Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

Mahakama yamtia hatiani Harmonize, atakiwa kuilipa mamilioni CRDB!

duwh juz kati nilikutananae classic mall yuko na range moja matata kaingia crdb moja kwa kwenye getto la branch manager tukasema dah mwamba kishapita level za kukaa kwente mnyororo yeye fungu anaenda kuchukulia kwa wakubwa kabisa.
kumbe muhuni ana majanga makubwa kuliko sisi
Wahuni Bado Wapo Wengi Sana, Kukopa Harusi Kulipa Matanga
 
Na wanafanya upuuzi kwakuwa wana backup ya wanasiasa wakubwa nchini, sijui walitumia vigezo gani kumpa mil300

Na wanafanya upuuzi kwakuwa wana backup ya wanasiasa wakubwa nchini, sijui walitumia vigezo gani kumpa mil300
Mimi ningekuwa wewe ningejiuliza; je, benki wanaweza wakanipa mimi milioni mia tatu? Ukipata utajua vigezo pia ukikosa utajifunza kuwa na vigezo vinavyo hitajika. Soma post namba 17
 
Nje ya mada kuna jamaa kapiga hesabu ya muda * riba + mkopo ili kupata rejesho la jumla

Muda - 3 years
Riba - 18%

Kisha akahitimisha kwamba mkopo wa 300M inatakiwa kurejesha 354M kwa miaka 3.

Mimi nina experience na industry ya Fintech (mfano mkopo wa kampuni kama za Watu Simu, Watu Pikipiki, Laina, Branch etc)
Na kwa Fintec huu mkopo unapigiwa hesabu kwa mtindo huu mkopo/muda+mkopo*riba. Hapa tunataka kuona kila mwaka mteja atalipa sh ngapi

300,000,000 / 3 + 300,000,000 * 0.18 = 154,000,000

This means kwa huu mkopo wa Harmonize alitakiwa kulipa 154,000,000 kila mwaka kwa miaka 3. Ambapo jumla inakuja 462,000,000

Hivyo jumla ya rejesho la mkopo wa 300M ni 462M kwa miaka 3.

Kama kuna mtu wa benki aconfirm, but hii ndiyo sababu mikopo huonekana mwiba kwakua watu wengi hawaulizi hesabu za kweli ili wajue kiukweli malipo yatakua sh ngapi
Sijui huo ukoje ila mimi nimekopa CRDB Kwa dhamana ya ajira, mkopo ulikuwa 6,000,000/= (miaka miwili)
Makato kwa mwezi ni 285,000X24=6,840,000
Riba hapo Kwa miaka miwili ni asilimia 14
 
hawana lolote hao CRDB

wangekuwa wanajua banking and lending wangeshikilia dhamana

Konde Boy, wapige kisawa sawa hao wasomi uchwara wa CRDB

Walikutaka ufungue akaunti ya. biashara ili waone miamala yote ya maokoto na ma bills ya kampuni.

Biashara went burst, and they see all the accounting records, what they what you to do, rob the bank to pay the bank ?

Wamezoea predatory lending kwa wanyonge wasio na sauti. Konde, kaza hapo hapo. We don't commiserate with these predatory banks. Eff them!
Samahani mkuu ningeomba ufafanue zaidi maana kuna kitu kwenye comment yako imenifikirisha sana. Kuna vitu vizito umeviongea ila kwa lugha ya uficho. Nina jirani yangu kanasa kwenye mkopo wa bank yaani wanavutana na bank kesi bado mbichi , jamaa kalamba 170M. Kwa hìvyo naomba utoe elimu hapo kuna jambo litanisaidia. Asante mkuu.
 
Upuuzi kabisa mtu unakuta anatamba eti kazi ya ualimu ni kazi ya Laana,Sasa tangu nizaliwe sijawahi sikia mwalimu kafikishwa mahakamani Kwa kushindwa kulipa mkopo wa benki au kauziwa assets zake Kwa kushindwa kurejesha mikopo ya benki.


Sasa Harmonize kashindwa kulipa M 100,Huu upuuzi,Sitaicha kazi ya ualimu kamwe,hapa navuta Muda nije niende nikavute mpunga M 32 nione mtu ananilaumu Kwa kutegemea mikopo , nijivinjari zaidi.Asante Mungu kwa kazi ya ualimu,Kiufupi huwezi toboa maisha bila kukopa ,kama unakopesheka kopa
Kabisa ,bila mikopo hatutoboi hata kidogo
 
Back
Top Bottom