Magumu yetu Viongozi wa Upinzani mkwepe lawama vipi?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Tufike mahali tutoleane uvivu wenyewe kwa wenyewe. Tufike mahali panya wamfunge paka kengele.

"Enyi viongozi wetu madarakani, mliochagua kukaa kimya na kututelekeza kondoo wenu, tokeni madarakani washike wenye kudhamiria."

Ikumbukwe wavumao baharini papa lakini na wengine wapo.

Imekuwa kuwalaumu vijana kwa kuendekeza mambo yasiyokuwa na tija kwa taifa, lakini je vijana hawa kwa uongozi upi wasimame imara wapi?

Ya nini kuendelea kumlaumu dobi, wakati kaniki ni rangi yake?

Misahafu inasema "nitampiga mchungaji na kondoo wa kundi watatawanyika."

Kondoo wametawanyika nani wa kuwakusanya?

Viongozi wanaohofia kufa au jela tafadhali wapishe madarakani. Damu mpya zipo. Hatuhitaji vyama vipya. Tubanane na hawa hawa. Hawataki kutoka madarakani, shime wanathaura tuanze kwa kuwafurusha wao kwanza.

Ziko wapi kauli zao? Iko wapi mikakati yao? Ziko wapi dira zao? Yako wapi maono yao? Nini tufanye au tuanzie wapi?

Ninakazia: tuna matatizo ya kiuongozi zaidi kuliko ya kujitoa kwa wafuasi.

Tumung'unye maneno hadi lini?

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Mfano wa habari kamili ni huu:

CHADEMA: Bila kuwapa Makavu hakuna Katiba Mpya
 
Acha wakae tu kimya na wenyewe ni binadamu wamepiga kelele sana, watanzania wakaishia kuwadharau na kuwaona kama wendawazimu au waliokosa cha kufanya!!

Kwa sababu walichokuwa wanapigania ni kwa ajili ya wote lakini wakaonekana wehu, sasa acha watawala wafanye watakacho mpaka akili ziwakae sawa!!

Siku mkiambiwa bungeni kunahitajika kuwa na wapinzani wengi sana ili sheria za hovyo za kumgandamiza mwananchi zisipitishwe kirahisi muelewe wanaamanisha nini!!

Wakipiga kelele tunahitaji katiba mpya kwa ajili kuweza kuweka dira mpya ya nchi yetu muelewe wanamaanisha nni!!

Watawala kamatieni hapo hapo,, ongezeni kodi zaidi, wakihoji waambieni waende Somalia kabisa,, hamna namna!!
 
Kwanini wasipishe madarakani? Kwamba walipiga kelele hawakusikilizwa? Labda hakupiga vya kutosha?

Mbona hawa walisikilizwa?

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Wito wa kiungwana, waliopo kama yamewashinda waweke manyanga chini wakae pembeni. Viongozi wenye kudhamiria wapo.
 
Kwanini wasipishe madarakani? Kwamba walipiga kelele hawakusikilizwa? Labda hakupiga vya kutosha?

Mbona hawa walisikilizwa?

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Wito wa kiungwana, waliopo waweke manyanga chini wakae viongozi wenye kudhamiria.

Acha watu akili ziwakae sawa kwanza!! Tope lote likiisha kichwani ndo watajielewa!!

Bila hata wapinzani sheria kandamizi zikija wataingia barabarani wenyewe!!

Haiingii akilini eti mtu ukikandamizwa mpaka umsubirie mwanasiasa aje akutetee?? Ni akili tu unakuwa huna!!!

Sheria kandamizi zikija kila mtu toka nje piga kelekele tunaonewa!! Hilo ndo Taifa la watu majasiri wanaojielewa!! Siyo kumtegemea mtu fulani kukusemea, big noo!!!
 
We need to wake up, wao pamoja nasi; naona wametekwa na yale maneno "siasa za kistaarabu" matokeo yake wamegeuka mabubu.

Muhimu kwangu waangalie principles zao, wajue wanachoongea ni cha kweli wasimuonee mtu, ili huo ustaarabu usigeuke ububu wa kukalia kimya uonevu.

Naona pia jinsia ya kiongozi wa taifa tuliyenaye imewavuruga psychology zao, wameshatekwa inawezekana wanahisi wakiongea wataonekana wanamuonea.
 
Wapinzani wasilaumiwe tena naomba waendelee kukaa kimya mambo yanavyozidi kuharibika, maana nasi tulikaa kimya wakati wakiteswa na utawala dhalimu. Lisu, Mbowe, Zitto msiwatetee watz acheni wanyooshwe kisawa sawa na tozo, bei juu nk, maana awakusimama nanyi wakati mkiteswa
 
hapana..... watu kuanza kujipigania wenyewe ndiyo utamu unaanza kukolea naomba mwigulu akazie hapohapo ikibidi aendeleee kuyapelkea moto manyumbu ya nchi hiii hadi akili zikae sawa
Nakuelewa sana unamaanisha sana!!

Watu wakishakamatwa vizuri wakaanza kujipgania wenyewe hapo ndo penyewe!! Wapinzani kaeni kimya kabisa kwa sasa!! Acha watawala waafanye watakavyo mpaka watanzania akili zitakapowakaa sawa, waingia barabarani wenyewe!!
 
Tufike mahali tutoleane uvivu wenyewe kwa wenyewe. Tufike mahali panya wamfunge paka kengele.

"Enyi viongozi wetu madarakani, mliochagua kukaa kimya na kututelekeza kondoo wenu, tokeni madarakani washike wenye kudhamiria."

Ikumbukwe wavumao baharini papa lakini na wengine wapo.

Imekuwa kuwalaumu vijana kwa kuendekeza mambo yasiyokuwa na tija kwa taifa, lakini je vijana hawa kwa uongozi upi wasimame imara wapi?

Ya nini kuendelea kumlaumu dobi, wakati kaniki ni rangi yake?

Misahafu inasema "nitampiga mchungaji na kondoo wa kundi watatawanyika."

Kondoo wametawanyika nani wa kuwakusanya?

Viongozi wanaohofia kufa au jela tafadhali wapishe madarakani. Damu mpya zipo. Hatuhitaji vyama vipya. Tubanane na hawahawa. Hawataki kutoka madarakani shime wanathaura tuanze kwa kuwafurusha wao kwanza.

Ziko wapi kauli zao? Iko wapi mikakati yao? Ziko wapi dira zao? Yako wapi maono yao? Nini tufanye au tuanzie wapi?

Ninakazia: tuna matatizo ya kiuongozi zaidi kuliko ya kujitoa kwa wafuasi.

Tumung'unye maneno hadi lini?

Mfano wa habari kamili ni huu:

CHADEMA: Bila kuwapa Makavu hakuna Katiba Mpya
Mbona watenda maovu wanajulikana na wanakejeli umma hadharani, kwanini mnalaumu wasiohusika?!
 
We need to wake up, wao pamoja nasi; naona wametekwa na yale maneno "siasa za kistaarabu" matokeo yake wamegeuka mabubu.

Muhimu kwangu waangalie principles zao, wajue wanachoongea ni cha kweli wasimuonee mtu, ili huo ustaarabu usigeuke ububu wa kukalia kimya uonevu.

Naona pia jinsia ya kiongozi wa taifa tuliyenaye imewavuruga psychology zao, wameshatekwa inawezekana wanahisi wakiongea wataonekana wanamuonea.
Acha wakae kimya wameteseka sana awamu iliyopita wakati sisi tulikaa kimya waliteseka pekee yao
 
Acha watu akili ziwakae sawa kwanza!! Tope lote likiisha kichwani ndo watajielewa!!

Bila hata wapinzani sheria kandamizi zikija wataingia barabarani wenyewe!!

Haiingii akilini eti mtu ukikandamizwa mpaka umsubirie mwanasiasa aje akutetee?? Ni akili tu unakuwa huna!!!

Sheria kandamizi zikija kila mtu toka nje piga kelekele tunaonewa!! Hilo ndo Taifa la watu majasiri wanaojielewa!! Siyo kumtegemea mtu fulani kukusemea, big noo!!!
Hakuna atajayeingia barabarani bila viongozi waliodhamiria kuongoza watu kuingia barabarani.

Kenya 2007 watu waliingizwa barabarani. Kenya 2022 watu wametakiwa kuwa wavumilivu.

Watu hawaingii barabarani wenyewe. Watu huingizwa barabarani.

The Hague ulisikia kina yakhe gani walikwenda kujibu ya watu kuingia barabarani Kenya?

Kwanini kama yamewashinda wasipishe hatamu za uongozi kwa wengine waone hii ngoma huchezwaje?

Kwani kuna siri - hakuna mafanikio bila uana harakati usiokoma. Maji yakikuzidi si unapisha tu? Hadi yakukute ufurushwe unceremoniously?
 
We need to wake up, wao pamoja nasi; naona wametekwa na yale maneno "siasa za kistaarabu" matokeo yake wamegeuka mabubu.

Muhimu kwangu waangalie principles zao, wajue wanachoongea ni cha kweli wasimuonee mtu, ili huo ustaarabu usigeuke ububu wa kukalia kimya uonevu.

Naona pia jinsia ya kiongozi wa taifa tuliyenaye imewavuruga psychology zao, wameshatekwa inawezekana wanahisi wakiongea wataonekana wanamuonea.

Hapana kwa sasa wakae kimya kabisa!! Acha kwanza mtanzania ajitambue!! Hakuna kitu kigumu kama kumpigia mbuzi zeze acheze!! Ni sawa na kupaka upepo rangi!!

Nasema waongeze kodi zaidi na zaidi, mfumuko wa bei uende juu kabisa!!! Hadi mtanzania akili itakapo mkaaa sawa aamke kwenye huo usingizi wa pono!!
 
Hakuna atajayeingia barabarani bila viongozi waliodhamiria watu kuingia barabarani.

Kenya 2007 watu waliingizwa barabarani. Kenya 2022 watu wametakiwa kuwa wavumilivu.

Watu hawaingii barabarani wenyewe. Watu huingizwa barabarani.

Den Haag ulisikia kina yakhe gani walikwenda kujibu ya watu kuingia barabarani Kenya?

Kwanini kama yamewashinda wasipishe hatamu za uongozi kwa wengine waone hii ngoma huchezwaje?

Kwani kuna siri - hakuna mafanikio bila uana harakati usiokoma. Maji yakikuzidi si unapisha tu? Hadi yakukute ufurushwe unceremoniously?
Mkuu,
Anzisha chama chako utekeleze hayo maono yako..
Sie tunajua Simba mwenda pole ndiye mla nyama!
 
Hakuna atajayeingia barabarani bila viongozi waliodhamiria watu kuingia barabarani.

Kenya 2007 watu waliingizwa barabarani. Kenya 2022 watu wametakiwa kuwa wavumilivu.

Watu hawaingii barabarani wenyewe. Watu huingizwa barabarani.

Den Haag ulisikia kina yakhe gani walikwenda kujibu ya watu kuingia barabarani Kenya?

Kwanini kama yamewashinda wasipishe hatamu za uongozi kwa wengine waone hii ngoma huchezwaje?

Kwani kuna siri - hakuna mafanikio bila uana harakati usiokoma. Maji yakikuzidi si unapisha tu? Hadi yakukute ufurushwe unceremoniously?

Unafananisha akili ya Mkenya na Mtanzania kweli?? Umekosea sana BrazaJ,,

Basi wewe huwajui Watanzania!! Watanzania wana akili za kikondoo, utamtoboa jichoni anakuangalia tu,,!!
 
Hakuna atajayeingia barabarani bila viongozi waliodhamiria watu kuingia barabarani.

Kenya 2007 watu waliingizwa barabarani. Kenya 2022 watu wametakiwa kuwa wavumilivu.

Watu hawaingii barabarani wenyewe. Watu huingizwa barabarani.

Den Haag ulisikia kina yakhe gani walikwenda kujibu ya watu kuingia barabarani Kenya?

Kwanini kama yamewashinda wasipishe hatamu za uongozi kwa wengine waone hii ngoma huchezwaje?

Kwani kuna siri - hakuna mafanikio bila uana harakati usiokoma. Maji yakikuzidi si unapisha tu? Hadi yakukute ufurushwe unceremoniously?
Watu waingizwe barabarani na nani,wapinzani wamehangaika sana hawakupewa support-sasa hivi ndio mnaona wa muhimu.
SAMIA ongeza kodi,na endelea zaidi hata VAT ongeza iwe 30% Watu akili ziwakae sawa.
 
Mbona watenda maovu wanajulikana na wanakejeli umma hadharani, kwanini mnalaumu wasiohusika?!

Wapi analaumiwa mtu? Mbona iko wazi? Uko madarakani huna sera au ufumbuzi toka wachukue wengine.

Hili lina apply kote serikalini na upinzani. Kama kumtoa Mwigulu hatua ya kwanza ni kuanza na wewe uliye hodhi namna yetu ya kulianzisha tatizo liko wapi kuanza na wewe?
 
Back
Top Bottom