Magumu yetu Viongozi wa Upinzani mkwepe lawama vipi?

Magumu yetu Viongozi wa Upinzani mkwepe lawama vipi?

Hapana Mimi si mmoja wao,
Kwanini basi usingependa kuona tuna viongozi waliodhamiria kuona tunawatia adabu walamba asali kwa vitendo, bila kuchoka wala kukoma?
 
Ukisema "mliwaita" unakusudia kuwasema kina nani hao waliowaita wenzao?

Vicious cycle taslimu. Yaani ujinga endelevu si ndiyo huu sasa?

Tufanye waliitwa wasaliti hivyo sasa wamenuna. Basi si wapishe waingie kina Mtikila, Malema, Seif, Nyerere, Tutu na wa namna hiyo wasiokuwa na utoto kama unaoona wewe ni mali mno?

Kwamba:

"Maandamano muanzishe ccm wenyewe huko ndani kwani mkianzisha nyie hayatakuwa maandamano?"

Kama namwona Mwigulu akikushangilia kweli kweli. Kama si nduguyo yumkini ni mfuasi wake nguli kabisa.
Hao wanaotaka kuingi kuna mtu kawafunga wasiingie?

Si watafute njia yao na mtaji wa kisiasa upo ndio kama huu wajitokeze wataungwa mkono sio lazima wapishwe.

Ni upuuzi kulaumu wengine wakati wewe hufanyi kitu.
 
tafuteni upinzan wenu au mfufuen mrema aendelee kusema ccm nji hii ni chama kizuri.

Yameelezwa kwenye mada. Mnaotaka kupoa mtatafuta vyenu. Tutabanana hapa hapa:

"Viongozi wanaohofia kufa au jela tafadhali wapishe madarakani. Damu mpya zipo. Hatuhitaji vyama vipya. Tubanane na hawa hawa. Hawataki kutoka madarakani shime wanathaura tuanze kwa kuwafurusha wao kwanza."

Habari ndiyo hiyo.
 
Hao wanaotaka kuingi kuna mtu kawafunga wasiingie?

Si watafute njia yao na mtaji wa kisiasa upo ndio kama huu wajitokeze wataungwa mkono sio lazima wapishwe.

Ni upuuzi kulaumu wengine wakati wewe hufanyi kitu.
Wapi analaumiwa nani? Ni upuuzi kudhani analaumiwa mtu kwenye kujizatiti kusonga mbele:

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Zaidi sana ni upuuzi kuwalaumu wafuasi kuwa hawafanyi ya kutosha bila ya kutoa nafasi kwa wenye dhamira zaidi ya kuendelea mapambano wakiwa wangalipo.

Ninakazia: hakuna harakati bila viongozi. Uongozi siyo marupurupu yake pekee.

Uongozi ni pamoja na madhila yake.
 
Kwanini basi usingependa kuona tuna viongozi waliodhamiria kuona tunawatia adabu walamba asali kwa vitendo, bila kuchoka wala kukoma?
Nani wa kumfunga paka kengele,kwani walamba asali awajui hatuna umoja wa kupinga wayatakayo.
 
Ulaya heshima ilikuja baada ya kupigana watawala na watawaliwa. Leo ni fully heshima KILA mmoja asipotimiza wajibu wake uona cha mtema kuni, usipolipa kodi unashughulikiwa ukifisadi kodi za umma unapotea
 
Nani wa kumfunga paka kengele,kwani walamba asali awajui hatuna umoja wa kupinga wayatakayo.
Hatuna umoja? Huu umoja unatoka mbinguni? Huu umoja ni wa watu wangapi wakifika ndiyo sasa tutakuwa tumekamilika?

Kama nchi tuko vibaya, nani mwenye kubeba dhima ya ukombozi wetu?

Siyo siri. Tuliopo tunatosha. Tuliwahitaji kina Mtikila, Nyerere, Tutu na wa namna hiyo kuliko wakati mwingine wowote.

Ninakazia viongozi waliopo ni muhimu kujitathmini. Vinginevyo atalaumiwa sana dobi.
 
Watu wanaza singeli,na bongo fleva Saa ngapi wawe na umoja
 
Sasa mkuu hii ya kulindima huku halafu ukiwa invisible huoni kama wasting time

Try to make your life better na ndicho kinachotokea kwa sasa
 
Sasa mkuu hii ya kulindima huku halafu ukiwa invisible huoni kama wasting time

Try to make your life better na ndicho kinachotokea kwa sasa

Kulindima na kubakia invisible? Wapishe madaraka tuchukue hatamu utatuona visibly.

Wakikomaa tutakomaa utatuona visibly.

Kwamba tungependa ustaarabu utamalaki huku tukimtambua adui yetu ni mlamba asali? Huo si ndiyo uungwana uliotamalaki?

Au wewe kuto waste time ni kutusokomezea sisi matozo huku nyie mkilamba asali?
 
Jamii zinazijitambua zinatokea mbingu ipi?

Kenya na sisi tofauti si watu bali viongozi.

Habari ndiyo hiyo.
Kenya na sisi ni tofauti ya ideology.Wao ni moto sisi ni baridi.Mfano mwanamke wa Kenya ukiweza ishi nae ujengewe mnara
 
Walamba asali waliwafukuza wakoloni Ili walambe wao asali
Hii si jamii ya walamba asali:

Nyerere, Seif, Mtikila, Malema, Mandela, Tutu na wa namna hiyo.

Watu hao walisukwa sukwa maisha yao yote.

Hao si Madelu na genge lake.
 
Kenya na sisi ni tofauti ya ideology.Wao ni moto sisi ni baridi.Mfano mwanamke wa Kenya ukiweza ishi nae ujengewe mnara

Kupambana na walamba asali inataka damu moto. Tumeridhia damu zilizopoa kutuongoza. Haya ndiyo madhara yake.

Sikia Muziki wa Seif. Hii si Kenya:

Kwetu tunasubiri Juma na Ali watoke kivyao vyao. Ni viongozi wamesusa. Makubwa! Watatoka je? Kwa mwongozo upi?

Tofauti yenu na walamba asali iko wapi? Miito yote kujifunza tumeifumbia macho:

Uzoefu wa Zanzibar 2020 - Tuna ya Kujifunza, yatasaidia kwa Ukombozi

Anasema Prof. Jay - "Tusaidiwe je?"
 
Back
Top Bottom