Paul Makonda, Mwenezi wa CCM akiwa anazunguka nchi nzima kwa misafara mirefu kuliko kiongzi yeyote na kusikiliza kero na kuwalalamikia CCM wenzake kwa kutofanya kazi .
Mwanzo alianza na kulalamikia CHADEMA, AKAJA KWA MBOWE SASA wana CCM wenzie.
Makonda amewaambia wananchi na kuwaagiza wasipeleke kesi mahakmani kwakuwa hawana hela kama yeye ili kununua haki na kwamba hata yeye alidhulumiwa nyumba masaki lakini akaona asiende mahakamani maana hatapata haki.
Juzi hapa Makonda alielimishwa na Mh AG Eliezer Feleshi ambaye kama watu hawajui FELESHI ndiye Mshauri mkuu wa Nchi ya Tanzania.
Sasa Makonda kampanda kichwani, Mahalkama na AG, wamekaa kimya.
Hii kauli ya Makonda tunaweza kuitazama kwa angle nyingi lakini inauvua nguo mfumo wa haki nchini. Na unfortunately ni kauli ya kweli kabisa. Ndio, ni kauli ngumu lakini inaakisi tatizo la mfumo wetu wa utoaji haki.
Anachosema Makonda ni kuwa bila kuwa na pesa na connection, sahau HAKI. Ninachopingana na Makonda ni kuwa haki ipo serikalini, hii sio kweli. Wala serikali sio chombo cha kutoa haki, chombo cha haki ni mahakama/judiciary. Ni muhimili unaojitegemea. Tunahitaji kujenga mfumo wa mahakama ulio huru na unaosimamia kweli na usioegemea upande wowote. Rostam Aziz alisema kuhusu Mfumo wa mahakama kuwa umeoza akaambiwa akanushe Chap Sasa Mwenezi anaonesha panapovuja na ndio Uhalisia
Mfumo ambao haki siyo upendeleo bali ni fursa inayoweza kupatikana na kila mtu. Ni muhimu sasa, zaidi ya wakati wowote, kutafuta suluhu na kufanya mahakama zetu kuwa huru.Mbona Kenya wanaweza? Hawa si ni wenzetu tu wa eneo hili la Afrika mashariki? Makonda anasema mfumo wetu wa utoaji haki umeoza, inawezekana ni kweli. Basi turekebishe huo mfumo, tusiukimbie na kutengeneza mfumo mwingine. Hiyo sio solution.