Mafwele azuiwa kuingia Marekani. Ahusishwa na Utekaji, ukiukwaji wa haki za binadamu

Mafwele azuiwa kuingia Marekani. Ahusishwa na Utekaji, ukiukwaji wa haki za binadamu

Ukiambiwa USA hauruhusuwi hizo Nchi ulizotaja pia hawakupokei pia yule jamaa aliezuiwa na Pompeo si alikumbilia ubalozi wa China Daslm kuchukua visa aende China walimkatalia kwa kumjibu malizana na USA kwanza..
Issue sio kwenda kwa sababu ya uzuri wa nchi, hio ni lugha ya kidiplomasia..

Suala ni diplomasia na taswira ya nchi. Marekani kuweka zuio hili maana yake imetangaza rasmi kuwa haina imani na Jeshi la Polisi na mifumo ya haki Tanzania.. nahaitoishia hapo..
Makonda alizuiwa nini kilitokea
 
Wangeanza na viongozi wa juu wanaomtuma, huyu mafwele ni mtu mdogo tu anayetumikishwa na kutumiwa na wakubwa kwa maslahi yao binafsi, waanze na mapapa ndio wafuate na hichi ki dagaa
 
Amteue awe rais na Mafwele awe IGP.
Unawapangia , yaani kwamba Mafwele anajiamulia yeye ..Shtuka wewe , mtu afanye ukatili TZ azuiliwe USA si bangi hizo kama wanamtaka waje kumchukua kabisa .
 
Mwambie akahudhurie mkutano wa World Cup unaendelea Marekani.
Kwani yeye ni waziri wa USA au Tz, Taifa stars inacheza kombe lipi la dunia ? Kwanza, hata kombe la dunia la mwaka huu halina vibes kwa vile host country , nchi yake haina usalama wa kutosha na ndiye gaidi mkubwa duniani.
 
Makonda alizuiwa nini kilitokea
Mkuu acha kuwa na kichwa kigumu, US katika lugha ya kidiplomasia hapo amesema serikali ya Tanzania inafuga majambazi , watekaji, wafiraji na wauaji, hio ndio maana yake.. hio ni picha mbaya tayari kwa serikali ya Tanzania duniani..

Makonda kuzuiwa kuingia US madhara yake huwezi kuyaona leo, lakini imeshamuharibia katika safari yake ya kisiasa.. kuwekwa kwenye list ya wahalifu na nchi kama US ni pigo.. kwanza kunabaadhi ya vyeo atabaki kuvisikia tokana na ban aliyonayo, mfano huwezi kuwa waziri wa mambo ya nje halafu una ban US..
 
Zingatia "diplomatic message" hayo mengine ya hisia mimi sijaongelea! US anaweza kukuground usiuze hata njugumawe na huo ushindani ukabaki kati ya Magu na njombe tu na ukashangaa! Majuzi tu hapa kabla ya uvamizi wa Iran, riyal yao ilishuka hadi laki kwa dola 1, zingatia hii sio message ya US to mafwele by the way who is mafwele hadi Rubio amzingatie? Hii ni massage kwa mwenye mbwa, period
Asante Mkuu hii ni message kwa Mwenye mbwa.

Watu wazungumzia ban kwenye angle ndogo sana ya viza, hawajui impact kwa nchi kidiplomasia, kiuchumi.
 
Unampiga ban kwenda USA wakati familia yake inaishi South africa non-sense kitakachosaidiq labda washikilie account zake za kifedha huko south
Familia ya Mugabe walivyopigwa ban USA na Europe walikuwa na mali nyingii South africa, kilichofata sahv si umeona

Ova
 
Safi, wamemuanika huyo fala. Upuuzi wake umewekwa hadharani. Hii itasaidia kupunguza ufala wao. Bashite na yeye walishampiga ban.
Bashite alipigwa ban na magufuli akamwondoa kwenye mfumo wake wote
 
Back
Top Bottom