Mahakama yamwamuru Lissu kufika mahakamani

siasa ni nadharia tu kama mwanasiasa kudhani wapinzani wakichaguliwa watavunja madaraja na kuuza ndege ili kufifisha juhudi.
Ila kiukweli maccm ya hovyo sana hivi kwa kauli kama hizi kweli!!zinatia kinyaa sana kwani hiyo miundombinu ndege na madaraja alinunua kwa hela yake ya mfukoni??
 
Dereva wa Lisu yuko wapi?

Ndiyo mpiga risasi
Kama kuna raia anaweza kupiga risasi 38 mchana kweupe tena kwenye nyumba za viongozi ...zenye ulinzi mkali wa Suma JKT basi kama Taifa tuko hatarini maana IS wako karibu sana
 
Nadhani ni Maagizo kutoka Chamwino! Jamaa hana amani kabisa na Lissu anavyomshushua hadharani.
 

Pia ni mtihani mkubwa kwa mahakama kiasi kwamba wakiendekeza “maelekezo” wanaweza kutusababishia matatizo nchi yetu na vyombo vya kimataifa na nchi wahisani!

Kwa wenye vichwa vibovu hawajui TL ni gusa unate!
 
Nchi isiyofuata sheria huitwa Banana Republic. Lazima kuwe na tofauti baina ya sheria na siasa. Hiyo ni kesi ya miaka minne sasa; haikuanza jana. Angekuwa amebambikwa kesi baada ya kutangaza nia tungesema siyo vizuri, lakini hapa ni kujibu kesi ambayo imekaa mahakamani miaka minne sasa mpaka inafikia wadhamini wake wanataka kujitoa.
 
Naona kama vile kumekuwa na mabadiliko kidogo kwa mahakimu wetu, mara nyingi mtu hasipofika mahakamani kinacho fuatia ni amri ya kukamatwa hasa kwa kesi kama hizi, na ukizingatia ameweka wazi kwamba sababu ya kutokuhudhuria kwake si sababu ya kisheria. Lakini hapa hakimu amemtaka mshtakiwa ahudhurie mahakamani septemba 14. Muda ambao itakuwa amesha rudisha fomu.
Hii ina maanisha kwamba hakimu ameamua kumpa nafasi Lissu ili akamilishe utaratibu wakutafuta wadhamini nakurudisha fomu kwa wakati? Ama hakimu amesoma alama za nyakati na kugundua kwamba uchaguzi wa mwaka hautabiriki chochote kinaweza kutokea na pengine Lissu anaweza kuwa bosi wake?
 

Dhamira ya kesi iko wazi kuwa ni siasa za hujuma.
 
Dhamira ya kesi iko wazi kuwa ni siasa za hujuma.
Sijui facts za kesi na utetezi wake ila ninajua kuwa ni kesi ambayo iko mahakamani kwa miaka minne sasa; kwa hiyo haikuanza eti kwa vile Lissu ametia nia, bali alitia nia wakati akiwa na kesi hiyo. Kutia nia hakuna maana ya sheria kutokufanya kazi zake.
 

Sasa kumbe unaongelea jambo usilolijua.
 

..hapa waTz wapinzani wanabambikiwa makesi kiuonevu.

..itafika mahali tutakuwa miongoni mwa nchi zinazoitwa Banana Republic.
 
Sasa kumbe unaongelea jambo usilolijua.
Kwani wewe unajua facts za kesi hiyo kabla hujasikia ushahidi wa pande zote mbili? Hii ndiyo tabia ya kukurupuka na kutoa baseless conclusions. Lissu hajatoa ushahdi wake amekuwa anakwepa mahakamani, kwanza kwa kutokana na ukweli kuwa alikuwa anaumwa, hilo hawezi kulaumiwa, lakini sasa baada ya kupona ameendelea kuwa anakwepa kwenda mahakamani. Mtu mwenye busara hawezi kutoa conclusion bila kuwa na facts zote. Wewe amini utakacho, mimi nitasubiri taarifa za pande zote mbili.
 
..hapa waTz wapinzani wanabambikiwa makesi kiuonevu.

..itafika mahali tutakuwa miongoni mwa nchi zinazoitwa Banana Republic.
Ukiachia mahakama za msingi ambazo ndizo zenye matatizo sana, kuanzia mahakama za hakimu Mikazi hadi mahakama za rufani ziko vizuri sana kuliko unavyodhani. Mara nyingi sana zimeshaamua dhid ya serikali
 
Ukiachia mahakama za msingi ambazo ndizo zenye matatizo sana, kuanzia mahakama za hakimu Mikazi hadi mahakama za rufani ziko vizuri sana kuliko unavyodhani. Mara nyingi sana zimeshaamua dhid ya serikali

..mahakama ktk ngazi zote imetumika kuumiza wapinzani, hilo halina ubishi.

..jeshi la polisi limetumika vibaya kuumiza wapinzani, huku ccm wakifanya wapendavyo.
 
Fc mp

Sent from my SM-A605FN using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…