Mafanikio ya Utawala wa Jakaya Kikwete ndani ya Miaka 10

Ila la kutumia mabilioni yetu katika mchakato wa Katiba mpya kisha kuitupa kapuni hili limeharibu yote mema aliyofanya. Katuachia msala mkubwa sana.
 
Jt kafanya kazi nzuri sana tatizo kila kazi ilikuwa na mchwa wengi sana kazi moja imeweza kugawanywa na kuwa kazi 5 kwa upigaji ulivyo kuwa na sio kwamba aijafanyika kazi, terminal 111 pesa zililiwa bila magu kuingilia kati isingeisha
 
Awamu ya tano imekua na promo saaaaana,.. Kitu kidogo tu, kitapigiwa kelele na kwakua vyombo vya habari vimebanwa, basi ni kama vile tuonavyo clouds katika promo zao.... Jk alikua kimya kimya, maendeleo na kula bata, yalikua maisha yenye afya, hata matatizo ya mgonjwa yatokanayo na msongo wa mawazo hayakua mengi kama Awamu ya tano
 

Wizi uliopitiliza. In order to be fair, acha tufanye comparison after 10 years.
Hapo tutakuwa tunatenda haki
 
Utawajua tu mafisadi waliokuwa wanafaidi keki ya taifa pekee yao. Wewe ni mmoja wao!
 
[Kajenga nyumba za jwtz nchi nzima
QUOTE="britanicca, post: 33128597, member: 290488"]
Kwa Kifupi Kikwete kafanya Mambo mengi sema kosa alilofanya ni kuruhusu watu wamchezee sharubu

Kikwete Kaongeza Hospital kadhaa
While za Kata
Nyumba za watumishi wa Umma kama Polisi na Walimu
Vivuko nchi nzima
Barabara za kutosha
Kajenga Mwendo kasi
Kajenga uwanja wa Ndege terminal 3 japo JPM kaja kuizindua tu
Kajenga viwanja vya ndege Songwe, Bukoba, Mbeya, na Mwanza
[/QUOTE]
 
Unalinganisha kwa mizani gani? Miaka minne kea miaka kumi?
Tuache ubabaishaji
Zaidi ya sekta ya afya kipi Magu anajivunia? Reli bado,stiglaz bado nini kingine mambo ya elimu bure toka kitambo primary hatulipi ada sekondari ilitoka elfu 40 hadi 20
Hata mpango wa kuboresha miji alianzisha jk sema na uchumi ulikuwa unapaa leo hii kila ripoti inatupiga chini tunasingizia mabeberu hakuna habari huru vuvuzela na mapambio hadi yanakera kwa wanufaika
Rushwa imedhibitiwa kwa wadogo tuu wakubwa kama Kawa afu mtu anasema nini,
 
[/QUOTE]
Pale monduli na gongo la Mboto wanajeshi wamejengewa mijengo ya kutosha.Nilitegemea Magu angewajengea walimu na mapoti nyumba za kutosha sasa wamejenga vijumba vitano vitano ufunguzi nchi nzima inaangalia haya ni mambo ya ajabu sana
 
Huo uwanja wa bilion 60 ukajengwa kwa bilion 100 mpaka siku ile magufuli aliona aibu kutamka ile thamani ya ule mradi kwa kweli
Bora ungenambia uwanja ni mbovu kama wa songwe ningekuelewa ila kuongeza bei sio kesi sana coz kazi na bata
By the way hosteli za Magu pale udsm ziligharimu zaidi ya 50 bln kwa mujibu wa CAG na bado zikawa chini ya kiwango kama vivuko nk nk wakati tulidanganywa kwamba ni 10 bln
Kumbi za tombo,mwln Nyerere coet etc pale mlimani zilijengwa vzuri tu na awamu ya Jk na mambo yanaenda
 

Watu wasichojua ni kwamba miaka ya mwisho ya utawala wa JK aliagiza ada sekondari iondolewe.

Na pia watu wasichojua ni kwamba hata SGR JK alishaitafutia pesa kwa wachina ila JPM alivyokuja akabadiri mfumo wa awali kwa kuwaondoa wachina na kuleta waturuki na kisha kuboresha design ya mwanzo (SGR ya JK ingekuwa kama ya Wakenya kuaccomodate trains zinazokwenda speed fulani slow, JPM akaboresha kuwezesha Train za speed ya kasi kidogo)
 
Mamaako alifanya makosa kutoitoa mimba uliozaliwa wewe hata family yenu inajuta kwa ilo
 
Usisahau kipindi Cha kikwete wapinzani walinga'ra kwa kuibua madudu ya serikali aliyokuwa akiongoza
 
Kwa maoni yangu sgr kama ya Kenya ingefaa lakini hii ya umeme kwangu naona sio maana hakuna cargo ya kufaa sgr ya umeme
Magu ahakikishe anamaliza hiyo sgr sina hakika akija rais mwingine atatoa pesa kuimalizia maana huu mradi kwa sehemu kubwa ni tembo mweupe kama Tazara inakula hasara sgr itapata wapi faida
 
Mkuu wala huna sababu ya kuorodhesha haya,either kiongozi wetu wa awamu ya tano ni mgonjwa au ana matatizo makubwa kichwani,juzi Kuna mwendawazimu fulani sijui ni Uvccm yule nilimpa lift akaanza kumsifia mwendawazimu mwenzie eti kisa barabara mijini mfano singida na Dodoma na miji mingine zimejengwa sasa,nikamuuliza hivi ukichukuwa urefu wa barabara zote za singida na zile za dodoma zinaweza kuwa sawa na barabara ya Mikumi Mafinga au Chalinze Melela au iringa Dodoma?Hawa watu wa awamu ya tano ni wendawaz dont waste your time
 
Kuacha watu wachezee sharubu ndo uongozi wenyewe, uongozi haupimwi kwa namna watu wanavyokuogopa,bali how do deal with issues hasa zile za usiowapenda
 
acheni kupaka rangi donkey ili ageuke kuwa zebra
 
Tulijenga sana mitaani.misauzi ilizagaa kila kona.
Awamu hii ujenzi wa nyumba binafsi umepungua badala yake watu wanauza nyumba walizojenga ili kujikimu.
Kwanza kitendo cha kutoongeza mishahara kwa wafanyakazi wa umma kwa miaka mnne ni ukiukwaji mkubwa wa haki za wafanyakazi.
- Bima ya mfanyakazi haiongezeki.
- Mafao ya kustaafu yanasimama kwa kiwango kilekile.
-Maisha yanazidi kuwa magumu hasa kwa wategemezi Kama wazazi wa Vijijini.
-Morali ya ufanyaji kazi inazidi kupungua.
- Kupungua kwa ushiriki wa mambo ya kisiasa pamoja na uandikishaji kura.
- Wafanyakazi kuanza kujitafutia kipato nje ya mshahala.
- Kuongezeka kwa hali ngumu ya kazi baada ya OC kutopelekwa katika idara za kazi.
- Utendaji kazi kushuka.
- Kikwete alimudu kuwaongezea mishahara kila mwaka Hadi Wafanyakazi Hewa.
Maisha yalikuwa yanaenda smooth kabisa.
Eti Leo tusubiri Hadi Sticlas Goji itakapoisha, na ndege 18, na Reli Hadi Kairo.

Bravo Mkwele
Una Upendo kwa watu.
Kama ujenzi angeumaliza Mfalme Suleimani.
Ndie Binadamu aliyemiliki pesa nyingi zaidi za ujenzi. Lakini alithamini maisha ya watu kuliko kokoto.
 
Wizi uliopitiliza. In order to be fair, acha tufanye comparison after 10 years.
Hapo tutakuwa tunatenda haki
Wizi uliopitiliza umetumia statics zipi kwa awamu zote ukaona awamu yake ilipitiliza? Ukiwa fair utagundua kuwa hakuna awamu isiyo na tatizo la wizi wa mali za Uma, hata wewe tukikuchunguza inawezekana kuna sehemu uliibia serikali kwa kiwango chako.

Ukitaka kulinganisha basi njoo na data za wizi awamu zote halafu linganisha, siyo kwa sababu tu awamu iliyopita watu waliachwa tu wazungumze, wachunguze na waongee watakavyo basi inahalalisha kuwa ndo awamu yenye wizi kuliko zote.

Kosa la mstaafu ni kuachia uhuru uliopitiliza mpaka kuitwa dhaifu. Wapinzani walikuwa wanaibua mambo mengine wanayakuza kupata faida za kisiasa. Yaani Unamwita mtu fisadi halafu unampa nafasi agombee kwa chama chako. Sasa hivi wanapata wanachostahili. Ngoja wabanwe tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…