Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Alikopa 300mil anadaiwa 100mil, maana yake ameshalipa 200mil.

Harmonize mhuni tu, ila anauwezo kabisa wakulipa hili deni tena kwa mara moja, dogo hela anayo sema mambo mengi tu.

Watoto wa mjini wanafahamu, sio Kila aliyeshindwa kulipa deni bank Hana hela, wengine wanaleta uhuni, ipo michezo ya collateral zisizolingana na thamani ya mkopo na mwisho wasiku wanaachiwa bank wapambane nazo.

Kiukweli vipaji vinawalipa sana hawa vijana na wanapata sana hela ndio vile tu ujana maji ya moto, lakini muziki unawalipa sana Kwa namna nyingi sana, kuanzia shows, matangazo, connections nk.
 
watu wanajisahau kua mkopo ni hela ambayo si yako
Sasa kama ni kweli hauna hiyo pesa ya kulipa huo mkopo utafanyaje na mipango yako imekwenda ndivyo sivyo!!?? Mikopo safe ni bado ile ya ajira,yaani kibarua chako ndiyo kinakuzamini kutokana na Mshahara wako wa kila mwezi! HR ndiyo anasimamia show yote na wwe kazi yako ni kuangalia ile amount ulio taka na.ku sign tu!!
 
Haya ndio matatizo ya kupata pesa nyingi ukiwa bado umri mdogo.Bank hawawezi kuwa wajinga kiasi hicho kumkopesha mtu bila dhamana,vinginevyo kuna nguvu kutoka serikalini ilitumika,na dogo kwakuwa ana ka ushamba flani ka asili anaona kutokulipa ni ujanja,kumbe hajui hilo linaweza kuwa ndio anguko lake...
na benki mpaka wanamwanika walishaona red light mbele, kiufupi wameshalijua anguko lake hata kimuziki na fame.
 
Hivi taaluma ni nini kwa kiswahili?
1723959959651.png
 
Ila Harmonize ni mtata kwenye kulipa madeni, nakumbuka miaka kadhaa hapo nyuma amewahi kukimbia deni la kodi ya nyumba aliyokuwa akiishi huko Mbezi Beach kwa Mchagga mmoja kama 150 Milioni hivi.
Hii sio kwamba inithibitisha wasanii hawana hela tofauti na vile ambavyo huwa wanajinasibu mitandaoni?
 
Back
Top Bottom