahesbau yapi; ndio wanaokagua vitabu vya serikali au ni CAG?
Kuna tofauti ya nidhamu na hofu je rushwa kakomesha vp? Umesahau 1.5 mi naona kiki tu kufanya kazi na makemera wakati bunge limefichwaMaendeleo ya vitu hata jakaya ameyafanya Magufuli cha maana alichofanya ni kukomesha Rushwa na kuleta nidhamu
Lugha mkuu anatuzugaTuacheni mihemko tumsifu pale alipopatia maana nchi ilikuwa imeoza.
Fikiri mkuu hajaenda hata dubai kuosha macho kwa Uzalendo wake.
Haha inachekesha kwelikweliujenzi wa chato international airport
afu ujue unazingua sana we jamaa inama SGR hujaiona ama? mbona unasahau vitu muhimu kamaView attachment 837432
Kama ambavyo Watanzania tunavyomkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kusaidia ukombozi wa upatikanaji wa uhuru ama kama ambavyo Hayati Moringe anavyokumbukwa kwa mapambano ya ubadhirifu wa mali za umma, pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anazidi kujenga historia ya kipindi chote isiyofutika kutokana na utendaji, uchapakazi na uzalendo wake kwa Taifa.
Haya hapa ni baadhi ya Mambo ya kihistoria na yenye heshima kubwa kwa Taifa ambayo Rais Dkt. Magufuli aliyoyafanya;-
*(i) Kuhamia Dodoma*
Wazo la Serikali kuhamia kwenye makao makuu ya nchi mkoani Dodoma liliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere mwaka 1973 lakini lilishindwa kutekelezwa katika awamu zote. Si awamu ya kwanza, wala ya pili, ama ya Tatu au ya nne bali limeweza kufanikiwa kwenye utawala wa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli. Leo hii karibia Serikali yote imehamia Dodoma. Wizara, taasisi na idara za Serikali, Waziri Mkuu wameshahamia Dodoma. Mwishoni mwa mwaka huu Rais Magufuli naye atahamia Dodoma. Iliasisiwa na Mwalimu Nyerere, ikahaidiwa kwenye ilani ya uchaguzi, imekuja kutekelezwa vyema na Rais Magufuli. Hii ni historia isiyofutika ya uthubutu, uzalendo alionao Rais Magufuli.
*(ii) Ujenzi wa Miundombinu*
Hili halina ubishi kwa asilimia kubwa kabisa miundombinu ya nchi hii imejengwa chini ya usimamizi wa Dkt. Magufuli toka alipokuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Waziri wa Ujenzi na sasa Rais wa nchi. Hauwezi ukazungumzia uwepo wa mitandao ya barabara nchi nzima pasipo kumtaja Rais Magufuli; hauwezi kuzungumzia uwepo wa madaraja makubwa ya kisasa kama ya Daraja la Nyerere, Daraja la Mkapa pasipo kumtambua mchango wa Rais Magufuli. Leo hii nchini tunajivunia uwepo wa flyovers. Rais Magufuli ameonyesha uwezo na heshima kubwa ya ujenzi wa Miundombinu nchini ambayo imekuwa msaada mkubwa wa kimawasiliano, usafirishaji wa Watu na mizigo, kukuza utalii, kuimarisha shughuli za kibiashara na kuongeza mapato ya nchi.
*(iii) Kulifufua Shirika la Ndege*
Tangu mwaka 1977 nchi yetu ilikuwa na shirika la ndege linalosua sua na linalojiendesha kihasara kubwa. Mara baada ya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli imefanikiwa kununua ndege mpya 7 na mpaka sasa zimeshawasili ndege mpya 4 ikiwamo ndege kubwa aina ya Boeing 787-8. Wale baadhi wanaosema ndege si kipaumbele wala muhimu kwa Watanzania inabidi watambue Leo hii makusanyo ya mapato ndani ya Shirika la ndege (ATCL) yametoka Tsh. Milioni 700 mpaka kufikia Tsh. Bilioni 4.5. Hii ndio faida ambayo Watanzania tumeipata ya kuwa na kiongozi mwenye maono na mtazamo wa mbali zaidi, Rais Magufuli.
*(iv) Ujenzi wa Stiegler’s Gorge*
Utawala wa awamu ya kwanza uliokuwa ukiongozwa na Mwalimu Nyerere ulikuja na wazo wa kujenga Stiegler’s Gorge mnamo mwaka 1981 lakini umeshindwa kufanyika mpaka awamu hii ya 5 inayoongozwa na Rais Magufuli umeamua kufufua na kuliendeleza wazo hili. Mradi wa Stiegler’s Gorge kupitia Mto Rufiji utafanikiwa kuzalisha Megawattz 2100 utakapo kamilika. Ukamilifu wa mradi huu utajenga uhakika wa umeme nchini, utashusha bei ya umeme nchini na pia utamjengea Rais Magufuli heshima kubwa isiyofutika.
*(v) Mapambano dhidi ya Rushwa na ufisadi nchini.*
Rais Magufuli ameingia kwenye historia ya kiongozi ambaye Serikali anayoiongoza kuwa na mapambano ya dhahiri ya rushwa na ufisadi nchini. Tumeshuhudia Mafisadi Papa ambao walikuwa hawashikiki wala kukamatika wakipandishwa Mahakamani. Katika miaka ya nyuma ilikuwa suala gumu sana kwa Watuhumiwa “Mapapa” kuguswa tu, achilia mbali kupandishwa Mahakamani. Haya ni mapambano ya wazi wazi ya Serikali ya Rais Magufuli ya vita dhidi ya rushwa na ufisadi nchini. Leo hii Tanzania imepanda kwa nafasi 13 katika mwaka 2016 na 2017 na pia ikishika nafasi ya pili (2) kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
*(vi) Uwazi wa taarifa na udhibiti wa rasilimali za nchi*
Tumeshuhudia Serikali ikiweka uwazi kwenye mikataba na uchunguzi wa rasilimali za Taifa na kuweka makubaliano mapya yenye tija Mathalani tumeona uwazi wa sekta ya madini ya dhahabu, almas na Tanzanite ambapo Taifa tumeona namna ambavyo tulivyokuwa tukiibiwa na Serikali kuweka mikakati mipya ya kutokuibiwa tena. Kama haitoshi tumeshuhudia wawekezaji wakibanwa vilivyo juu ya mikataba isiyokuwa na tija kwa Taifa. Ni Serikali ya Rais Magufuli iliweka uthubutu wa kuwabana wawekezaji wa madini wa ACACIA iliyozaa matunda kwa Serikali ya Tanzania kumiliki asilimia 16 ya hisa katika makampuni ya uchimbaji wa madini, Serikali kupata gawio la faida ya madini ya asilimia 50 kwa 50. Yote haya yamewezekana kwa sababu ya uzalendo wake Rais Dk. Magufuli
*(vii) Ujenzi wa Bomba la Mafuta*
Serikali ya Rais Magufuli imefanikisha vilivyo kushirikiana na nchi ya Uganda kujenga Bomba la Mafuta linalotoka nchini Uganda mpaka Tanga nchini Tanzania. Ujenzi huo wa bomba la mafuta utazalisha ajira nchini na utaongeza pato la Taifa. Hayo yote yamefanikiwa kutokana na Serikali ya Rais Magufuli kuzidi kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi nyinginezo.