Mahakama yaamuru Eng. Hersi aachie ngazi Yanga!

Mahakama yaamuru Eng. Hersi aachie ngazi Yanga!

Serikali ishajua kivuli chake ni simba na Yanga, ndo mambo yanayowapumbaza wananchi wake, baada ya Simba kutawala soka miaka minne ikaja zamu ya yanga, kwa mwendo wa eng hersi wanaona kabisa huyu anaweza kutawala soka hata miaka 10, makolo wapate depression waingie mtaani kama gen Z wa kenya, Bora wamtoe makolo wapate hata ahueni kidogo, and the circle goes on
Sjawahi kuona akili mbovu kama za kwako. Sasa unailaumu serikali kuwatumia hizi timu kuwapumbaza wananchi, ulivyo andazi hapa umeleta udhibitisho kwamba serikali imefanikiwa kweli kukupumbaza wewe na wenzako ambao hamna mbele wala nyuma
 
Eng asikimbie, kama shida ni kofia mbili aachane na GSM.
 
1721163949588.jpg

Mzee Magoma akiwa katika pozi la kupokea kiti cha Uraisi 😁😁😁
#Ubayaubwela
 
Safi xnaaa muanze kua busy na matatizo .waizi wa wachezaji nyie
Kuna namna naiona wachezaji hasa wa Simba na hasa wa kigeni kushawishiwa na timu ingine ili waifikirie hiyo timu.
CEO Masingisa was gone
Manara was gone
Chama is gone
Baleke is happy now
Innonga was not happy at the end
Sio maadili ya timu kuwashawishi wachezaji wa timu ingine wakiwa wanaitumikia timu yao
Ubaya Ubwela
 
Hiyo kesi ilikuwa inasikilizwa upande mmoja? Halafu hukumu ya Mahakama inayojiamini isingeamuru waachie ngazi bali ingebatilisha uongozi uliopo, unaamuruje uongozi kuachia ngazi wakati hukumu haijabatilisha?
Kata rufaa nenda ukayaseme haya mahakamani,, hakuna janja janja, maamuzi ya mahakama lazima yaheshimiwe
 
Itakuw hao wazee ni misukule ya makolo iliyo kufa zamani inataka kuharibu mipango ya club yetu mbona sisi wazee wa yang tuko uku tumetulia tu
Ubaya ubwela. Si mnataka roho mbaya..mamaeh. kila mtu ashinde mechi zake
 
Kata rufaa nenda ukayaseme haya mahakamani,, hakuna janja janja, maamuzi ya mahakama lazima yaheshimiwe
Rufaa ni sehemu ya kutafuta haki au uhalali, ila niliyoyaandika yanamilikia ujinga uliomo na hivyo rufaa kuwa nyepesi zaidi.
Ni hayawani tu anayeweza akashangilia hili akiona kuwa ni bundi katua Jangwani. Bundi wa Jangwani alishapugwa manati kitambo
 
View attachment 3044264
Mzee Magoma akiwa katika pozi la kupokea kiti cha Uraisi 😁😁😁
#Ubayaubwela
Ataweza akiachiwa timu ?
Huwa nastaajabu sana
Kama timu inafanya vizuri na pesa ipo Kuna shida gani kuendelea na viongozi waliopo?
Na kama Kuna shida ya kikatiba ni kwanini msikae pamoja muone namna ya kuitatua bila mgogolo?
 
Haya mambo bana kumbe hivi vilabu vinawenyewe wata walidandia na kwenda na upepo tuu.
 
View attachment 3044226

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, imeamuru Uongozi wa Club ya Yanga ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi na wenzake, kuachia ngazi na kuondoka kwenye Club hiyo kwakuwa Katiba ya Yanga haitambui uwepo wao.

Imedaiwa kuwa uamuzi huu wa Mahakama umekuja baada ya Kundi la Wazee wachache waliowahi kuwa Wazee wa Yanga kipindi cha nyuma, kushitaki Mahakamani likidai uwepo wa Viongozi wa sasa wa Yanga (Injinia Hersi na wenzake) ni batili na haujafuata Katiba ya Club hiyo.

Kutokana na Wazee hao kushinda kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inamaana kuwa Rais wa Yanga Injinia Hersi na Viongozi wenzake wanatakiwa kuachia ngazi na kukabidhi Ofisi kuanzia sasa.

Injinia Hersi alianza kuiongoza Yanga kama Rais miaka miwili iliyopita baada ya kushinda nafasi hiyo akiwa ni Mgombea pekee July 2022 na kumfanya kuwa Rais wa kwanza wa Yanga SC toka kuanza kwa mfumo mpya wa mabadiliko ambapo alitangazwa kuwa atakuwa madarakani kwa miaka minne ( hadi 2026 ) kwa mujibu wa Katiba ya Club hiyo.

Source: #MillardAyoUPDATES

====


Source nyingine:
Wanachama wawili wa Yanga SC JUMA MAGOMA na GEOFREY MWAIPOPO walishinda kesi waliyofungua katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar mwaka jana mwezi Agosti. Kesi yao ilikuwa dhidi ya Baraza la wadhamini la klabu hiyo kuikabidhi klabu kwa mtu wasiyemjua wala asiyekuwa Mwanachama wakati kesi inafunguliwa mwezi Mei mwaka 2022 siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa klabu uliomuweka madarakani Rais wa Yanga Eng Hersi Said. Awali walifungua kesi hiyo Mahakama ya Wilaya ya Ilala iliyopo Kinyerezi jijini Dar, kabla ya kushauriwa kuihamishia katika Mahakama ya Kisutu.

Walipinga kutumika kwa katiba ya mwaka 2020 ambayo ilitumika kwenye uchaguzi Mkuu uliouweka uongozi uliopo madarakani wakisema katiba hiyo sio halali. Inasemekana RITA waliitwa kutoa ushahidi na wakasema wanaifahamu katiba ya mwaka 2011 ambayo ipo ofisini kwao na hiyo ya mwaka 2020 hawaitambui.

Baada ya kupata hukumu yao mwezi Agosti mwaka 2023 JUMA MAGOMA NA GEOFREY MWAIPOPO wameona hakuna utekelezaji wa hukumu hiyo hata baada ya kuwasilisha kwa wahusika wakaamua kufungua kesi ya kukazia hukumu ambapo itatolewa maamuzi mwezi Agosti tarehe 5 mwaka 2024, ili hukumu hiyo ianze kufanya kazi. Ambapo inategemewa Mkutano Mkuu wa Yanga kuitwa ambao utajumuisha WANACHAMA WOTE HAI sio wawakilishi wa matawi pekee (kama ilivyo sasa) na kwenda kwenye uchaguzi mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa klabu kwa kufuata katiba ya mwaka 2011.

Kama hili litatokea manake Eng Hersi na timu yake watakuwa wameondoshwa madarakani kwakuwa watakuwa wameingia isivyo halali.
View attachment 3044242
Siku ya kwenda kutoa vitu vya ally kamwe jagwani pale mniambie!
Nitajitolea nauli za vijana kwenda kumtoa kwa nguvu pale!
 
Back
Top Bottom