Mafanikio ya Utawala wa Jakaya Kikwete ndani ya Miaka 10

Kumbe hujui hata IPTL ilianza lini...? IPTL ipo toka miaka ya tisini kwa taarifa yako.
IPTL JK kaikuta nenda kasome historia..Kuna case za IPTL mahakamani London toka miaka ya tisini kasome historia vizuri..
Wewe hujui historia ya IPTL kaa kimya!! Kikwete ameiasisi kampuni ya IPTL kabla hajawa Rais; wakati huo alikuwa naibu waziri wa Nishati na Madini chini ya Al Noor Kasum
 
Jk alikuwa hana Promo tu ila mengi kafanya HUYU ANALIPA WATU WA KUMFANYIA PROMO NA PRAISE TEAM NAYO INA MKUZA SANA.JK KAFANYA YOTE BILA KUATHIRI KIPATO NA MAISHA HUKU MTAANI.
 

Bomba la gesi tulipigwa ile mabaya bomba la bilion 200 tukajengewa kwa 1.2T ,
 
Kuna wakati unaweza kudhani wenzako ni wajinga kumbe ni kwa sababu wewe umeshikwa na uwendawazimu.

Vichaa huwa wanaamini wana akili kuwazidi wenye akili, na pia wanaamini wana nguvu kuliko chochote, ndiyo maana huweza kusimama hata katikati ya barabrara wakiamini wana nguvu kuyazidi malori yanayoitumia hiyo barabara.

Waulize ndugu na marafiki zako kama wanakuona ni mzima. Mara nyingi magonjwa ya akili, dalili ya kwanza ni kuamini una akili kuwazidi watu wengine wote.
 
Wewe hujui historia ya IPTL kaa kimya!! Kikwete ameiasisi kampuni ya IPTL kabla hajawa Rais; wakati huo alikuwa naibu waziri wa Nishati na Madini chini ya Al Noor Kasum

Yanazungumziwa mafanikio ya urais wake, wewe unaleta habari za uwaziri.. Kama dhambi kuanzia watu walivyokuwa huko chini wengi wanazo.. Unajua kama IPTL ipo toka mwaka 1994 Rais ni Mwinyi tumuache tumlaumu JK wakati mwenye mamlaka yupo.
 
Kikwete alijitahidi sana. Na kwa kipimo chochote huwezi kumlinganisha na huyu wa sasa.

Tulimlaumu Kikwete kwa baadhi ya mambo. Tulitarajia tumpate kiongozi atakayekuwa bora kuliko yeye lakini kwa bahati mbaya tukampata huyu wa sasa.

Kosa kubwa la Kikwete ambalo mimi namlaumu ni kuruhusu mtu awauzie vimada na ndugu zake, nyumba za serikali kwa bei za kutupa (sh 10m nyumba iliyopo Upanga!). Halafu mtu huyo huyo badala ya kumpeleka Segerea, unampa nafasi ya kupewa madaraka ya juu zaidi. Huo ni udhaifu wa hali ya juu.
 
Mimi ongeeni yooote ila kubwa namshukuru sana mzee JK alinikopesha nkasoma elimu ya juu tena bila shida yoyote. Wazee wangu wasingeweza ila JK aliweza.
Ni jambo Jema, umalize mkopo wako kama bado wengine nao wafaidike.
 
DART ilianzishwa na kuzinduliwa JPM
Barabara zilitekelezwa na bado zinatekelezwa na JPM

Daraja la Kigamboni (Nyerere Bridge) lilianzishwa na kuzinduliwa na JPM. E.t.c.

Na kwa kweli miradi ambayo ilikamilika kwa ufanisi chini ya Kikwete mingi ni ile iliyosimamiwa na JPM kama waziri ndiyo maana tulimpa Urais. Over.
 
JK aliachia nchi inaenda kwa auto pilot. It was a disaster. It was very painful experience.
Amepumzika sasa. Tumpe heshima yake na kumuacha apumzike kwa amani
Nchi ingekuwa kwenye autopilot hali isingekuwa ilivyo sasa. Autopilot ndo ilikuwa unalipa mishahara na kujenga barabara? Autopilot ndo. Iliwaangamiza m23? Autopilot ndo imefaya hayo yote mleta mada aliyosema? Upo sahihi mzee aachwe apumzike maana hatuna Shukrani.
 
Na hili ndo kosa kubwa, watu wanafikiri aliyepita akipewa heshima yake anayostahili basi aliyopo anapungukiwa na sifa, wakati ukweli uliopo ni kwamba kila mtu anafanya yake kwa wakati wake. Kwani ni lazima mafanikio yaliyopita uyaunganishe na yanayofanyika?
 
Umenena vyema.

Kwa haya uliyoyaandika na yaliyoorodheshwa na mleta mada, nina hakika awamu hii mpaka sasa hawajafikia hata 10%. Hata kama wakiongezewa miaka iliyobakia, sidhani kama watafikia hata 30%.

Awamu hii wamekwishaharibu kwenye eneo la uchumi, ari ya utendaji kazi na uzalishaji, kamwe hawawezi kufanya makubwa.

Kikwete alifanikiwa kwa vile kulikuwa na fedha. Uwekezaji wakati wa kikwete ulifikia ukuaji wa 28%, sahizi ni 4% tu! Uwekezaji huongeza pesa ya kodi lakini pia huleta fedha toka mataifa ya nje na kuhuisha uchumi wa ndani. Huyu amefukuza uwekezaji wa nje na hata kuondosha ambao tayari ulikuwepo ndani ya nchi. Angalia akina Bakhresa walivyowekeza SA, Burundi, Zambia n.k. Angalia viwanda vya cement vinavyojengwa na Watanzania nchini Msumbiji. Angalia vituo vya mafuta vinavyojengwa na Watanzania nchini Zambia, n.k. Angalia wawekezaji waliokuwepo Tanzania walioenda kuwekeza Mauritius. Wawekezaji wamekosa confidence ya mazingira ya uwekezaji Tanzania. Ni vigumu sana kuwarudisha au hata kuwaleta wapya.

Kikwete aliongeza sana uzalishaji na mauzo ya nje ya zao la korosho. Pesa hiyo ilisaidia mzunguko wa fedha na uletaji wa fedha za kigeni. Huyo ameua mauzo ya nje ya zao la korosho. Taarifa ya BoT inaonesha thamani ya mauzo ya mazao ya nje yameingia kwenye negativr growth. Haijawahi kutokea tangu uhuru.

Kikwete alijitahidi sana kuendeleza sekta ya utalii. Utalii ulifikia ukuaji wa 15%. Ongezeko la ukuaji wa utalii, liliifanya sekta ya utalii kuongoza katika uingizaji wa fedha za kigeni, ikifuatiwa na sekta ya madini. Huyu wa sasa ameushusha ukuaji wa sekta ya utalii mpaka 3.6%. Sasa hata wakija watalii 500, inatangazwa nchi nzima ili tujue kuwa watalii bado wanakuja!

Kikwete aliimarisha sana mahusiano ya nje. Licha ya kupata fedha kutoka kwenye uchumi uliokuwa unanawiri lakini pia aliweza kupata fedha nyingi za misaada na mikopo rahisi bila shida. Kwa nchi kama ya kwetu huwezi kupaa kiuchumi bila kutumia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na misaada na mikopo. Ni wakati wa Kikwete, Tanzania ilikuwa ndiyo nchi ya kwanza katika Afrika kuweza kupata msaada mkubwa toka Marekani, ikifuatiwa na Ghana. Huyu alipokuja kutokana na mambo ya hovyo aliyoanza nayo pesa hiyo TZS 1.3 trillion tuliyokuwa tukiioata kila mwaka, ikapotea. Wenzetu Ghana walibahatika kupata mwendelezo mzuri wa uongozi, wanaendelea kupata mpaka leo, na Ghana inaongoza kwa ukuaji wa uchumi Afrika, na kuna wakati iliongoza kwa ukuaji wa uchumi Duniani. Ujerumani, ni kati ya mataifa yenye uchumi mzuri sana Duniani lakini ili kupiga hatua za maendeleo, baada ya vita kuu ya Dunia, ilipewa misaada. Misaada siyo mibaya, kama utaitumia kama mtaji.

Katika ujumla wake, ukiyatazama ambayo yalifanyika wakati wa Kikwete, tuwe wakweli wa nafsi zetu, yanayofanyika sasa ni kidogo sana yasiyostahili hata ulinganifu, lakini kelele ya kuyasifia imekuwa kubwa kuliko uhalisia. Nini cha ajabu kilichofanyika awamu hii ambacho hakikuwahi kufanyika?

Mwalimu Nyerere aliipokea nchi ikiwa haina grid ya Taifa. Alijenga grid ya Taifa. Alijenga mabwawa kama kidatu na Mtera. Kikwete akaongeza vyanzo vipya vya umeme wa gas. Kwa hiyo ujenzi wa bwawa jingine jipya awamu hii siyo kitu cha muujiza. Ni jambo la kawaida kwa nchi inayokuwa na ongezeko la watu.

Mwalimu Nyerere alinunua ndege 14 mpya, hakuna pangaboi hata moja. Sasa ndege za safari hii ni muujiza?

Wakati wa mwalimu kulijengwa reli toka Dar mpaka Kaprimposhi Zambia, karibia 2,000km. Sasa hii ya 300km ndiyo uwe muujiza?

Hospitali kama Muhimbili, na karibia zote za mikoa zilijrngwa wakati wa Mwalimu. Kikwete kioindi chake kulijengwa hospitali kubwa na uimarishaji wa hudumu za afya kwa kuboresha miundombinu yake. Sasa zahanati za awamu hii ziwe muujiza?

Hatujafikia pakulinganisha miradi ya awamu hii na ile ya awamu ya kwanza au awamu ya nne. Bado sana. Nauliza mambo machache:

1) Miaka 4 imepita, barabara km ngapi za lami zimejengwa awamu hii linganisha na 14,000km wakati wa Kikwete?

2) Madaraja makubwa mangapi yamejengwa awamu hii linganisha na madaraja 6 wakati wa Kikwete?

3) Ongezeko la la makusanyo ya serikali kwa 500% wakati wa Kikwete linganisha na ongezeko la sasa la makusanyo ya serikali

4) Linganisha ujenzi wa hospitali kubwa tatu (Mkapa, JK taasisi ya moyo na Mloganzila) zilizojengwa wakati wa Kikwete linganisha na awamu hii (hakuna hata moja labda ununuzi wa vifaa)

5) Linganisha ongezeko la wanafunzi wa vyuo vikuu lililoendana na ongezeko la mikopo, ujenzi wa UDOM na ubadilishaji wa vyuo vya kawaida kuwa vyuo vikuu, kutoka wanafunzi 3,000 mpaka 14,000. Ongezeko la 466%. Huyu wa sasa ameongeza wangapi?

6) Uletaji wa wawekezaji wakubwa kama Dangote wa zaidi ya $700m ulioendana na ajira za Watanzania 10,000. Huyu wa sasa ameleta uwekezaji gani ambao hata wa kufikia angalao $500m, na ajira za mara moja japo 5,000 tu? Au ndiyo vile viwanda 4,000 vilivyoajiri watu 12,000 (yaani kila kiwanda kina wafanyakazi 3!!!)

Awamu hii wafanye kazi lakini hawajafikia popote kiasi cha kujilinganisha na awamu iliyopita au awamu ya Mwalimu Nyerere. Wameharibu mambo mengi kwenye uchumi, wajisahihishe ili Mungu akiwajalia uhai, warekebishe katika kipindi cha pili. Kwa kipindi hiki their performance is very minimum, below our expectation.
 
Kikwete ndio muasisi wa kampuni ya IPTL na ufisadi WOTE ulifuata ukiwamo wa ESCROW!!!
Kikwete alikuwa muwazi na kiasi kikubwa aliheshimu uhuru wa mihimili mingine.

Tuliijua Escrow na IPTL kwa sababu aliruhusu watu kujadili.

Huyu kwenye awamu yake 1.5 trillion haijulikani iliko, na hataki watu wajadili. Huyu aliyelinda upotevu wa 1.5 trillion na aliyeruhusu kujadiliwa kwa 300 billion, nani afadhali?
 
Mijitu mizimaa yanalumbana eti kwa Kingozi kufanya wajibu wake. Waafrika hatutaendelea maisha yetu tutabaki kufadhiliwa kama maiti fungua usikilize
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…