Mafanikio ya Rais Magufuli 2015 - 2021
.
Siku zinakwenda mbio sana ila hatuna budi ku endelea kumuunga mkono Magufuli

[emoji3502]Elimu bure

[emoji3502]Kaliimarisha Shirika la Ndege [Atcl]

[emoji3502]Kaboresha Miundombinu Reli, barabara mjini na vijijini hususani kwa kiwango cha lami

[emoji3502]Kaongeza na kuboresha Vituo vya Afya kila kata

[emoji3502]Karejesha nidham serikalini na kuleta uwajibikaji wenye tija

[emoji3502]Mabeberu kila uchao wanatutengenezea mazingira ya kumchukia JPM ,Kwa ushawishi wao wanarubuni vijana kufikia hadi kudiriki kuwatusi Viongozi..

[emoji828]Ila Kwa maslahi mapana ya taifa letu, Magufuli amelijenga Taifa ipasavyo.

[emoji3502]Tukumbuke kuwa kila analofanya Magufuli ni kwa ajili ya Maslahi ya Taifa letu

[emoji3502]Watanzania wengine wanashindwa kutofautisha wema na ubaya..Ila Ipo siku Magufuli tutamkumbuka






Sent using Jamii Forums mobile app
IMG-20191227-WA0122.jpeg


Jr[emoji769]
 
[emoji828]Wamepita Marais wengi JMT lkn huyu JPM ameweka usawa sana..Anapenda Win win situation...

[emoji828]Nakukumbusha kuwa kabla ya ZJPM kuja

[emoji828]Makampuni makubwa yalifanya kazi nchini bila kulipa kodi

[emoji3502]Kila mtu alikuwa boss nchi hii

[emoji828]Twiga walipanda ndege

[emoji3502]Ujambazi ulishamiri sana
Atakumbukwa na wasioijulikana na mkuu wao wa Dar na Musiba wake
Sisi tutamkumbuka kama Raisi wa kwanza kuichambia Katiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji828]Wamepita Marais wengi JMT lkn huyu JPM ameweka usawa sana..Anapenda Win win situation...

[emoji828]Nakukumbusha kuwa kabla ya ZJPM kuja

[emoji828]Makampuni makubwa yalifanya kazi nchini bila kulipa kodi

[emoji3502]Kila mtu alikuwa boss nchi hii

[emoji828]Twiga walipanda ndege

[emoji3502]Ujambazi ulishamiri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweni magufuli amedondoka kutoka mbinguni si alikuwa kwenye system hiyohiyo

Acheni kulawiti fikra za mtanzania kwa cheap Propaganda zenu za kijinga

Uhaba wa madawati.jpg
 
[emoji828]Huenda na wewe ulikuwa unahadithiwa nadharia ya uongozi uliotukuka

[emoji828]Leo tunauona kwa JPM na bado huamini

[emoji828]Pole sana unahitaji ukombolewe kifikra
Tutamkumbuka kuwa Rais wa hovyo kupata kutokea nchi hii. Siamini kuwa kuna uwezekano akawepo Mtanzania ambae akipewa urais atakuwa hovyo kuzidi Magufuli.
Magufuli ni SI unit ya urais mbovu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sa
SGR ya umeme ikianza kufanya kazi ndio atakua amemaliza mchezo, Dar-Moro-Dodoma-Tabora-Mwanza/Kigoma watu watakua wanatumia treni ya umeme, umbali wa safari utapungua, unapiga mishe zako baina ya Dar na Mwanz
Safari zisizo kuwa za kiuchumi no upoyoyo kuziwaza, sgr ilikuwa kwenye ilani ya chama cha mapinduzi lakini mradi ulitakiea uende sambamba na ujenzi wa bandari mpya ya bagamoyo lakinibandari imewekwa kapuni hatujui hatujui inajengwa lini
 
Na Kasambula Theonest, Kigoma.

Tanzania leo inaungana na mataifa mengine duniani kuuaga mwaka 2019. Kuna mengi mazuri ya kuusemea huu mwaka lakini makala hii inaongelea kazi nzuri aliyofanya Rais John Magufuli wa Tanzania katika mwaka huu wa 2019 na inayoendelea mwaka 2020.

Kwanza nikiri kwanza kwamba Rais Magufuli amefanya mengi katika mwaka 2019 katika kuwaletea watanzania maendeleo. Kwa wingi huu naomba nikiri kuwa siwezi kuandika yote maana komputa mpakato itavunjika. Nitaandika machache kwa leo mengine nitayandika siku za usoni kwani kazi ndo imeanza.

Ujenzi wa bwawa kubwa la umeme katika Afrika Mashariki na la nne kwa ukubwa Afrika ( Mwalimu Nyerere Hydropower Project)
Katika mwaka 2019, Rais Magufuli ameweza kusimamia wazo la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere la kujenga bwawa kubwa la umeme litakalozalisha megawati 2,115 litakalo kamilika mwaka 2022 katika mto Rufiji.

Haikuwa kazi rahisi kwa sababu ya kelele za wapinga maendeleo wa ndani na nje ya nchi waliotaka kukwamisha kazi hii lakini Rais alisimama kidete na kuhakikisha mradi unatekelezwa.

Mradi huu unaojengwa kwa kodi za wananchi kwa zaidi ya shilingi tirioni sita za kitanzania ukikamilika utaweza kuifanya Tanzania kuwa msambazaji mkubwa wa umeme katika nchi za Afrika mashariki na kati.

Usafiri wa Anga
Ni vigumu kuamini lakini ndo ukweli kuwa tunamaliza mwaka 2019 Rais Magufuli akiwa amenunua ndege nane katika 11 ambapo tatu zinatarajiwa mwakani. Shirika la ndege lilishafirisiwa na mafisadi na kulikuwa na ndege moja tu wakati Magufuli anaingia madarakani. Sasa Magufuli amerudisha heshima ya Tanzania.

Ukiwa Afrika Kusini, Zambia, Malawi, DRC, Mumbai- India na muda si mrefu Guangzhou utaona twiga wetu akikuambia Tanzania tupo laivu kazini. Tunaambiwa baada ya ndege za abiria sasa madege ya mizigo yanafuata. Huyo ndo Magufuli Rais wa Watanzania, mchapa kazi na asiyependa nchi kuitwa maskini wakati ina rasilimali nyingi.

Umeme Vijijini
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania tangu tupate uhuru, Rais Magufuli anaifanya nchi kuingia katika mwaka mpya wa 2020 huku vijiji 9000 kati ya 12,000 vikiwa vimeunganishwa na umeme. Asante sana Rais Magufuli kwa kuona shida za watanzania wanyonge na kuwaunganisha na gridi ya Taifa ili wapate maendeleo.
Ikumbukwe pia kuwa bila umeme hamna maendeleo.

Huyo ndo Rais Magufuli ambaye ameamua pia kila mwaka bilioni 200 za kitanzania zitolewe kupitia mradi wa umeme vijijini ( REA) ili kujenga mifumo ya umeme vijijini na kununua miundo mbinu yake. Naweza Kusema hongera wana vijiji wa kitanzania hayo ndo matunda mliyochuma mlipomchagua Maguguli kuwa rais wenu mwaka 2015.
Upatikanaji wa maji safi na salama vijijini.

Katika moto uleule wa kuwajali watu maskini na watanzania kwa ujumla, Rais Mafuguli anaifanya Tanzania kuingia mwaka 2020 huku asilimia 67 za wananchi wanaoishi vijijini wakiwa wameunganishiwa maji safi na salama kutokana na miradi 1600 iliyoanzisha na serikali ya awamu ya tano.

Raisi Magufuli anatuambia kuwa mpaka mwaka 2025 kila kijiji kitakuwa kimeunganishiwa maji. Kwa wale tunaoishi tunaona kuwa upatikanaji wa maji umeongezekeza.

Takwimu zinasema zaidi ya asilimia 70 ya watanzania wanaoishi mjini wameunganushiwa maji na yanatoka kila siku. Haya ndo matunda ya uhuru, tuendelee kumuunga mkono jemedali wetu Rais Magufuli.

Sekta ya utalii
Kwa mara ya kwanza tangu nchi hii ipate uhuru, Rais Magufuli ameongoza jitihada za kungeza watalii ili kuinua pato la Taifa ambapo sekta ya utalii ni ya pili katika kuchangia pato la Taifa.

Pamoja na kelele za mabeberu na wanasiasa wa upinzani kuizushia Tanzania kuwa ina ebola ili watalii wasitemebelee nchi mwaka 2019, nchi imeendelea kupata watalii zaidi ya 10,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani ikiwamo ulaya, Asia…
 
Alinenalo mtu ndilo limsumbualo kama hilo ni tatizo kwako njoo nikupe msaada Nina Taasisi inayosaidia watoto wenye IQ kubwa kuwasomesha kwa shule za Tanzania mpaka chuo kikuu
Hahahaahahaaaaa,Taasisi yako inaitwaje?
Pakashume endelea kulamba miguu ya watu hapo Lumumba!
 
*2020 TUMEMCHAGUA RAIS MAGUFULI ATUONGOZE*




Heri ya Mwaka mpya 2020 Ndugu yangu Mtanzania. 2020 ni Mwaka mwingine wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anaendelea kuongoza. Naam! Watanzania tumemchagua Rais Magufuli aendelee kuongoza 2020 ili tuone kazi aliyoianza inakamilika ipasavyo na Watanzania wananufaika na matunda ya kazi hiyo.

(i) Kuhamia Dodoma

Wazo la Serikali kuhamia kwenye makao makuu ya nchi mkoani Dodoma liliasisiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere mwaka 1973 lakini lilishindwa kutekelezwa katika awamu zote. Si awamu ya kwanza, wala ya pili, ama ya Tatu au ya nne bali limeweza kufanikiwa kwenye utawala wa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Magufuli. Leo hii karibia Serikali yote imehamia Dodoma. Wizara, taasisi na idara za Serikali, Waziri Mkuu wameshahamia Dodoma mpaka Rais Magufuli naye amehamia Dodoma. Iliasisiwa na Mwalimu Nyerere, ikahaidiwa kwenye ilani ya uchaguzi, imekuja kutekelezwa vyema na Rais Magufuli lakini uhamiaji huu ni kwa awamu awamu. 2020 Watanzania tumemchagua Rais Magufuli akaimalizie hii kazi iliyokwama hapo awali bali yeye ameiweza kwa kuhakikisha Serikali kamili pamoja na idara zake zinahamia Dodoma.

(ii) Ujenzi wa Stiegler’s Gorge ama Mto Rufiji

Utawala wa awamu ya kwanza uliokuwa ukiongozwa na Mwalimu Nyerere ulikuja na wazo la kujenga Stiegler’s Gorge mnamo mwaka 1981 lakini umeshindwa kufanyika mpaka awamu hii ya 5 inayoongozwa na Rais Magufuli umeamua kufufua na kuliendeleza wazo hili ambalo pasipo ushujaa na ujemedari wa Rais Magufuli basi usingefanyika. Mradi wa Stiegler’s Gorge kupitia Mto Rufiji utafanikiwa kuzalisha Megawattz 2115 hadi utakapo kamilika ambapo utakuwa umeme mkubwa kuzidi huu unaotumika sasa. 2020 Watanzania tumemchagua Rais Magufuli ahakikishe ukamilifu wa mradi huu ambao utajenga uhakika wa umeme nchini, utashusha bei ya umeme nchini na pia utasaidia kuimarisha sekta ya viwanda nchini. Ni kwa uwepo wa uongozi imara wa Rais Magufuli pekee atasimamia vyema ukamilifu wa mradi huu ambao ni mkombozi wa umeme mjini hadi vijijini.

Pamoja na changamoto zote Dkt Kalemani: Hadi kufikia leo vijiji 8,818 kati ya vijijini 12,000 nchini vimepata umeme kutoka vijiji takribani 2,000 ushee tu vilivyokuwa na umeme 2015. Mwaka 2020 tumemchagua Rais Magufuli akamilishe kazi ya kusambaza umeme vijiji vyote nchini vilivyosalia.

(iii) Ujenzi wa reli ya kisasa (SGR)

Ni takribani miaka 120 ambapo historia iliandikwa mwaka 1912 kwa Serikali ya kikoloni kujenga Reli inayotumia dizeli. Leo hii kwenye sekta ya reli Rais Magufuli amefanya makubwa. Kwanza amefufua usafiri wa Dar - Moshi uliokuwa umekufa kwa zaidi ya miaka 25; Ameimarisha usafiri wa reli wa Dar - Dodoma - Kigoma ambapo sasa ni wa uhakika zaidi.

Tuachane na hayo, kuna hili la ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango cha Standard gauge (SGR) ambapo awamu ya kwanza imeanzia Dar - Morogoro na baadae Morogoro - Dodoma na kumalizia Dodoma - Mwanza kukamilisha umbali wa Kilomita 1219.

2020 Watanzania tumemchagua Rais Magufuli ahakikishe ukamilifu Reli hiyo ulete tija kwenye usafirishaji, Kilimo, utalii, uzalishaji na kibiashara. SGR itakuwa na uwezo wa kubeba tani milioni, 10,000, kwa mkupuo sawa na malori 500 yenye tani 20, Treni tano zenye tani 10,000 na kuwa na kasi kubwa ya 160km/saa, tofauti na ya sasa ambayo inakasi ya 30km/saa, kwa Afrika itakuwa ni Reli pekee yenye uwezo mkubwa kama huo, tani Miliomi 10-17 zitasafirishwa kwa mwaka, kwa hiyo SGR ni mwamba sekta ya usafirishaji nchini.

Itaendelea ...

T2020JPM
Rubbish
 
Huwezi kumiliki taasisi huku unalamba uchafu wa watu wengine huna lolote dume zima unanyemela teuzi
 
Back
Top Bottom