Wazaliwa wa kwanza ni baba mbadala,Esau alizalau uzaliwa wake wa kwanza akamuuzia mdogo wake kwa chakula cha dengu akawa ndio ameuza baraka zote za uzaliwa wa kwanza,Yakobo ambaye ndiye mdogo wake Esau ndiye Israel wa leo taifa lenye nguvu duniani.
Hio maana yake ni nyingine kabisa Mungu huangalia
last born sio first born hio ndio fundisho la hilo andiko la Esau na nduguye Yakobo
Hata mfalme Daudi alipoenda kupakwa mafuta waliitwa watoto wote baba yake akampendekeza kaka mkubwa apakwe mafuta ila Mungu akakataa akasema sio huyu namtaka yule mdogo kuliko wote ambae hapa hayupo baba kuulizwa anasema ndio yupo bwana mdogo kaenda machungani huko anarudi jioni basi yule mpaka mafuta anasema mimi namtaka huyo
last born nimpake mafuta
sio hawa.
1 Samueli 17:12-14
12 Basi Daudi alikuwa mwana wa yule Mwefrata, wa Bethlehemu ya Yuda, aliyeitwa jina lake Yese; naye huyo alikuwa na wana wanane; na yeye mwenyewe alikuwa mzee siku za Sauli, na mkongwe miongoni mwa watu.
13 Nao wale wana watatu wa Yese waliokuwa wakubwa walikuwa wamefuatana na Sauli kwenda vitani, na majina ya hao wanawe watatu waliokwenda vitani ni haya,
mzaliwa wa kwanza Eliabu, na wa pili wake Abinadabu, na wa tatu Shama.
14 Naye huyo
Daudi alikuwa mdogo wa wote; na
hao watatu waliokuwa wakubwa wakafuatana na Sauli.
Haya tusome na hii
1 Samueli 16:5-12
5 Naye akasema, Naam, kwa amani; nimekuja kumtolea BWANA dhabihu; jitakaseni; njoni pamoja nami kwenye dhabihu. Akawatakasa Yese na wanawe, akawaita kwenye dhabihu.
6 Ikawa walipokuja, alimtazama
Eliabu, akasema,
Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake.
7 Lakini BWANA akamwambia Samweli,
Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana
mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana
wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA
huutazama moyo.
8 Ndipo Yese akamwita
Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye akasema, BWANA
hakumchagua huyu.
9 Ndipo Yese akampitisha
Shama. Naye akasema, Wala BWANA
hakumchagua huyu.
10 Yese
akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, BWANA
hakuwachagua hawa.
11 Kisha Samweli akamwambia Yese,
Watoto wako wote wapo hapa? Naye akasema,
Amesalia mdogo wao, na tazama,
anawachunga kondoo. Basi Samweli akamwambia Yese,
Tuma watu, wamlete; kwa sababu
hatutaketi hadi atakapokuja huku.
12 Basi akatuma mtu, naye akamleta kwao. Naye alikuwa mwekundu, mwenye macho mazuri, na umbo lake lilikuwa la kupendeza. BWANA akasema,
Ondoka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.
Mfalme Suleman alikua ni last born kwa baba yake Mfalme Daudi ambae alikua na kaka yake mkubwa Abesolum mtoto wa kwanza wa mfalme Daudi aliependwa sana na baba yake Daudi lakini akafanya njama za kumpindua Daudi na kuchukua ufalme wa baba yake kwa nguvu ikapigwa vita first born akakatwa kichwa kisha
last born akawa mfalme Suleman
Yusuphu na nduguze watoto wa Yakobo waliomuuza kwa wale wamisiri baadae akaja kua mtu wa juu alikua ni
last born
Mafundisho ni machache tu ukitaka nikuongezee mengine nakuongezea ili uone kwamba Mungu haangalii first born maandiko yanakataa Mungu anaangalia
last born yule aliye
mdogo kuliko wote ndie mwenye ufalme wa MUNGU