Mahakama Kuu yafuta mashtaka 14 kati ya 25 ya Masheikh wa Uamusho

Ni sawa sawa na wakristo waseme injili ni English, kwamba ujifunze kwa kiingereza kwanza halafu ndio uje kiswahili. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sasa kuna point gani utumie lugha ngumu kujifunza jambo halafu unakuja tena kutafasiri kwa lugha yako wakati ungetumia tu shortcut kujifunza kwa lugha yako...
 
Kumwagia tindikali watalii ni economic sabotage, kama ikidhibitika pasi na shaka walifanya hivyo, wataozea jela
Sidhani kama ni wao walifanya pengine ni mashabiki wao. Ila ni vema hawa mashehe wakawajibishwa kwa makosa yao na sio kujivika vazi la utakatifu ile hali wanajua kuwa walianzisha ghasia kwa sura ya kusimamia haki au dini.

Hakuna mkosaji wa makusudi anaeonewa huruma mbele ya sheria. Unapokosea tegemea sheria ikuwajibishe. Mbele ya sheria hakina umri, jinsia, imani, wadhifa, uraia au sijui nini, ukikosea wewe ni kuwajibishwa.
 
Ni wakati gani zanzibar watu walipigwa risasi na kuuawa "ovyo ovyo" ? Habari hii umeipata wapi na sisi ambao hatujawahi kuisikia tukaisome ??
Kipindi wakiwa active kule zanzibar kulikuwa na matukio ya wafuasi wao kushambulia watu kwa itikadi zao binafsi. Kuwashambulia watalii, mauwaji ya raia wa kigeni kama wale wa ufaransa, kushambuliwa kwa mapadre na kuchomwa kwa makanisa, kumwagwa uchafu makaburi ya wakristo kule zanzibar.

Na kadhalika. Kama haya matukio hukuyaona then haujui kitu kuhusu makundi ya uamisho na shughuli zao kipindi kile au pengine ulikuwa mdogo.
 
Ila tukubaliane walikamatwa enzi za Kikwete na wameachiwa utawala wa Mama
 
Ni sawa na Asalaam aleykum sio Kiswahili Asalam alekum ni kiswahili
Katika kiswahili hatuna maneno yenye Consonants tupu bila vowels.

Vowels ni zile a e i o u. Na consonants ni zile herufi zinazobakia.....

So huwezi kuta neno la kiswahili lina ishia na consonants bila Vowels mwishoni.

Kama unabisha nipe hilo neno hapa nikupe kinyuko cha kitaaluma...

Sasa haleluya imeanza na consonant H na imeishia na Vowel A, wewe asalaam imeanza na Vowel imeisha na Consonant unaniambiaje hilo ni neno la kiswahili....

Aleykum inaanza na Vowel A inaishia na consonant M, ni wapi umejifunza kiswahili cha kuunda maneno kwa kanuni hii....?!
 
Sasa haleluya imeanza na consonant H na imeishia na Vowel A, wewe asalaam imeanza na Vowel imeisha na Consonant unaniambiaje hilo ni neno la kiswahili
Tuache kuremba yote hayo ni maneno ya Kigeni
 
Tuache kuremba yote hayo ni maneno ya Kigeni
Kubali haujui ufunzwe ndugu..... Mbona ni rahisi tu kukubali sote tukaridhika. Mpe mtu anachotaka akupe unachotaka. Me ninachotaka ni kukurekebisha ulipokosea wewe unachotaka ni kujifunza ila unataka kuonekana haujakosea.... [emoji23][emoji23][emoji23]
 
kwani kwa miaka yote hio hawakujua hayo mashitaka 14 yalikua sio ya kweli? kwani hao wanasheria wa Serikali na DPP wasiwajibishwe
 
Maneno ya Lugha tufundishsne kwa Kamusi
 

Duuh. Walifanya mini?
Kwa kutowatendea haki wowote wale akiwa kwenye nafasi hiyo mwendazake hawezi kukwepa lawama.

Hii ni kama ambavyo leo mama Samia hatakwepa lawama akiamua kupuuzia miito ya wazi inayosikika mno yakuhitajika haki kwa watu.

Kuna mambo tunamsingizia. Issue nyingine maji yanazidi unga.
Hawa wanaburuzwa hivi sababu gani? Ni zaidi ya mwendazake. JK alikuwa anajua. Naamini kama wanaonewa angewaachia huru.
 
Hiki ulichoandika hapa ndio kinajibu

watu walipigwa risasi na kuuawa "ovyo ovyo"?
 
Baadhi yetu ..tunawapeleka mahakaman na mitutu tumeishkilia vyema!!!!?

Lakin nafsi zetu hazikubalian kabisa na kinachowapata!!!!!(tunaumia )lkn~
Tunatimiza wajibu:
 
Hao jamaa imeonekana walikuwa wakijuhusisha 100% na mambo ya ugaidi.

JK na Shein hawakufanya makosa kuwaweka ndani aisee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ndio utopolo Sasa!

Unaposema "imeonekana walikuwa wakijihusisha 100% na Mambo ya ugaidi..." maana yake upo ushahidi wa kuwatia hatiani.

Sasa, hii nchi ina sheria ya ugaidi na hukumu zake kisheria zipo. Kwanini kesi inapigwa danadana hukumu haitolewi..?!

Tusiache hisia zetu zituendeshe!
 
Hongera na pole zao, ila tukumbuke, dola huwa haipimwi halafu ukataka haki! Fundisho kwetu wote..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…