Mahakama yatoa amri Paul Makonda atangazwe gazetini na Kolomije kupata taarifa za kesi
Yule hajafutwa ajira (kwa wanaoelewa maana ya kufutwa ajira wamenielewa).

Hivyo mwajiri wake ana taarifa zake zote.

Kwanini iwe vigumu kujulikana alipo?

Hapa kuna uhuni unaendelea
Mkuu wa mkoa ni cheo cha kisiasa akichokipata akitokea mtaani so amefutwa ajira ndugu yangu
 
JPM kawazidi sana. Kafa Lakini mnateseka sana kama ma x. JPM alikuwa Rais sio mchungaji au yesu au mtume. Kama kumbukumbu yangu iko Sawa. Makonda aliibuliwa bunge la Katiba. ( Sijui JPM alihusika) Then Kikwete akamteua kuwa mkuu wa Wilaya. Watu walimsifia kama mkuu wa Wilaya kijana na mchapa kazi. Alikutana na makundi ya watu nk. JPM aliwateua wakuu wa Wilaya Vijana sio kwa kuwajua personally bali kwa channel za utendaji nk. Iwe kwa kupenyezewa au Basi kuwa kwenye mzunguko. Katika kugombea Urais alimteua Pia mama yetu mgombea mwenza. Sasa Rais wetu. Tabia ya mtu Ni Kama ngozi tu. Wewe hatukujui ndo mana una uwezo wa kutangaza ya wengine. Katika miaka 5 na miezi yake ya JPM Kuna watu wema wengi na wazalendo aliowateua kupitia machinery zake. Wema na uzalendo wao hauwezi kutoka kwa JPM. Ni maisha na malezi yao.

Tatizo kubwa la watu kama wewe Ni ugonjwa. Ukiona mtu ambaye hata humjui. Hujui Undani Wake na tena Sasa Ni marehemu anakusumbua akili na moyoni ujue unapaswa kuwahi kulazwa haraka. Wanaojinyonga wanaanza kama wewe. As kwa makonda kama binadamu Ana yake Wacha mahakama itaamua.

Katibiwe mkuu.
Unajua hutofautiani Akili na Afande Swilla?
Nionyeshe neno JPM kwenye post yangu kwanza.
 
Labda wenzake wamemaliza Ili kulinda siri, huyu akikamatwa tutajua waliopiga Lisu risasi. Kama mbwa kala mbwa case closed
 
Tatizo hujui, kuna utaratibu wa mtu kumpelekea wito wa Mahakama, moja wapo ni kumkabidhi mkononi mhusika kama hapatikani unapeleka kwa mwajiri ama nyumbani kwake na hapo nyumbani kama hamna wa kupokea unabandika kwenye mlango wake.

Njia zote zikishindikana, sheria inasema inabidi litolewe tangazo la huo wito kwenye magazeti angalau mawili hadi matatu yanayo sambazwa nchi nzima, so hapo hamna cha ajabu.
Na hiyo ya kutangaza ikishindikana ina kuaje?
 
Hujafa kweli hujaumbika..toto la baba leo lipo hatua hii...

Mzee wa listi ya wauza madawa ya kulevya anaposakwa na mahakama
 
Wanajua alipo mbona,

Sababu za kutoonekama ni aibu wale alowazodoa wako juu yake kwa sasa anaona shida.

Kumbuka alivyouiliwa kwemda jukwaa la VIP kwenye kampeni za jiwe.
 
Notice sio swala la kuku na yai; kipi kimetangulia.

Unasajili kesi kwanza, mahakama inaamua kama kuna kesi ya kujibu na kutoa notice.

Wakili awezi kujitapa tu tunamtaka mtu aje mahakamani kusikiliza upumbavu wao. For their own amusement ya kuona Makonda kapigwa picha akiingia mahakamani na kuchapisha kwenye magazeti yao au kurusha kwenye social media.

Ni sawa jirani ampige mkewe, aliepigwa agome kufungua mashtaka. Nyumba ya pili ivalie njuga kumshitaki mpigaji una uhusiano gani na tukio? Hana.

Mtu anaeweza shitaki kwa lazima ni jamuhuri, umepeleka umbea wako kwao. Wamemwita victim ameshauri waachane na case na wao wametii.

We jirani bado kihehere unashtaki kwa lazima, unaunganisha na ofisi ya DPP kwa kutoshitaki.

Hi case ya Makonda inatengeneza bad precedent mahakamani; kwa kuendekeza siasa za kishamba na ujinga ujinga.

Kama mimi ndio Makonda siendi, huyo Kubenea he might as well include Clouds Media kwa kutoshitaki.

Clearly motive ya case ni personal vendetta. Na hii case ikisikilizwa inafungua Pandora Box ya NGO kufungua mashtaka kwa niaba ya victim mbali mbali kama jamuhuri aitofanya na ndio mwanzo wa kusikilizwa case za ovyo ovyo kama hii ya Makonda.

It is a for a reason case civil dispute zinataka kuona relation la mshitaki na mshitakiwa vinginevyo kila mtu akikwera na tukio atafungua case.
 
Jamaa ni nouma anadharau hadi mahakama.
 
Wako busy na tamthiliya ya Mbowe kua ndio gaidi ila sio huyo mwana CCM alievamia media na mabenduki!!
 
Mahakama ina taratibu zake, usiilazimishe kufanya isivyotakiwa. Wakati wakutumia nguvu ukifika utamuona lupango km Sabaya.
 
Mahakama ya Kinondoni leo Jumanne imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili apate taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea. Kesi itatajwa 2 Machi 2022.

Pia soma > Paul Makonda ashindwa kufika Mahakamani katika kesi inayomkabili. Kesi yaahirishwa hadi 08 Feb 2022

Shauri hilo limetajwa kufuatia Mahakama hiyo kushindwa kusikiliza hapo awali baada ya shughuli kuingiliana.

----

Akizungumza mahakamani hapo Leo Wakili wa upande wa waleta maombi Nyaronyo Kicheere, ameeleza kwamba wameshindwa kumpata mjibu maombi namba 3 ambaye ni Paul Christian Makonda kwa kuwa Masaki alikokuwa anakaa amekwishahama na namba yake ya simu haipatikani na hivyo kuiomba Mahakama hiyo iwapatie hati ya kumsaka maeneo mbalimbali.

Aidha wameomba kupewa hati za wito ambazo zitapelekwa alipokuwa akifanyia kazi kwa mara ya mwisho, kwenye nyumba aliyokuwa anaishi kwa mara ya mwisho, maeneo anayotembelea mara kwa mara na nyingine iwekwe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, nyingine ipelekwe bandarini, Kolomije, Misungwi mkoani Mwanza na ya mwisho ipelekwe kwenye gazeti la Kiswahili na la kingereza.

Wakili ameongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka mjibu maombi hayo ambaye ni Paul Makonda apate taarifa juu ya uwepo wa kesi hiyo mahakamani.

Kwa upande wake Hakimu wa mahakama hiyo Aron Ryamuya, ameeleza kuwa hoja ya kwenda kubandika hati hizo katika viwanja vya ndege na bandarini ni kinyume cha sheria na ni uchafuzi wa mazingira na badala yake akakubali matangazo hayo yapelekwe kwenye nyumba yake ya Masaki aliyokuwa akiishi, kwenye gazeti na kijijini kwao Koromije pekee.

Kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2022, imeahirishwa hadi Jumatatu ya Machi 2, 2022.

Chanzo: EATV

Kweli kuna watu wana muda wa kuchezea. Private prosecution sio kazi ya lelemama. Private prosecutors don’t have the privileges and powers that public prosecutors enjoy!
 
Nahis kunakitu hakipo sawa, Ni ama walifungua kesi hawana mandatory yakufungua, au utaratibu wa mashitaka yake hajafuata utaraibu, halafu najiuliza Kwan nn waende mahakama ya kinondoni?? Y kndondn?? Mahakama ya chin?? Kwa link ya pm kunajambo haliko sawa,

Halafu hii nchi inautaratibu wa kuwa na wa mtu binafsi kufungua mashitaka kijinai?? Kwa nn naona maajabu?? Yaan mfunguaji wa kesi Hana connection yoyote hata ya mbali kwa nn afungue kesi, yaan mm tu nisiejua Sana sheria naona kunakosa ya kesi wao hawaoni??

Nadhani kubenea kunamahali anapata ufadhiri, au anatumika?? Maana angalia mashitaka yake et matumizi mabaya ya madaraka, duh[emoji1][emoji1] au kuvamia radio,ebooo,[emoji9][emoji15] kubenea unahasira zako binafs na hyo mtu??

Paul Wala Hana haja ya kumtafuta hvyo, kunauwezekano wanaemtafuta Ni mwingine na aliepo Ni mwingine
 
Back
Top Bottom