Magumu yetu Viongozi wa Upinzani mkwepe lawama vipi?

Magumu yetu Viongozi wa Upinzani mkwepe lawama vipi?

Hii si jamii ya walamba asali:

Nyerere, Seif, Mtikila, Malema, Mandela, Tutu na wa namna hiyo.

Watu hao walisukwa sukwa maisha yao yote.

Hao si Madelu na genge lake.
Lakini wao na hata vizazi vyao hata kesho awalali njaa na wala sio walamba chumvi. Wapigania UHURU walipigania maslai yao binafsi na vizazi vyao na sio maslai ya waafrika wote.
 
Amsha amsha ya watz ni hadi wakati wa uchaguzi
Haieleweki unasema nini au husemi nini. Ukombozi unahitaji watu wenye ufahamu zaidi ya wako mjomba. Zaidi sana dhamira. Maji kukuzidi kimo ni jambo la kheri tu.
 
Lakini wao na hata vizazi vyao hata kesho awalali njaa na wala sio walamba chumvi. Wapigania UHURU walipigania maslai yao binafsi na vizazi vyao na sio maslai ya waafrika wote.
Mtikila, Seif, Tutu, na hata Malema wawaona mle pia?
 
Acha watu akili ziwakae sawa kwanza!! Tope lote likiisha kichwani ndo watajielewa!!

Bila hata wapinzani sheria kandamizi zikija wataingia barabarani wenyewe!!

Haiingii akilini eti mtu ukikandamizwa mpaka umsubirie mwanasiasa aje akutetee?? Ni akili tu unakuwa huna!!!

Sheria kandamizi zikija kila mtu toka nje piga kelekele tunaonewa!! Hilo ndo Taifa la watu majasiri wanaojielewa!! Siyo kumtegemea mtu fulani kukusemea, big noo!!!

Namwona Mwigulu akikushangilia kweli kweli. Kaza uzi hapo hapo. Kwani na wewe ni mlamba asali pia? Tuliwahi kuwatambua watu hawa wasiopenda mafanikio yetu:

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

"Watafanya lolote kuona hatupigi hatua yoyote ya maana."

Vipi na wewe ni mmoja wao?

Kwamba walipuuzwa? Kwa hiyo wamesusa? Rahisi si ilikuwa ni kuachia ngazi tu, au?

Mbona MV mapenzi safari ilisonga?
 
Comment yako ilikuwa muhimu mkuu.

Uchawa wa aina ya kina Jumbe Brown na wenzao hauwezi kuwa na nafasi katika jamii iliyostaarabika.
Ukweli usemwe tu wakishindwa waachie ngazi washike wengine na sio kuzila wakati posho na marupurupu unapokea....hata Kama watz wajinga lkn sio hivi wafanyavyo viongozi
 
Nakuelewa sana unamaanisha sana!!

Watu wakishakamatwa vizuri wakaanza kujipgania wenyewe hapo ndo penyewe!! Wapinzani kaeni kimya kabisa kwa sasa!! Acha watawala waafanye watakavyo mpaka watanzania akili zitakapowakaa sawa, waingia barabarani wenyewe!!

Watu kama wewe na wenzio mliangaziwa hata mwaka uliopita. Hii comment #7:

IMG_20220823_134516_288.jpg


ya uzi huu wa mwaka jana:

CHADEMA: Bila kuwapa Makavu hakuna Katiba Mpya

Waungwana Kulikoni?

Cc: antimatter, Kalunya
 
Ukweli usemwe tu wakishindwa waachie ngazi washike wengine na sio kuzila wakati posho na marupurupu unapokea....hata Kama watz wajinga lkn sio hivi wafanyavyo viongozi

Moto wa ukombozi haupaswi kupoa. Joto jikoni likikuzidi kama kiongozi unapisha wengine wenye uhimilivu.

Kuna wadau wengi, hatufurahishwi na status quo. Hili si leo ni muda sasa. Mengine ni yatokanayo:

CHADEMA: Bila kuwapa Makavu hakuna Katiba Mpya

Ikumbukwe vyama hivi ikiwamo Chadema si mali binafsi za watu.

Mwanzo wa ngoma ni lele.
 
Watu kama wewe na wenzio mliangaziwa hata mwaka uliopita. Hii comment #7:

View attachment 2332327

ya uzi huu wa mwaka jana:

CHADEMA: Bila kuwapa Makavu hakuna Katiba Mpya

Waungwana Kulikoni?

Cc: antimatter, Kalunya
Mkuu,
Wananchi wakishachoka hawahitaji kuhamasishwa na yeyote.
Kwenye ule uchaguzi wa Oktoba 28, 2020, kulikua na matukio kadhaa ambayo ni somo tosha.
Mkiiba Kura tena 2025, ndo mtajua hamjui

 
Mkuu,
Wananchi wakishachoka hawahitaji kuhamasishwa na yeyote.
Kwenye ule uchaguzi wa Oktoba 28, 2020, kulikua na matukio kadhaa ambayo ni somo tosha.
Mkijaribu kuiba tena 2025, ndo mtajua hamjui


2007 Kenya wananchi waliingizwa barabarani. Waliowaingiza barabarani Wana rekodi zao pale ICC, The Hague.

2022 Kenya wananchi wameombwa kutulia, tuli wametulia wanasubiri amri nyingine.

Kwa uongozi huu wa upinzani kama ulivyo sasa hataingia mtu barabarani. Si wewe, mimi wala wao.

Kwa uongozi wa waliodhamiria kama kina Mtikila, Seif, au Malema tutakuwapo mitaani ukiwamo wewe, mimi na wao.

Kwani kuna hata haja ya kujidanganya? Huo ndiyo ulio ukweli mchungu.

Zingatia bandiko hili la Aug 2021 kwa chawa kama wewe:

IMG_20220823_134516_288.jpg


Uchawa uchwara haulipi!
 
"He will win who knows when to fight and when not to fight"
Sun Tzu

"The greatest victory is that which requires no battle.”
Sun Tzu

By definition, "opportunists are those who think they can have it, the easy way."

Namwelewa sana Prof. Lwaitama, - "ni heri kufa nikipigania haki kuliko kufa kwa Malaria."
 
By definition, "opportunists are those who think they can have it, the easy way."

Namwelewa sana Prof. Lwaitama, - "ni heri kufa nikipigania haki kuliko kufa kwa Malaria."
My position is not Chadema's though..
Mie siyo mwanachama, ni mpenda Haki tuu.
Usije ukachukulia mawazo yangu binafsi kama ya hicho chama!
 
My position is not Chadema's though..
Mie siyo mwanachama. Usije ukachukulia mawazo yangu binafsi kama ya hicho chama!
What makes you think whoever may associate you anyhow with any party or Chadema so to speak?

Au nani hata ametaka kujua wewe ni mwanachama wa chama gani? Mambo kama haya mbona yameangaziwa sana humu mjomba?

Watambue Wanachama wa Vyama Mitandaoni

Nani asiyejua humu yatolewayo ni mawazo binafsi ya watu?
 
Tufike mahali tutoleane uvivu wenyewe kwa wenyewe. Tufike mahali panya wamfunge paka kengele.

"Enyi viongozi wetu madarakani, mliochagua kukaa kimya na kututelekeza kondoo wenu, tokeni madarakani washike wenye kudhamiria."

Ikumbukwe wavumao baharini papa lakini na wengine wapo.

Imekuwa kuwalaumu vijana kwa kuendekeza mambo yasiyokuwa na tija kwa taifa, lakini je vijana hawa kwa uongozi upi wasimame imara wapi?

Ya nini kuendelea kumlaumu dobi, wakati kaniki ni rangi yake?

Misahafu inasema "nitampiga mchungaji na kondoo wa kundi watatawanyika."

Kondoo wametawanyika nani wa kuwakusanya?

Viongozi wanaohofia kufa au jela tafadhali wapishe madarakani. Damu mpya zipo. Hatuhitaji vyama vipya. Tubanane na hawa hawa. Hawataki kutoka madarakani, shime wanathaura tuanze kwa kuwafurusha wao kwanza.

Ziko wapi kauli zao? Iko wapi mikakati yao? Ziko wapi dira zao? Yako wapi maono yao? Nini tufanye au tuanzie wapi?

Ninakazia: tuna matatizo ya kiuongozi zaidi kuliko ya kujitoa kwa wafuasi.

Tumung'unye maneno hadi lini?

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Mfano wa habari kamili ni huu:

CHADEMA: Bila kuwapa Makavu hakuna Katiba Mpya
Makini sana
 
Back
Top Bottom