digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 8,926
- 17,880
Mkuu tuwe wakweli unafikiri mtuhumiwa yeyote kuruka dhamana ni sawa?Huyu hakimu ajue kuna siku tutakuwa na utawala tofauti.
Anataka awekwe ndani ionekane anaonewa lakini ajue hapa anavunja sheria na kule majukwaani anasema akiwa raisi anataka viongozi wafuate sheria.Huyu lissu naona mahakama ka inambembeleza vile,ilipaswa hata muda wa kutafuta wadhamini asingepata
Lissu amejawa kibri na majigambo ya kishamba sana
Hivi hii mahakama Haina nidhamu, yaani raisi mtarajiwa anaitawa kwenye kesi za kipuuziMahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemwamuru kufika mahakamani mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wenzake watatu, wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi, Septemba 14, mwaka huu, baada ya jana kushindwa kufika kusikiliza kesi yake.
Amri hiyo ilitolewa jana na mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kesi hiyo ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa.
Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai shauri lilipangwa kwa kutajwa na kwamba mshtakiwa Lissu, hakufika kusikiliza kesi yake.
Mdhamini wa Lissu, Robert Katula, alidai mshtakiwa aliwasiliana naye juzi asubuhi na kumueleza kwamba yuko mkoani anatafuta wadhamini kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu.
Hakimu Simba, alimtaka mdhamini huyo kuhakikisha mshtakiwa anafika mahakamani na sio kutoa sababu ambazo sio za kisheria.
"Mdhamini hizo sababu hazikubaliki kisheria tusiikosee sheria, sisi ni watekelezaji wa sheria ambapo tunatoa amri. Ukisema unaiachia mahakama tunaweza kusema ulipe dhamana na ukishindwa unakwenda jela hatutaki kufika huko, wewe hakikisha unamleta mshtakiwa tarehe ijayo," alisema.
Hata hivyo, wadhamini wa Lissu waliomba mahakama kujitoa katika udhamini kwasababu wanayemdhamini hana ushirikiano mzuri na wadhamini wake na mahakama iliwaeleza kuwa kisheria mdhamini akitaka kujitoa lazima kwanza anamleta mshtakiwa halafu ndiyo aweze kujitoa.
Kwa upande wa mshtakiwa wa tatu ambaye hakufika mahakamani Mehbooh, ilidaiwa na mdhamini wake kuwa ni mgonjwa na kuwasilisha fomu mahakamani hapo.
Hakimu Simba baada ya kusema hayo, alimtaka mdhamini wa Lissu ahakikishe mshtakiwa huyo anafika mahakamani hapo tarehe ijayo na sio vinginevyo.
Mbali na Lissu washtakiwa wengine ni, Wahariri Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.
Katika kesi ya msingi kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.
Ilidaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’
Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.
Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13 ,2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, alichapisha gazeti la Mawio lililokuwa na taarifa za uchochezi.
Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.
Hivi hii mahakama Haina nidhamu, yaani raisi mtarajiwa anaitawa kwenye kesi za kipuuzi
Unaonaje Beberu Mchina navyofanya Zimbabwe sasa hivi? Kila wakitaka fedha anaambiwa bong'oa, almasi zote, dhahabu zote zipo chini ya WachinaSawa tu lakini hatuwezi kuuza nchi kwa mabeberu
Jana nilisema Lissu anadhaurau " machineries" na pia anatudharau sisi watanzania. Sasa naona tayari,Lissu kashawaambukiza wafuasi wake kuanza kudharau machineries zetu ikiwemo Mahakama.Huyu hakimu ajue kuna siku tutakuwa na utawala tofauti.
Hivi wew matanga unajua ulichokiandika kweli, Slowslow kweli amekosa watu wa kuwalipa hizo buku 7 mpaka analeta watu kama nyie hata kujenga hoja hujui.Lissu kumbe ana kesi. Hawezi kuwa mgombea basi. Katiba hairuhusu
TrueHe is under unbearable pressure.
Hapana itakuwa vigumu, Yule atakuwa keshawatega wakimkamata na kumuweka ndani itaonekana kuwa alichohofia akiwa ughaibuni nikweli na hivyo kuzidi kuiaminisha dunia kuwa Kuna ukiukwaji wa Amani.Asipofika mahakamani hiyo tarehe anaweza kukamatwa kwa nguvu, kutupwa ndani na kunyimwa dhamana kwa madai kwamba ana historia ya kutoheshimu masharti ya dhamana. Watatumia sheria zilizopo ikibidi kuzipindisha kidogo tu ili wampe discipline.
Yajayo yanafikirisha
Huyu hakimu ajue kuna siku tutakuwa na utawala tofauti.
Wazamini?Mahakama ndio tuseme hawaoni kuwa anatafuta wadhamini kitendo ambacho kina time limit? Mbona hizo kesi zilizokuwepo hawazisikilizi wanawapiga watuhumiwa tarehe tu na kuwarejesha Segerea.
Upinzani ukichukuwa nchi mwaka wowote, hakuna kuwasamehe wale wote waliotumia madaraka yao vibaya. Wanafanya hivyo kwa utashi wao binafsi na kinyume cha kiapo cha maadili. Piga chini mahakimu na majaji wote watakaonekana wamekiuka kufata sheria ya maadili ya umma.
kWA KILA kinachotaka kufanyika na CCM na hawa watawala Tanzania kuna dalili ya Zimbabwe ijayo, na wanajua kabisa, wanajidanganya sana. Zimbabwe ilkuwa strong, ila hii Tanzania iwekewe hivyo vikwazo mnawezi kurudi ule wakati kupanga foleni kunua sukari na unga wenye muhogo. POLENI SANA