Mahakama Kuu yafuta mashtaka 14 kati ya 25 ya Masheikh wa Uamusho

Ukiona wameachiwa... Ujuwe washadhibitiwa!!!..

Mda utaongea....

Sent from my TECNO CD6 using JamiiForums mobile app
Nlichokisikiaga mimi ni kuwa hao jamaa hawajasingiziwa kabisa.

Kumbuka walianza toka awamu ya Jk na Shein kule Zanzibar.

Jk akashauriwa na kupewa maelezo yote vile jamaa walivyohusika, na bila kutafakar mara mbili akaamua awaweke ndani.

Jk hakuwa mdini, kumbuka hata Shekh Pondo alkuwa akipambana na Utawala wa Jk na alikuwa akisulubiwa mno Shekh Ponda.

Hayat Magufuli alipokea tu kijiti kwa kuelezwa uhalisia wa hawa mashekh.

Sijajua hasa Rais Samia ni kitu amekiona ama kimepangwa juu ya hili jambo.
 
Kesi na kushikiliwa kws masheikh wa uamsho kunafikirisha sana (iwe Wana hatia au hawana). Iweje baada ya hao masheikh kukamatwa na kuhamishiwa Bara, Zanzibar kumekuwa shwari, yale mashambulio ya tindikali na risasi kwa wageni yamekoma kabisa.

Vv
Kaka, hawa jamaa walikutwa na hatia.

Kama sikosei ktk upelelezi wa hawa watu, Tz tulipata msaada nje ya nchi chini ya utawala wa Jk.

Na wale jamaa walitaka hawa wahukumiwe moja kwa moja wakae ndani ama wapotezwe mazima.

Kama sikosei baadhi yao walishatangulia.

Jk alipewa each n everthing kuhusu hawa watu, akaona ni sahihi wakae ndani.
 
Sio wanasheria ni maelekezo toka juu kwan? Hao wanasheria miaka yote walikua wap?
 
Hawa watu wako ndani toka 2014. Tuache kuishi uongo uongo

Wako ndani toka 2014.

Kipindi chote cha awamu ya mwendazake kaziba masikio na hakuona kuwa hawatendewi haki pamoja na makelele yote yaliyokuwapo?

Wangapi wengine zaidi mwendazake alihakikisha wanaendelea kuozea jela na kuishi kama mashetani?

Hiiiiii bagosha!
 
Wakikutwa hawana hatia watalipwa fidia ya kupotezewa muda kwa miaka waliyokaa ndani?
Kutolewa ndani ni fidia tosha! Wakileta zengwe warudishwe kula ugali wa serikali na kulima migomba na machungwa ya serikali huku wakifuga samaki
 

Wewe ni Wakili, naona umechemka kweli kweli! Unatulazimisha kusikiliza kesi ya Masheikh tu? Why! Kesi ni kesi tu haijalishi wewe ni nani! Kuwekwa kwao ndani kuna sababu!
 
Mnazunguka zunguka tu.

Masheikh wa UAMSHO wako ndani sababu ya MUUNGANO!

WALIUGUSA VIBAYA MUUNGANO!

Fuatilia video zao utaelewa.


Walikuwa wanawaamsha Wazanzibar kuachana na SIASA za u-CCM na u-CUF ambazo zilikuwa zinawagawa na kwamba adui wa kweli wa Taifa lao ni MUUNGANO!

Na Wazanzibari kwa wingi wao walianza kuwaelewa.
Yaani wasingewekwa ndani; pengine hivi tunavyoongea huu MUUNGANO, hata Kama ungekuwepo, usingekuwa hivi ulivyo!

Dini ilitumika Kama kiungo tu kwavile majority ya Wazenji ni Muslims. Ukiwakusanya Kama waislam inakuwa rahisi kuzungumza 'lugha' moja!
 
Dare to Struggle and dare to Win [emoji123][emoji106]
 
Acha wewe kuongea kiebrania kama unaona ni utumwa...mwenzako akiongea kiaraabu usiumie hayo ni maamuzi yake kwani hajavunja sheria yeyote.
Nikuulize Ndugu kweni Mungu ni Kabila gani?
 
Kwi hao mashehe wa uamsho wamejifunza mengi kwa kukaa rumande hata wakiachiwa huru leo hatutasikia tena watu wakipigwa risasi na kuuawa ovyo ovyo kama wakati ule walipoanzisha uamsho wao
Kwani wao walihusika? Je huo ushahidi Polisi haina wakatiwa hatiani na kuhukumiwa ?

Hanna kesi palé, ni kesi ya kisiasa tu .
 
Uko sahihi kabisa na umetoa hoja muhimu sana. Inauma sana kuwatesa watu pasipo kuwafungulia mashitaka ili wakipatikana na hatia wafungwe kwa mujibu wa sheria na kama hawana watolewe. Tusiwageuze mahabusu kuwa wafungwa. Ni kosa, ni dhambi na ni dhuluma kubwa!
 
Lakini ingefaa zaidi washtakiwe rasmi na kufungwa kama wana hatia, kuliko kuwasotesha tu mahabusu pasipo kuhukumiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…