Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2021
Hela ya kuajiri mwanao au mtoto wa ndugu yako, ndio inatumika kuendesha hili shirika huko faida yake hujawahi ambiwa ni kiasi gani kama ipo.

Hela ya kuongeza mshahara wa mkeo ili akusaidie kulea wanao au akopesheke zaidi benki mfungue kamradi kuwasaidia ndio inatumika kununua hizi ndege huku ukaguzi wa mahesabu ya hili shirika tunaambiwa hata CAG kwa sasa hawezi kukagua kisa tumelihamishia vote 2000!!!
Utaolewa wewe
 
Ninakupongeza kwa kuamua kwa dhati kulifufua shirika letu la Ndege.Penye ukweli lazima usemwe inawezekana wapo watakaobeza jitihada zako, lakini wanapaswa kukumbuka kuwa hatukuwa na ndege za serikali kwa muda mrefu.

Kifupi sana kama taifa kuna mambo mengi ya kufanya lkn hatuwezi kuyafanya yote kwa pamoja hivyo kuna Yale ambayo yamepewa kipaombele kama kuimalisha shirika letu la ndege.

Hongera tena Rais kwa maamuzi magumu yenye tija kwa taifa letu siku za usoni.Mungu ibariki Tanzania,Mungu mbariki Rais wetu Dr.John Pombe Joseph Magufuli.
Issue siyo waliokuwapo hawakutaka bali walitaka kufuata taratibu za uidhinishwajj bajeti za nchi na Sheria ya Manunuzi. Vilevile walikuwa wanaangalia Vipaumbele muhimu kama barabara, elimu, afya na maji.

Kama nao wangekuwa wameteua wapwa zao kuwa Paymaster General na kulifanya Bunge kuwa muhuri wa maamuzi, pengine tungekuwa na ndege nyingi kuliko hata South Africa.

Watanzania siyo wajinga wanajua kuwa msukumo mkubwa wa kununua ndege bila kufuata taratibu ni kupata rushwa au commission. PERIOD

Subiri awamu ya 6 ndiyo mtajua ukweli
 
Ni kweli tumeona mafanikio ila mafanikio mengi yanakuwa upande ya watu wenye uwezo tu..kuna jamii mida huu inapata janga la maji na wakati huo huo serekali kwa hela zetu inanunua ndege sasa hapo unakuta tatizo sio maendeleo ila pia ni kuumia kwa raia
 
Kile kiwanda chenu cha kupika majungu na upotoshaji kimebaki uchi sasa, mmebaki tupu sasa
Mambo ni mengi yenye maana yapo hapa tunaweza kuyajadili na sio hili lako kiongozi punguza gadagada mfeme katika siasa
 
Hii ndiyo Serikali ambayo mwananchi tuliisubiria miaka mingi.
Kazi ya Serikali ni kutatua kero na changamoto mbalimbali za mwananchi.
Tumeona Huduma ya afya ikiboreshwa maradufu,maji,umeme na miundombinu ya barabara ikiendelea,pembejeo za kilimo
 
Ni kweli tumeona mafanikio ila mafanikio mengi yanakuwa upande ya watu wenye uwezo tu..kuna jamii mida huu inapata janga la maji na wakati huo huo serekali kwa hela zetu inanunua ndege sasa hapo unakuta tatizo sio maendeleo ila pia ni kuumia kwa raia
Katika kutatua shida za wananchi ...huwezi kusolve shida zote kwa wakati mmoja....ndiyo maana Serikali inatatua changamoto kwa awamu kulingana na bajeti hapa Serikali inajaribu kubeba kila jambo kwa umhimu wake kwa awamu....hii Serikali ni ya awamu ya 5 mbona hizo kero hazikutatuliwa Huko nyuma?
Kuna sehemu sasa ndani ya nchi ukosefu wa maji imekuwa historia na Serikali inaendelea na adhima yake ya kumtua mama ndoo, Umeme imepeleka mpaka vijjn Huko,afya ndiyo usiseme ,barabara za kihistoria zingine toka Tanzania iumbwe hazikuwa kufikiriwa kujengwa lakini Leo tunajenga.
Serikali awamu ya 3,4 na 5 zimenikuta MTU nnayejielewa na nnaona!
Serikali ya awamu hii ya tano inakitu extraordinary kuzidi hizo hizo zingine.
Hata kwenye familia sidhani changamoto zinaisha ukianza na hili linakuja hili na kesho linabiku jingine na hiyo ndiyo maisha ya binadamu.
Na kwa muono wa siasa hasa kwa wapinzani wako watakukejeli tu!wataona hufai na kila aina ya majina utaitwa ili uonekane hujafanya kitu...au uambiwe huna kipaumbele na hiyo ndiyo siasa.
 
Huyu mtu ni mzalendo hasa. Wapiga dili hawana hamu, mafisadi yamepoteana, wauza madawa ya kulevya chali.

Wakulima wanafurahia, wamachinga wanafurahia, mamantilie wanafurahia.

Wanafunzi wanasoma bure. Ukienda TRA hakuna kuzungushwa, mikopo chuo kikuu ya kutosha.

Muungano umeimarika. Midege imependezesha anga ya Tanzania,
kufuzu Kombe la Africa kwa Taifa Stars mara mbili mfululizo.


Wacha waisome namba eeee
 
Mnahangaikaaaa lakini ukweli ni kwanba watanzania wamegoma kutawaliwa na hiyo kitu.
 
Huyu jamaa ni wa kum-ignore. Nilisema jiwe ana timu ya watu wanalipwa kabisa ambao kazi yao ni kuhandle social media zote na kusawazisha propaganda 24/7. Huyu anaweza kua moja wao. Wapo wengi na wana account kibao
 
Huyu mtu ni mzalendo hasa
Wapiga dili hawana hamu,mafisadi yamepoteana,wauza madawa ya kulevya chali

Wakulima wanafurahia,wamachinga wanafurahia, mamantilie wanafurahia

Wanafunzi wanasoma bure
Ukienda Tra Hakuna kuzungushwa
Mkopo chuo kikuu yakutosha
Muungano umeimarika
Midege imependezesha anga ya Tanzania
Kufuzu kombe la Africa kwa Taifa stars mara mbili mfululizo


Wacha waisome namba eeee
Kiki zingine hazina hata maana. Mtumie ujumbe akupatie Kitengo huku sidhani kama anapitaga.
 
Huyu mtu ni mzalendo hasa
Wapiga dili hawana hamu,mafisadi yamepoteana,wauza madawa ya kulevya chali

Wakulima wanafurahia,wamachinga wanafurahia, mamantilie wanafurahia

Wanafunzi wanasoma bure
Ukienda Tra Hakuna kuzungushwa
Mkopo chuo kikuu yakutosha
Muungano umeimarika
Midege imependezesha anga ya Tanzania
Kufuzu kombe la Africa kwa Taifa stars mara mbili mfululizo


Wacha waisome namba eeee
Ganja bhana
 
Back
Top Bottom