Magari ya Jeshi kwa makusudi hawaheshimu Sheria za Usalama barabarani

kuna utaratibu wa kuendesha hizo gari zao kama kuna emergency
 
Unajua kilichobebwa humo? Huenda hakipaswi kusubiri
Si angetembea n'a king'ora sheria ni muhimu zinazuia ajali kwa kiasi kikubwa sasa hapo junction mtu angetokea upande mwengine si angemvaa na kusababisha ajali.
 
Shida ni moja hilo siyo tatizo la jeshi Ila ni shida ya huyo dereva hicho anachofanya ni makosa kabisa hata jeshi halijawahi kumfundisha kuwa mtovu wa nidham kiasi hicho na anatakiwa aandikiwe faini
 
Sasa si awe na king'ora huna king'ora mtu atajuaje kama gari la jeshi
 
Kama anadharula asubili taa zizime cha msingi kabla ya kuvuka anatizama usalama wake kwanza sio kupita pita kama unavyofikilia
 

Mfano ttcl wana mkongo wa taifa labda mkongo umekatika sehem flani kwahyo watangoja taa zizime ndo wapite wakati eneo flani linakua halina mawasiliano[emoji849]
 
Shughuli zao zinakinzwa na foleni,na zikikinzwa na foleni nani anajua hatari itayotukuta
 
Leo, kuna mama mmoja amepaki gari yake sehemu isiyoruhusiwa kupark sasa kuna wale jamaa wanaitwa manispaa walipoona hilo wakapiga pin la mnyororo kumsubiri mwenye gari....sasa yule maza kumaliza mambo yake akarudi kwenye gari na kukuta imezuiwa muda huo mpiga pini yupo mbali kidogo....yule maza bila kuuliza akachukua simu akaongea na mtu Kisha akaenda kutulia mbali kidogo na gari, baada ya muda kidogo ikaja gari moja ikasimama nyuma ya ile gari ya yule maza....wakatoka majamaa wawili, mmoja kavalia kijeshi, wakaangalia kumcheki yule manispaa walipoona hajitokezi wakatoa kimsumeno kidogo wakaanza kukata ile pini ya mnyororo, manispaa alipoona wanalihalibu lock lake akajitokeza akafungua bila kuongea nao Kisha yule maza akaja kuwasha gari na kusepa...wale jamaa nao wakasepa

Kuna watu wanajiona wana haki ya kuvunja sheria.
 
Serikali pia iangalie kwa jicho la pili foleni nyingi za magari mijini zinasababishwa na wanaoendesha magari used kama la mleta mada

Gari used ziruhusiwe tu vijijini kupunguza foleni mijini
 
Naongezea, uhamiaji, Rc Dar, Zimamoto,
 
Hao wanalinda hii nchi,,, Waache tu waende..
 
Punguza nongwa ikiwezekana acha kabisa ingawa kama umekulia mazingira ya nongwa ni vigumu sana kuacha.Kwani ndio tukio lako la kwanza kuliona kwa gari za serikali tokea uwe mkubwa.?Tanzania ni Tanzania na itabaki Tanzania, Ulaya ni Ulaya, mtu mweusi ni mweusi na mzungu ni mzungu, tutaiga machache mengine hatutoweza milele.
 
Msiwe wanafiki.
Tabia mbaya ni tabia mbaya tu.
Indiscipline katika vyombo vyetu if unchecked this will lead to lawlessness and anarchy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…