Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2021
Ameondoa watumishi hewa na wenye vyeti feki lakini ametengeneza watumishi hewa wenye vyeti halali. Alipo teua wagurugenzi zaidi ya 160 wapya huku wale wa zaman wakiendelea kula mshahara ule ule wa ukurugenzi, kwa hyo cheo kimoja analipa mara mbili, hili n kosa na ndio maana anakosa pesa za maendeleo yanayo mgusa mwananchi moja kwa moja.

Tatizo lingine la usiri wa serikali yake juu ya rasilimali za nchi, kuzuia bunge lisirushwe mbashara huu ni usiri na uwoga wa kuogopa kuona serikali yake inakosolewa

Kuingilia mamlaka ya mihimili mingine, kwa mfano kuingilia bunge na kusema bajet hii isipopita atavunja bunge na wabunge wengine hawatorud, huku ni kuingilia muhimili wa bunge katika uhuru wake wa kufanya maamuzi

Kuwa na double standard, huku anatumbua kule anafunikia jipu na kuliacha kana kwamba halioni.

Yako mengi mno ambayo yanafanywa kinyume cha katiba kama kubaka democrasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
10102ac521314716b0cdeb7f1e57ec04.jpg


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga
Ukiondoa esigiara na stigilas goji ni kitu gani jiwe amefanikisha??jibu tafadhali!
 
Hizo milioni 50 kila kijijini wala siwezi kumkumbusha maana najua hawezi kutoa.
Maendeleo hayaletwi kwa kutumia ubabe,dharau, kiburi, jeuri, nguvu , kwani kazi anafanya peke yake?
Watu kama wewe bila ubabe hakuna lolote. Nchi hii bila ubabe ni kulalamika tu. Mtu mwenyewe hata unaiba hadi sindano !!
 
Yote hayo yamemsaidia vipi mwananchi alieko Tandahimba?
Unaambiwa kuna barabara ya kwenda Tandahimba. Unavyouliza yote hayo yanamsaidia nini mwananchi wa Tandahimba ni upuuzi mtupu. Kitu cho chote kinachofanyika hakiwezi kuwasaidia moja kwa moja Watanzania wote kwa ujumla. Acha utoto. Tumuunge mkono Rais wetu katika jitihada zake za kuendeleza nchi.
 
1)uwezeshaji wa kupotea kwa pesa 1.5trillion bila mtu kuhoji
2)uendelezaji wa kazi nzuri ya kusaidia watu kuhama vyama na kupata tena vyeo walivyokuwa navyo bila mtu kuhoji
3)viwanda 3000+ kuanzishwa na uchumi kupanda kwa kasi nzuri wapinzani na wananchi kumuunga mkono
4)polisi kusimamia haki katika vituo vyetu vya uchaguzi na kulinda amani mitaani
Uwanja wa ndege chato
 
Tatizo kubwa la waafrika tumejenga dhana kwamba raisi na Viongozi wengine tuliowachagua wanatusaidia wananchi, siyo kwamba wanatimiza majukumu yao. Uongozi ni ajira, kwani unalipwa na kodi za wananchi. Yampasa raisi wetu, Viongozi na watanzania watambue kuwa raisi ni mtumishi, siyo mfalme. Kufanya hili au lile ni jukumu lake. Endapo tutalazimishwa kusifu, basi tutambue michango ya watendaji wakuu na wafanyakazi wanaofanya kazi kwa bidii na kuleta maendeleo katika jamii zetu. Tuwe wakweli, sifa siyo za raisi peke yake. Raisi anapaswa kukosolewa zaidi ili ajitume zaidi kwa waajiri wake ambao ni raia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi namshukru kwani Barbara ya mtaani kwangu Bombamzinga -Tabora imewekewa lami kwa Mara ya kwanza endelea hivyo mheshimiwa wananchi Wa mtaani Sana juju bal
 
Hivi jaman tukiachana na masuala ya kujenga jenga pesa si angepeleka na sector nyingine. Ili mzunguko wa pesa uwe mkubwa.

Maana ukifuatilia makampuni mengi ya ujenzi ni ya foreigners so pesa haibaki nchini. Hivyo uchumi kuzidi kudorora zaidi
Hapana na ndiyo! Hapana kwa sababu hii miradi ya ujenziinatoa fursa za kazi au ukipenda ajira; haijalishi ni kwenye ngazi au kiwango gani, lakini wananchi wetu, Watanzania wa kawaida wanapata kazi huko. Kazi hizo zinaweza kuwa zile za moja kwa moja (direct employment) au zile zisizokuwa za moja kwa moja (indirect employment). Nadhani unanielewa, kwa hiyo pesa, hata kama ni chache kiasi gani zitabaki humu nchini! Hicho kiasi kinacho kwenda nje ni kadri ya mikataba ilivyo. Hii ndiyo ninyi mnaita win - win situation! Usitarajie wajenge tu na wao wasipate cha kurudisha kwao; fahamu kwamba haya ni makampuni yana ofisi na staff wengine huko na ni halali wapeleke pesa kwao!
 
Ulietoa mada,unaonekana bado upo karne ya 20 na sio ya 21..Why?
*Nikiangalia,Trump na JPM wameingia madarakani muda sawa....yeye Trump,ameweza kuzalisha kati ya ajira 157,000 kila mwezi,huku kiwango hicho kikitarajiwa kuongezeka hadi 190,000 kwa kila mwezi..kwa takwimu za wachumi na maswala ya jamii.
*Trump ameweza kushusha ukosefu wa ajira kwa 3.9% kutoka 5%,na inaendelea kupungua...UDSM pale wanamaliza watu 5000 na wote HAMNA KAZI,Mitaani vijana hawaelewi cha kuwapa riski ya siku...kuna nchi ambazo hayo ni ‘hadithi za kusadikika’
*Trump hakuishia hapo,ameweza kuongeza ujira kwa lisaa kufikia $27.5 ikiwa ni ongezeko kwa 0.3%,na kufanya 27% kama ongezo la kipato kwa saa.
*Na pia Mfufumuko wa bei na riba vimedhibitiwa kwa 1.75%-2%......Sasa kati ya watu hawa wawili NANI AMEFANIKIWA?
 
Back
Top Bottom