Mahakama yamwamuru Lissu kufika mahakamani

Mahakama yamwamuru Lissu kufika mahakamani

Magufuli kama Magufuli hawezi siasa za ushindani, na kwa muundo wa katiba yetu rais ndio anaagiza mahakama ifanye vipi kazi. Kwa vyovyote vile Magufuli hawezi kukubali ushindani toka kwa Lisu, wakati ana uwezo kabisa wa kuitumia mahakama kumzuia mshindani wake. Kwa sasa hivi hiyo mahakama iko kwenye mbinyo mkubwa ili itumike kumdhibiti Lisu. Na kwa uhakika hata hukumu imeshapangwa iwe vipi.
Magufuli anaingiaje hapo ?

pambaneni hali zenu na mkae mkijua sikio halizidi kichwa ...
 
Magufuli anaingiaje hapo ?

pambaneni hali zenu na mkae mkijua sikio halizidi kichwa ...

Iko wazi hiyo boss. Kwa mwenendo wa hizi mahakama zetu, hata wakitoa hukumu dhidi ya Lisu bado itaonekana ni kwa msukumo wa mtu, kwani mahakama imekuwa ikitumika kufanya mambo ya kutia shaka.
 
Tatizo jingine la upinzani ni kudhani au kufikiri kuwa Tundu Lissu ni mwanasheria pekee hapa Tanzania.

Sasa wanasahau kuwa pia anae mwanasheria wake na pia wapo wanasheria wengine kama yeye.
Sasa kama kuna magwiji wa sheria, risasi 36 za nini ?

Linapokuja suala la UTU, PESA na MADARAKA hakuna cha mchungaji wala sheikh.

Yawezekana mungu wao ni ni we madaraka na pesa
 
Mahakama ndio tuseme hawaoni kuwa anatafuta wadhamini kitendo ambacho kina time limit? Mbona hizo kesi zilizokuwepo hawazisikilizi wanawapiga watuhumiwa tarehe tu na kuwarejesha Segerea.

Upinzani ukichukuwa nchi mwaka wowote, hakuna kuwasamehe wale wote waliotumia madaraka yao vibaya. Wanafanya hivyo kwa utashi wao binafsi na kinyume cha kiapo cha maadili. Piga chini mahakimu na majaji wote watakaonekana wamekiuka kufata sheria ya maadili ya umma.

Kama ni engine wanasema itahitajika total overhaul.

Uhuru wa mihimili na uwajibikaji kwa wananchi hakuna mbadala. Kwanini USA, Kenya, India nk waweze Ila sisi?

Ajaye kama si huyu:

IMG_20200804_210728_515.jpg

Asipewe nafasi.
 
Huyu hakimu kuna siku atajikuta hupo ktk serikali ya utawala bora na wa sheria ndipo atatamani ardhi ipasuke immeze!
 
Magufuli kama Magufuli hawezi siasa za ushindani, na kwa muundo wa katiba yetu rais ndio anaagiza mahakama ifanye vipi kazi. Kwa vyovyote vile Magufuli hawezi kukubali ushindani toka kwa Lisu, wakati ana uwezo kabisa wa kuitumia mahakama kumzuia mshindani wake. Kwa sasa hivi hiyo mahakama iko kwenye mbinyo mkubwa ili itumike kumdhibiti Lisu. Na kwa uhakika hata hukumu imeshapangwa iwe vipi.
Hawezi siasa sa ushindani lakini kashindana mpaka kawa rais sasa hao wanaoweza kushindana nadhani watakuwa marais wa dunia.
 
Nasema atakwenda Segerea kama atataka ku-jump bail. That is what I am saying or that is what I meant.
huna lolote we nani mpaka useme hivyo, tahadhali , usipende kujitwisha mzigo ambaoa huna ,maisha hayako hivyo ,jishushe na umma utakuelewa . hakuna mwenye nguvu zahidi alieumba nchi ya tz na dunia kwa ujumla , mkuu
 
Haya mambo huwa hayahitaji kukurupuka tuache mahakama zifanye kazi yao.

..Hakimu anatumika kumuwekea TL "spidi-gavana."

..ili haki itendeke ni kesi zote zilipaswa kuahirishwa mpaka baada ya uchaguzi.

..TL siyo mhalifu sugu au wa kutisha, hivyo kesi hizo zinaweza kumsubiri.

..HAKI inapaswa kutendeka, na zaidi inapaswa kuonekana inatendeka.
 
Haina shida tutamsindikiza tu Rais wetu!!
 
Back
Top Bottom