Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa Kiwanda
cha kutengeneza mabomba Vingunguti jijini Dar
es Salaam, alieleza jinsi alivyoshangazwa na
Watanzania walioshangilia mkasa ulioikumba
ndege hiyo ambayo imenunuliwa kwa kodi za
wananchi.
“Wasaliti walikuwapo tangu enzi Mungu
alipoumba dunia akatengeneza malaika, wengine
wakagoma ndiyo mashetani wanaotusumbua
huku, kwa hiyo wapinzani hawawezi wakakosa,”
alisema Rais Magufuli. “Inashikwa ndege ambayo
imenunuliwa na baba yake na mama yake, yeye
anashangilia anashindwa kuelewa kuwa ile ni
fedha ya baba yake na mama yake, kuelewa ni
kodi ya Watanzania maskini, kwa kutokujua kwa
kutumiwa anashangilia afadhali imeshikwa
ndege,” alisema. Aliwataka waelewe kuwa ndege
siyo ya Magufuli bali ni ya Watanzania. “Mimi
nikifa leo ndege itabaki pale, inawahudumia
wengine wanawahisha wagonjwa, Kigwangalla
(Hamis) anaitwa waziri kwa sababu ya watalii,”
alisema. “Unaweza kujua huyu amepungukiwa
kichwani, siyo mtu wa kawaida amepungukiwa
kichwani, wewe uwe na duka kijijini liibiwe mtoto
akashangilie, utamuona huyu mtoto ana kasoro
kwa hiyo wenye kasoro wapo tuwasamehe,
tuendelee kuwaombea.”“Baba Askofu muendelee
kuwakemea mashetani yawatoke kichwani mwao,
Masheikh muwasomee dua wakatambue Tanzania
ni makabila yote, vyama vyote na kwamba
maendeleo hayana vyama tunataka tuitoe nchi
ilipokuwa iende mahali fulani nilishawaambia hii
ni donor country.”
Alisema kupitia kodi za wananchi zimejengwa
hospitali 352, pia Sh. bilioni 23.863 kila mwezi
zinatumika kwa ajili ya kugharamia elimu ya
watoto.
Alisema katika mapambano wasitegee kupendwa.
Lazima kujitegemea kwa nguvu za nchi.