Wakuu hamjambo?
Naandika Uzi huu nikiwa na huzuni kubwa ya kutokulidhishwa na hukumu iliyotolewa kwa Mbowe Na viongozi wenzake,binafsi nikifikilia kuhusu vurugu zilizo himizwa na viongozi wa chadema hadi kupelekea kifo cha binti akwilina naumia sana.
Kwa hukumu iliyotolewa Leo ikilinganishwa na uhai wa binti yetu akwilini naona kama haviendani,hukumu ya maisha kwa Mbowe Na viongozi wenzake ndiyo ilikuwa suruhu katika kuweka mambo sawa, hii ni kutokana na athari mbaya zilizojitokeza kutokana na uana harakati uchwara wa akina Mbowe Na wenzake.
Swali langu ni kuwa,je Kama raia naruhusiwa kukata rufaa kutokana na kutokulidhishwa na hukumu iliyotolewa kwa viongozi hawa,kwani naona milioni 350 au jela miezi mitano ni hukumu ambayo haikuzingatia uzito wa kosa,na haijawatendea haki wazazi na ndugu wa binti akwilina.
Wataalamu wa sheria nijuzeni.
Sent using
Jamii Forums mobile app