Tufike mahali tutoleane uvivu wenyewe kwa wenyewe. Tufike mahali panya wamfunge paka kengele.
"Enyi viongozi wetu madarakani, mliochagua kukaa kimya na kututelekeza kondoo wenu, tokeni madarakani washike wenye kudhamiria."
Ikumbukwe wavumao baharini papa lakini na wengine wapo.
Imekuwa kuwalaumu vijana kwa kuendekeza mambo yasiyokuwa na tija kwa taifa, lakini je vijana hawa kwa uongozi upi wasimame imara wapi?
Ya nini kuendelea kumlaumu dobi, wakati kaniki ni rangi yake?
Misahafu inasema "nitampiga mchungaji na kondoo wa kundi watatawanyika."
Kondoo wametawanyika nani wa kuwakusanya?
Viongozi wanaohofia kufa au jela tafadhali wapishe madarakani. Damu mpya zipo. Hatuhitaji vyama vipya. Tubanane na hawa hawa. Hawataki kutoka madarakani, shime wanathaura tuanze kwa kuwafurusha wao kwanza.
Ziko wapi kauli zao? Iko wapi mikakati yao? Ziko wapi dira zao? Yako wapi maono yao? Nini tufanye au tuanzie wapi?
Ninakazia: tuna matatizo ya kiuongozi zaidi kuliko ya kujitoa kwa wafuasi.
Tumung'unye maneno hadi lini?
Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu
Mfano wa habari kamili ni huu:
CHADEMA: Bila kuwapa Makavu hakuna Katiba Mpya