Mahakama yamuumbua waziri Magufuli na sheria zake za uongo

binafsi nimekua mtetez mzuri wa ,agufuli lakini kwa fact huyu jamaa alizoziweka siwez pinga moja kwa moja hayuko sahihi maana kila kitu amejitaidi kukiweka sawa... ni kweli likua inasikitisha mtua leo aambiew mvamiz kwa sheria ya mwaka 67 wakat anaanza kukaa maneno hayo kulikua pori kabisa hata barabara watu walizianzisha wenyewe tu na kama ruling kweli imetolewa na mahakama basi magufuli inabidi ashauliwe vizuri na timu yake ya wanasheria na ikibid arud nyuma still he is the right man for the job!!!
 
unabisha.mambo haya yashajadiliwa sana humu na kwenye vyombo vya habari,sasa bisha maana ndiye aliyekuwa waziri mwenye dhamana kipindi hicho.kama siasa umeanza kufuatilia juzi sawa.subiri
Maneno matupu hayavunji mfupa hizo tuhuma za kutengeneza na kusadikika hazina nafasi kwenye dunia ya leo jipange tena.
 

nasikitika sana nimeulizwa swali zuri sana kutoka kwa ID ambayo huwa sipotezi muda wangu kubishana nayo.angekuwa kaniuliza swali hili mtu mwingine ningemjibu tena nasikitika swali hili nilipaswa kulijibu ila ni bora nikae kimya kuliko kujibu hii ID ya Simiyu Yetu.mnisamehe wanajf,kuna watu wakishaonekana humu wengi wetu huwa tunakosa hata apetite ya kulog in jf,haya mkuu Simiyu,endelea kutapika humu,hili jukwaa la siasa tulishawaachieni nyinyi.
 
Last edited by a moderator:
Mnafiki na mzandiki tu huyu Maghufuri hana lolote ni kupenda sifa kwa kuwaonesha ubabe raia wengine. Naona mara hii ametegwa akategeka
 
Hivi umemsoma ameandika nini au umekurupuka na kutapika tu.

Unahitaji kujua kuwa ujumla wa maelezo ya mtoa thread ni kumnanga Magufuli kwa kile alichokikosea bila kujali yale mazuri aliyowahi kuyafanya ambayo bila shaka ni mengi
 
Hakuna waziri mkweli CCM wote ni uongo kwa mbele dhuluma na fitina Raisi Mwongo, Makamu mwongo waziri mwongo vivyo magufuli ukiona mto anaongea huku anazingusha macho kila upande juwa muongo mahakama kuu kitengo cha ardhi wamefanya vyema kumstopisha mtu anayetesa watanzania
 



​
 
Reactions: UTC

Ahsante kwa ili mkuu!wewe u mwerevu sana!nimeipenda hii
 
Last edited by a moderator:

Hata siku moja usitegemee wapinzani au wanasiasa wa aina yoyote kubabaikia kitu ambacho hakina athari ya moja kwa moja katika uchaguzi au kumuingiza ikulu; watu wako bize kwenda ikulu bhana malori na hifadhi ndio kitu gani tena hicho kama sio kuzinguana makufuli ruksa kunyanyasa mradi asiguse mkono wa wanasiasa
 
Watanganyika mna tabiya ya kumfagilia mtu pas na sifa,Magufu Pombe hamna kitu alivunja sheli Mwanza then jamaa akenda mahakamani akalipw fidia ya kumwag jamaa alipig hesab kam kashafany biashara Pombe hafai ht mjumbe wa nyumba 10,WATANABE UMEELEZA UKWELI
 
Maelezo yako ni mazuri japo marefu sana! Nadhani umekuwa too much negative than reality.... kazi nzuri ya Magufuli hakuna asiyeijua. Unapoponda kiasi hiki hata kama kuna ukweli flani, wewe ndo unaonekana mzushi tu.....

Akili zingine za kushikiwa ni kama hizi.wewe unataka mleta facts hizi akufurahishe,achakachue maelezo ili wewe mvivu wa kusoma upate mteremko?Yeye kawakilisha kilichoamuliwa na kutafsiriwa na mahakama wewe unataka upapaswe ili ufurahi?
 
Magufuli hana tofauti na magamba mwenzake..

Anaonea maskini tu kama kweli yeye kidume mbona kaigwaya Tanesco corporate head office Ubungo..

Aache siasa kama yeye kidume mbona hajakemea Strabag inavyoziba ziba barabara na wanafanya kazi polepole tena mchana tu, usiku wanalala zao tofauti na kampuni zingine za ujenzi wa barabara na kwa jinsi wanavyotaka.. Anaonea vikampuni uchwara kupiga mikwara..

Aguse Strabag aone atachofanywa na World Bank chezea Kampuni zenye mtaji kuliko serikali yake iliyomwajiri..

Huyu nae Gamba tu anapenda sifa za kijinga lakini hana lolote..

Strabag ipo same level duniani na kampuni za nguvu kama Toyota, Sony, Samsung, coca cola etc duniani so hata kama wakiwa wanachelewesha kazi mnakaaa kimyaa kama hamuoni vile ndio magufuli kilichomkuta
 

Nakushukuru sana UTC angalau sasa uzi huu unaanza kupata serious discussants wenye kuweka vielelezo pia. Ni kweli kuwa mwaka 2007 Sheria mpya ya barabara iliweka upan huo kama hifadhi ya barabara. The burning issue katika mjadala huu ni kuwa ardhi ni mali ya nani? Toka mwaka 2000 Mhe Magufuli alipoteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi kwa mara ya kwanza amekuwa akidai kwa mujibu wa Sheria za mwaka 1932,40,42,46,57,na 67 kupitia The Highaway Ordinance Cap 167 GN 161 ya 5/5/67 ardhi hiyo ni mali ya Serikali na wananchi wamevamia barabara.

Sisis wananchi ulikuwa tukipinga na kudai ana tuonea ardhi hiyo ni mali yetu kwa kuwa hakuna aliyejileta bali tulihamishwa kwa nguvu toa maporini na kuja kulindikwa mabarabarani katika vijiji vya ujamaa na Mwl Myerere. Sasa Mahakama imetamka wazi kuwa kupitia Sheria ya Arhi ya Vijiji Na 5 ya 1999 ardhi iliyko pembezoni mwa barabara ni mali ya wananchi na mita 30 tu toka katika ya barabara ndio inaweza kuwa hifadhi ya barabara kama TANROAD itawajazia wamiliki wa ardhi hiyo fome maalum za fidia na kuwalipa fidia stahili ndipo waondoke.

Kwa kuwa mahakama imetamka wazi kuwa Kanuni "The Highway Ordinance Cap 167 GN 161 ya 5/5/67" ambayo kwa muda wote tokea mwaka 2000 Mhe Magufuli amekuwa akitunyanyasa nayo ilipoteza nguvu tokea mwaka 1999 mara tu baada ya kupitishwa kwa sheria ya ardhi ya vijiji ni dhahiri kuwa vipimo vilivyomo ndani ya Sheria ya barabara ya na 13 ya 2007 moja kwa moja vinaingia katika ardhi ya wananchi hivyo wanastahili kulipwa fidia kinyume na madai ya mauda mrefu ya Mhe Magufuli.

Pili kuhusu lane 18 nilitaka wasomaji wangu muelewe kuwa Mita 30 zilizotamkwa na Mahakama kuwa ndio zinzweza kuwa hifadhi ya barabara kama TANROAD watawalipa wananchi fidia zinatosha kwa ajili ya upanuzi wa barabara kwa miaka hata 100 ijayo.
 
Hivi umemsoma ameandika nini au umekurupuka na kutapika tu.
Kuna tatizo kubwa kwa baadhi ya wachangiaji kumshambulia mtu badala ya kujibu au kujadili hoja. Wengine hata hawasomi mada nzima wakisha ona kichwa cha mada tu wanajibu. Mada imejieleza vizuri kwa hoja na vifungu vya sheria na uamuzi wa mahakama sasa huyo jamaa inaonekana ni shabiki wa magufuli. Mbona hasemi mahakama ina uwezo mdogo wa kufikiria?
 
Kesi ni 2005, kesi imeendeshwa kwa miaka mingapi? Reference ya 2007 yawezekana ikatumika kwa namna moja au nyingine.

Nakushukuru kwa kinisaidia kumjibu lyxeffect 22 kama nilivyomjibu UTC the burning issue ni kuwa hadi sasa ardhi ji mali ya nani na nani anawajibika kufanya lipi ili kifanya ardhi hiyo kuwa ni hifadhi ya barabara. Mahakama imatamka kuwa kwa mujibu wa Kifungu cha 15 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na 5 ya 1999 toka tarehe 01 Januari 1970 sheria zote hapa nchini zilizpoteza nguvu juu ya ardhi za vijiji. Hivyo Tofauti na madai ya mara kwa mara ya Mhe Magufuli kuwa watu wamevamia barabara, hiyo sio kweli wananchi wameweza kuithibitishia mahakama kuwa walitolewa maprini kwa mitu ya bunduki na Serikali na kuja kulundikwa katika vijiji mabarabarani hivyo wana haki ya kulipwa fidia kama Wizara ya Ujenzi inataka kujaenga barabara kama ambavyo wamekuwa wakifanya mawaziri wote waliomtangulia na kuja baada ya Mhe Magufuli. Ni yeye pekee anayesigina haki za wananchi.

Kwa hiyo lyneffect 22 asiwe na wasi wasi Mahakama imeelza utaratibu wa TANROAD kutuma ili kuhamisha ardhi hiyo toka ardhi ya Kijiji kuwa hifadhi ya barabara kwa mujibu wa sheria ya barabara Na 13 ya 2007.
 
Hivi umemsoma ameandika nini au umekurupuka na kutapika tu.

Wako watu wengi anbao hupenda kutumia hisia badala ya ubongo hasa pale kilichoandikwa ni kirefu au kimeandikwa kwa lugha ya kigeni. Hivi Magufuli uzamili yake ni ya sheria au? Angekuwa amemsikiliza rais alipomwambia atumie na utu vilevile haya yasingempata. Mwisho wa kupenda sifa ni aibu.
 

Ndugu JUVE 2002 umeongelea mambo ya msinga sana katika majibu yako kuhusu watu kukoseshwa fidia za ardhi, nyumba, maji, barabara za kinglia ma,wao n.k. Naomba niwahahkikishie ndugu zangu kuwa katika mradi huu wa mabasi ya kwenda kazi hapakutakiwa hata mtu mmoja kuathiri kwa namna yoyote ile kwa sababu Benki ua Dunia inao sera yake iitwayo World Bnak Operational Policy 4.12 for involuntary Resettelement inyoweza kupatikana katika Ext Opmanual - OP 4.12 - Involuntary Resettlement

Kabla mradi wowote mkubwa haujafadhiliwa na Benki ya Dunia hfanyika Resetlemnet Plan ambayo hupaswa kuwa shirikishi kwa wadau wote watakaoathriwa na mradi huo na kukabalina namna ya kupunguza athari za aina yoyote zizkzowapata watu as a result of the project. Kwa hakika Benki ya Dunia huwa wako makini katika atahari hizi alizozisema ndugu yangu Juve 2002 ndio maana utekelezaji wa miradi hiyo huchukua muda mrefu.

Kama mtakumbuka vyema Waziri aliyemtangulia Mhe Magufuli hapo Wizara ya Ujenzi Ndg Shukuru Kawambwa alikuwa akifanya kazi zake kwa mujibu wa Sheria na Sera za Benki ya Dunia ili kuhakikisha kuwa hakuna mathara yoyote yatakayowapata wananchi kutokan na utekelezaji wa mradi huu. Kwa maan anyingine Benki ya Duni ipo tayarai kutoa fedha zaidi ili kupunguza athari zote zitazoainishwa na watu wanoazunguka mradi husika.

Mwaka 2010 Mhe Magufuli aliporejeshwa hapo wizarani akaamua ukinhgilia mchakato huo kwa kuminya haki za watu na kumdhiaki Waziri aliyemtanguia kuwa alikuwa akichelewesha mambo akamuingiza mkandarasi site pasipo fidia kulipwa hata kwa mashirika kama Tanesco na DAWASA ili waondoe miuno mbinu ya umeme na maji. Kama wengi wetu mtakumbuka mgogoro ulioibuka katika Mhe Magufuli na Tanesci Mhe Magufuli akilazimisha Tanesaco waondoe nguzo na Tanesaco wakidai hawatafanya hivyo bila ya kulipwa fidia.

Hali hiyo ililazimu Benki ya Dunia kutoa fedha zingine zaidi kulipa fidia za Tanesco na DAWASA ndio kazi ya kuondoa miundo mbinu yao ikaanza. Kutokana na Mkandarasi kuingizwa site kwa ubabe kabla ya maandalizi yote kukamilika kwa mujibu wa sera za mtoa fedha Benki ya Dunia ndio maaana Mkandarasi huyu STRABAG anakosa nafasi ya kutengeneza njia mbadala "Diversion" na hivyo barabara hi kulazimika kuwa na foleni kali kwa watumiaji.

Kimsingi ubabe wa Mhe John Magufuli ni janaga kwa taifa badala ya kuwa neema,
 

Ndugu yangu SIMIYU YETU uzi wangu haukulenga kulinganisha wanasiasa bali kuelezea machungu yanayotukabili kwa kuvunjiwa hali zetu za msingi kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi. Na ndio maana kwa muda wote huu toka mwaka 200 alipoanza kusigina haki zetu tumekuwa kimya tukifuatilia katika vyombo vya kutafsiri sheria hadi vilipotoa maamuzi ndio nimeleta kwenu kuwatahadharisha kuwa si kila linalotoka kinywani mwa Mhe Magufuli ni sahihi japokuwa kauli hizo zinzkuwa na madhara makubwa ya kijamii na kiuchumi kwa waathrika
 
Ndugu yangu tena SIMIYU YETU tafadhali soma majibu yangu kwa JUVE 2002 ili ujue Mhe Magufuli anavyohusika kumuingiza site Makndarasi kabala ya kukamilisha taratibu za Benki ya Dunia za upunguzaji wa atahari kwa walengwa na wote wanaozunguka mradi huo. Kwa taarifa yako foleni ndefu zilizopo katika barabara hiyo, watu kukosa maingilio katika biashara zao, maji umeme n.k vyote vilipaswa kujadiliwa kwa uwazi katiak ya Wizara yake na wadau ili kuiwezesha Benki ya Dunia kutoa fedha za kutosha kwa Mkandarasi. kwa ubabae wake akamuingiza site Mandarasi kwa fedha kiduchu na ndio matokeo yake.

Kwa hakika nathubutu kusema bado ipo haja ya watu kufanya utafiti ni wapi Mhe huyu anapolia kubabaini ni lazima ananufiaka kutokana na wananchi kukoseshwa haki zao kwa makusudi. Iweje mtu afurahie watu kuka katika foleni kwa masaa kibao eti kwa sababu Waziri alimaua kuingialia mchakato wa wataalamu na kukataa Tanesco na DAWASa wasilipwe fidia ya kuondoa miundop mbinu yao na kusababisha Mknadarsi akose sehemu ya kutengenza njai mbadala "Diversions"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…