Hii mada inachekesha, maana bajeti ya Tanzania inategemea misaada ya hawa wazungu ili kukidhi huduma za afya, hivyo ina maana wazungu watume misaada kisha waje kupigana vikumbo na wanaokusudiwa kunufaika kwa hiyo misaada, such an irony.
Ni kama umkute omba omba barabarani anahangaika akiomba, umpe hela kisha umfuate kitaani ukang'ang'anie chakula atakachonunua kutokana na vipesa vyako. Hiyo ni kukosa huruma, kwa hapa nawalaumu wazungu, wanafaa wafahamu Watanzania wanateseka sana, hizi huduma hawana za kutosha, ikumbukwe kuna madaktari wao wamesota kitaani hawana ajira, maana ndio nchi ya kwanza kusikia ina madaktari mitaani waliokua wanaotea kuja Kenya kushikilia nafasi ya hawa wetu waliokua wanagoma.