Mahakama yamuachia huru Lengai Ole Sabaya, yasema ushahidi wa Jamhuri una utata
Serikali ya vilaza

Hatima ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi inatarajiwa kujulikana leo Juni 10, 2022.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iliyokuwa ikisikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2021 imepanga kwa mara ya pili kutoa hukumu hiyo.

Awali, Mei 31, 2022. Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo, Patricia Kisinda aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo, alipanga kutoa hukumu lakini ilishindikana kutokana na kudaiwa kuwa nje ya kituo cha kazi kwa majukumu mengine.

Sabaya na wenzake walikuwa wakisubiri hukumu hiyo endapo wangeachiwa huru au la, kabla ya kufunguliwa kesi nyingine na wenzake watano ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Juni Mosi, 2022

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Fadhil Mbelwa akiahirisha kesi hiyo Mei 31, 2022 alisema hakimu aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo amepangiwa majukumu mengine nje ya kituo cha kazi hivyo hukumu hiyo itatolewa leo.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa baada ya kesi hiyo kusikilizwa kwa miezi saba tangu ilipoanza Julai, 2021.

Sabaya alikamatwa Mei 27, 2022, Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam na kufikishwa mahakamani Juni 4, 2021 na kufunguliwa kesi mbili tofauti.

Katika kesi ya kwanza walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, hukumu ambayo Mei 6, 2022 ilitenguliwa na Mahakama Kuu na kuwaachia huru baada ya kubaini dosari.


============================

SABAYA NA WENZAKE WAACHIWA HURU

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya pamoja na wenzake sita waliokuwa wanakabiliwa na Kesi ya Uhujumu Uchumi.

Mahakama imesema ushahidi uliotolewa na Mashahidi wa upande wa Jamhuri ulikuwa na utata. Pia imeelezwa kuwa Hati ya Mashtaka ilikuwa na mapungufu ya Kisheria.

Hata hivyo, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu, John Aweyo na Nathan Msuya wataendelea kubaki Mahabusu kutokana na Kesi nyingine ya Uhujumu Uchumi waliyonayo Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi.
[/QUOTESerukalier
 
Wananchi wa Arusha wampongeza mwenyekiti.mstaafu wa UVCCM mikoani jump Dr Ole Sabaya kea mafanikio anayopata dhidi ya Kesi zinazomkabili.

Wananchi wamedai kuishinda serikali mahakamani bila DPP kuingilia kati kwa kutokuwa.na nia ya Kesi siyo jambo dogo

Kwa sasa Ole Sabaya ameokoka
Hata hivyo, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu, John Aweyo na Nathan Msuya wataendelea kubaki Mahabusu kutokana na Kesi nyingine ya Uhujumu Uchumi waliyonayo Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi
 
Hata hivyo, Sabaya na wenzake Sylvester Nyegu, John Aweyo na Nathan Msuya wataendelea kubaki Mahabusu kutokana na Kesi nyingine ya Uhujumu Uchumi waliyonayo Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi
Hata hivyo Mbowe anaweza kurudishwa mahakamani DPP atakapoona inafaa!
 
Sabaya anatengenezewa mazingira ya kuachiwa huru Kila mwenye akili anaelewa hilo. Tanzania jela zina waendaji sio kila mtu
 
Mahakama zinatumika vibaya.

Jaji mkuu anapaswa kumkemea DPP aache kutumia mahakama kunyanyasa Raia.

Haya ni matumizi mabaya ya vyombo vya Serikali.
Ndio mnajua Leo? Kipindi Mbowe anasota gerezani mkimuita Gaidi mbona mlitaka tuheshimu uhuru wa mahakama?
 
Wananchi wa Arusha wampongeza mwenyekiti.mstaafu wa UVCCM mikoani jump Dr Ole Sabaya kea mafanikio anayopata dhidi ya Kesi zinazomkabili.

Wananchi wamedai kuishinda serikali mahakamani bila DPP kuingilia kati kwa kutokuwa.na nia ya Kesi siyo jambo dogo

Kwa sasa Ole Sabaya ameokoka
Endelea kuota mchana huu
 
HahhA... Samia ilibidi awaite viongozi wa Dini Ikulu wamuombee mbowe msamaha baada ya Chadema kumshambulia Zito na kusema hawataki msamaha..
Ila nampongeza maana aliamua kuweka pride pembeni na kumuachia

Kwa Sabaya sina uhakika kama ni lobbying inafanyika ama ni kulialia kwa wale wamama waliojiita ndugu zake ndio imefanya kazi ama ni ushahidi kweli hautoshi

Ila cha muhimu ni kuwa yule hayawani aliyekuwa anamtuma keshalamba mchanga na amejuta
 
Back
Top Bottom