Magufuli siyo shujaa wa Afrika, Kikwete ni shujaa wa Afrika

Magufuli siyo shujaa wa Afrika, Kikwete ni shujaa wa Afrika

Dhaifu ni kauli ya kisiasa tu. Kuitwa dhaifu hakumfanyi asiye dhaifu awe dhaifu.

Dhaifu anawatwanga M23? , Anasuluhusha mgogoro Kenya watu wasichinjane? , anarudisha amani Madagascar? , Anampiga muasi huko Anjuan Comoro?, Dhaifu anamuonyesha advertise Kagame kwa kumrudishia wahamiaji wake kwake?, Dhaifu anamrudisha Nkurunzinza madarakani kijeshi?
Sikuwahi kumwita Kikwete dhaifu wala kumuona ni shujaa ila waliyomuona Kikwete dhaifu na walikuwa wanatoa sababu kwa kuangalia hali ya nchi kutokana na uongozi wake, sasa hao watu ndio wanao kushangaa humu na kupinga huko kumwita JK ni shujaa tena wa afrika.
 
KIKWETE BABA LAO. Anayebisha na aseme. Hana kiburi, kinyongo, kisasi wala hasira. Ni mtu ambaye si mchoyo kabisa na mwepesi wa kutoa na asiye na maneno makali na ya masimango.

Ni moja kati ya watu wa kipekee sana na ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wote. MUNGU ampe maisha marefu. Amina.
 
JPM kafikisha umeme Tanzania nzima, zunguka tu hapa kwa majirani zetu halafu uone kama mtandao wao wa umeme ni kama wa kwetu.

JPM alinunua rada nne zilizofungwa katika mtindo wenye kuweza kuiona kila sehemu ya ardhi ya nchi hii, hakuna tena yale mambo ya ndege za wizi kuingia huko maporini na kuondoka bila ya kuonekana. Ni kwa sababu tu ya corona sekta ya anga imezorota vinginevyo pesa itakayokuwa ikiingia hazina kila mwezi kutokana na tozo za ukatishaji wa anga letu ni mabilioni ya pesa.

Ukimpima JPM ukiwa umekaa na laptop yako au simu huwezi kuona mchango wake wa mabadiliko ya ustawi wa watanzania, ukiwa mtu wa field utaiona kazi kubwa aliyofanya.

Kuna viwanda vya kuchenjua madini hapa hapa nchini. JPM amefanya mengi. Suala la kuzuia mtandao wa mishahara hewa limesifiwa na waandishi wa habari wa Nigeria.
 
Kalinganishwa JK na JPM kwa waliyofanya Africa, sio JN. Kulingana na mleta mada JK inaonekana kafanya zaidi ya JPM inapokuja suala la Africa.
Wanajua sana sema tu wako insecure, wanadhani kumsifu mtu mwingine ni kumshusha Nyerere kitu ambacho siyo lengo la mada hii!

Wao wanadhani shujaa peke kutoka nchi hii ni Nyerere basi!
 
Magufuli hata mikutano ya AU alikuwa haendi, Mikutano ya SADC nayo alikuwa akihudhuria kwa manati. Sasa mtu kama huyu ambaye hata kukutana na wenzie kujadili mambo ya Afrika alikuwa anaona tabu ni shujaa wa namna gani wa Afrika?
Alipokuwa akienda anazungukwa na maraisi wa Afrika..mpaka wadhungu wanauliza kwani huyu JPM ana nini?!
 
Mleta mada uko sahihi, kinachotakiwa ni je umeifanyia nini Afrika cha kukumbukwa?. Ukiangalia mwendazake hakuna chochote atakachokumbukwa nje ya mipaka ya Tanzania.
Mheshimiwa Kikwete na watangulizi wenzake wanastahili kuitwa mashujaa wa Afrika.
 
Back
Top Bottom