chikambabatu
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 1,339
- 1,318
Vipi kwenye account zake mtandao, mmewahi kumtumia wito?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu wa mkoa ni cheo cha kisiasa akichokipata akitokea mtaani so amefutwa ajira ndugu yanguYule hajafutwa ajira (kwa wanaoelewa maana ya kufutwa ajira wamenielewa).
Hivyo mwajiri wake ana taarifa zake zote.
Kwanini iwe vigumu kujulikana alipo?
Hapa kuna uhuni unaendelea
Unajua hutofautiani Akili na Afande Swilla?JPM kawazidi sana. Kafa Lakini mnateseka sana kama ma x. JPM alikuwa Rais sio mchungaji au yesu au mtume. Kama kumbukumbu yangu iko Sawa. Makonda aliibuliwa bunge la Katiba. ( Sijui JPM alihusika) Then Kikwete akamteua kuwa mkuu wa Wilaya. Watu walimsifia kama mkuu wa Wilaya kijana na mchapa kazi. Alikutana na makundi ya watu nk. JPM aliwateua wakuu wa Wilaya Vijana sio kwa kuwajua personally bali kwa channel za utendaji nk. Iwe kwa kupenyezewa au Basi kuwa kwenye mzunguko. Katika kugombea Urais alimteua Pia mama yetu mgombea mwenza. Sasa Rais wetu. Tabia ya mtu Ni Kama ngozi tu. Wewe hatukujui ndo mana una uwezo wa kutangaza ya wengine. Katika miaka 5 na miezi yake ya JPM Kuna watu wema wengi na wazalendo aliowateua kupitia machinery zake. Wema na uzalendo wao hauwezi kutoka kwa JPM. Ni maisha na malezi yao.
Tatizo kubwa la watu kama wewe Ni ugonjwa. Ukiona mtu ambaye hata humjui. Hujui Undani Wake na tena Sasa Ni marehemu anakusumbua akili na moyoni ujue unapaswa kuwahi kulazwa haraka. Wanaojinyonga wanaanza kama wewe. As kwa makonda kama binadamu Ana yake Wacha mahakama itaamua.
Katibiwe mkuu.
Mpelekee witoYupo Uganda
Na hiyo ya kutangaza ikishindikana ina kuaje?Tatizo hujui, kuna utaratibu wa mtu kumpelekea wito wa Mahakama, moja wapo ni kumkabidhi mkononi mhusika kama hapatikani unapeleka kwa mwajiri ama nyumbani kwake na hapo nyumbani kama hamna wa kupokea unabandika kwenye mlango wake.
Njia zote zikishindikana, sheria inasema inabidi litolewe tangazo la huo wito kwenye magazeti angalau mawili hadi matatu yanayo sambazwa nchi nzima, so hapo hamna cha ajabu.
Duh. .. aliwazidi vipi akili asee,,, siku zote nilijua ile airport itatumika kupitisha mabox ya noti siku moja[emoji23][emoji23]Ndio jumla ya zile 7 walizopigwa na PAKA
Mahakama ya Kinondoni leo Jumanne imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili apate taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea. Kesi itatajwa 2 Machi 2022.
Pia soma > Paul Makonda ashindwa kufika Mahakamani katika kesi inayomkabili. Kesi yaahirishwa hadi 08 Feb 2022
Shauri hilo limetajwa kufuatia Mahakama hiyo kushindwa kusikiliza hapo awali baada ya shughuli kuingiliana.
----
Akizungumza mahakamani hapo Leo Wakili wa upande wa waleta maombi Nyaronyo Kicheere, ameeleza kwamba wameshindwa kumpata mjibu maombi namba 3 ambaye ni Paul Christian Makonda kwa kuwa Masaki alikokuwa anakaa amekwishahama na namba yake ya simu haipatikani na hivyo kuiomba Mahakama hiyo iwapatie hati ya kumsaka maeneo mbalimbali.
Aidha wameomba kupewa hati za wito ambazo zitapelekwa alipokuwa akifanyia kazi kwa mara ya mwisho, kwenye nyumba aliyokuwa anaishi kwa mara ya mwisho, maeneo anayotembelea mara kwa mara na nyingine iwekwe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, nyingine ipelekwe bandarini, Kolomije, Misungwi mkoani Mwanza na ya mwisho ipelekwe kwenye gazeti la Kiswahili na la kingereza.
Wakili ameongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka mjibu maombi hayo ambaye ni Paul Makonda apate taarifa juu ya uwepo wa kesi hiyo mahakamani.
Kwa upande wake Hakimu wa mahakama hiyo Aron Ryamuya, ameeleza kuwa hoja ya kwenda kubandika hati hizo katika viwanja vya ndege na bandarini ni kinyume cha sheria na ni uchafuzi wa mazingira na badala yake akakubali matangazo hayo yapelekwe kwenye nyumba yake ya Masaki aliyokuwa akiishi, kwenye gazeti na kijijini kwao Koromije pekee.
Kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2022, imeahirishwa hadi Jumatatu ya Machi 2, 2022.
Chanzo: EATV