Mahakama yamuumbua waziri Magufuli na sheria zake za uongo


Nakushukuru sana BONA kwa kuukubali ukweli. Hata sisi waathirika imetuchukua miaka zaidi ya 10 kutafiti sheria ili kubaini kuwa Mhe Magufuli anatuonea na kuuzungunza ukweli huo katika vyombo vya sheria na kuviwezesha kutoa maamuzi hayo. Kichekesho kilikuwa mahakamani ambapo wawakilishi wa wizara na TANROAD walishindwa kuifafanulia mahakama wapi Morogoro Road ilikuwa ikipita katika miaka hiyo ya 1932 hadi 67.

Kuhusu Mhe Magufuli kupatiwa ushauri anapatiwa sana na wasaidiz wake na viongozi wake wa juu lakini matokeo yake anaonyesha dharau kutokana na kujiamini kuwa anapendwa na wnaanchi. Utakumbuka alivytaka kubomoa ghrofa la Tanesco je Waziri Mkuu na Raisi Jk wangemwacha aendelee na ubomoaji huo na leo hii Mahakama inatamka sheria anayoitumia ni feki ingekuwaje?
 

Kwa taarifa yako Mhe Magufuli ndio amesababisha matatizo yote yaliyopo katika mradi wa STRABAG kwa kutudanganya kuwa aliyemtangulia Mhe Shukuru Kawambwa ni dhaifu kwa kutakua kufuata taratibu zote za Benki ya Dunia ambazo zingewezesha fedha za kutosha kutolewa kwa STRABAG na wote wanaostahili fidia kama TANESCO, DAWASA n.k ili waondoshe miundo mbinu yao. Sasa leo hawezi kumkemea STRABAG kwa foleni iliyopo kwa sababu alimuingia site Mkandarasi wakati kukiwa hakuna nafasi ya kutengeneza Diversions kwa sababu Tanesco hajatoa nguzo za umeme na DAWASA hajatoa bomba za maji kwa sabbu hawajalipwa fidia. SOMA Ext Opmanual - OP 4.12 - Involuntary Resettlement ujue ni namna gani ubabe wa Mhe Magufuli umetusababishia matatizo watumiaji na wote wanaozunguka mradi huo
 

mkuu WATANABE umenichosha kabisa.Yaani taabu zote hizi wanazopata wapiga kura wa John Mnyika hawana maji,umeme kila siku kukatika,foleni kibao,nyumba kuvunjwa ni kwa sababu tu watu wanapiga hela ya WB?haya akina Mwita Maranya kamwambieni Mnyika hii,dah,maskini Tanzania,inauma sana!
 
Last edited by a moderator:

Juve 2002 hebu soma hiyo link ya WB uone jinsi ubabe wa Mhe Magufuli ulitusababishai matatizo kibao kwa sababu ya kutotaka kufuata taratibu zote za WB
 

kwa dar cjui kama inawezekana
 

Maneno mazito sana! Big up mkuu!
 

JF ni shule,asante mkuu wangu kwa elimu hii umetoa ktk post hii.
 

yaani,,,,,hapa pana raha yake,cjui anasimamia sheria gani??
 
...nikipitia Land Act 1999, section 4(1) "All land in Tanzania shall continue to be public land and remain vested in the President as trustee for and on behalf of all citizens of Tanzania".
...endelea 4(2) kuhusu president's delegation wanavyo exercise functions....
 

asiyekuelewa ana agenda yake tu moyoni,mtu kama Simiyu Yetu hatakuelewa daima,
ubongowe umebungua
 
Last edited by a moderator:

yaani suala la kubomolewa nyumba linaumiza sana
 

UTC ni kweli kuwa ardhi Tanzania "trustee" wake ni Rais kwa mujibu wa Katina na sheria lakini there is user to the land ndio tunachokiongelea hapa. Kama ingekuwa si hivyo Serikali ingetaka ardhi yoyote kwa miradi ya maendeleo ingekuwa hailipi fidia. hata katika sauala hili la hifadhi ya barabara Mahakama Kuu imetamka ile ardhi Mhe Magufuli anayoiita ni hifadhi ya barabara tayari ina watumiaji wanaotambulika kisheria toka 1999, hivyo hakihitaji afuate utaratibu aliolekezwa katika hukumu husika kubadili ardhi ya Kijiji kuwa resersve land.
 
...wenye haki ya kuwa compensated wamekuwa wanapata haki yao...mjadala mzuri kama obsession na Magufuli itawekwa kando!
 
bila shaka na we pia utakuwa mmojawapo wa waathirika wa maamuzi hayo ya magufuli maana ulivyotiririka.
 
Magufuli position yake in CCM ni Robot,linapelekwa upande anaotaka controller

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Ulifikiri nini kabla ya kuandika hapa!? ...ilikuwa mwaka 2013 aisee.
 
Reactions: SDG
Si nimesikia watu wamebomolewa mita 120 sasa hivi huko kibaha? Na kuna tamko inatakiwa iwe hivyo tokea kimara??? Mwafaaaaa
 
Si nimesikia watu wamebomolewa mita 120 sasa hivi huko kibaha? Na kuna tamko inatakiwa iwe hivyo tokea kimara??? Mwafaaaaa
Kibaha wamebomoa mita 60 kama awamu ya kwanza japo mawe ya barabara yako mita 120! Wakirudi tena awamu ya pili bar maarufu ya Maili moja ijulikanayo kama container kwishney! Njuweni hotel pia itakumbwa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…