Mahakama yatoa amri Paul Makonda atangazwe gazetini na Kolomije kupata taarifa za kesi
Tatizo hujui, kuna utaratibu wa mtu kumpelekea wito wa Mahakama, moja wapo ni kumkabidhi mkononi mhusika kama hapatikani unapeleka kwa mwajiri ama nyumbani kwake na hapo nyumbani kama hamna wa kupokea unabandika kwenye mlango wake.

Njia zote zikishindikana, sheria inasema inabidi litolewe tangazo la huo wito kwenye magazeti angalau mawili hadi matatu yanayo sambazwa nchi nzima, so hapo hamna cha ajabu.
na hiyo njia ikishindikana ?
 
upuuzi mwengine huu!!!
watu wengine hawana majukumu ya kufanya, au wana muda wa kuchezea.
eti unamshitaki makonda na serikali!!
huyo mlalamikaji ndio nani? ujinga kabisa huu
 
Mahakamani hakunaga ujinga mzee

Kama ameitwa si aende tu akawaweke sawa huko wasi wasi wa nini?wakati yeye anajua ni msafi

Ova
Anashindwa kwenda sababu ya jina, mkienda KOLOMIJE mkamtafuta Paul makonda hawamjui, inabidi muuliza Daudi Bashite, na hati inasema Makonda.
 
watu tunawaza jinsi ya kuanzisha Anwani za Makaazi.....nyie mnatuletea upuuzi huuu.
 
Mahakama ya Kinondoni leo Jumanne imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili apate taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea. Kesi itatajwa 2 Machi 2022.

Pia soma > Paul Makonda ashindwa kufika Mahakamani katika kesi inayomkabili. Kesi yaahirishwa hadi 08 Feb 2022

Shauri hilo limetajwa kufuatia Mahakama hiyo kushindwa kusikiliza hapo awali baada ya shughuli kuingiliana.

----

Akizungumza mahakamani hapo Leo Wakili wa upande wa waleta maombi Nyaronyo Kicheere, ameeleza kwamba wameshindwa kumpata mjibu maombi namba 3 ambaye ni Paul Christian Makonda kwa kuwa Masaki alikokuwa anakaa amekwishahama na namba yake ya simu haipatikani na hivyo kuiomba Mahakama hiyo iwapatie hati ya kumsaka maeneo mbalimbali.

Aidha wameomba kupewa hati za wito ambazo zitapelekwa alipokuwa akifanyia kazi kwa mara ya mwisho, kwenye nyumba aliyokuwa anaishi kwa mara ya mwisho, maeneo anayotembelea mara kwa mara na nyingine iwekwe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, nyingine ipelekwe bandarini, Kolomije, Misungwi mkoani Mwanza na ya mwisho ipelekwe kwenye gazeti la Kiswahili na la kingereza.

Wakili ameongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka mjibu maombi hayo ambaye ni Paul Makonda apate taarifa juu ya uwepo wa kesi hiyo mahakamani.

Kwa upande wake Hakimu wa mahakama hiyo Aron Ryamuya, ameeleza kuwa hoja ya kwenda kubandika hati hizo katika viwanja vya ndege na bandarini ni kinyume cha sheria na ni uchafuzi wa mazingira na badala yake akakubali matangazo hayo yapelekwe kwenye nyumba yake ya Masaki aliyokuwa akiishi, kwenye gazeti na kijijini kwao Koromije pekee.

Kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2022, imeahirishwa hadi Jumatatu ya Machi 2, 2022.

Chanzo: EATV
Watangaze zawadi atafika usiku wa manane hapo mahakamani kabla ya kesi yupo jirani na hapa nilipo.
 
Huyu jamaa ni MTU wa wapi? 😁
16443273995030.jpg
 
Makonda Yuko Morogoro, Jana alikuwa anakodi jengo lililokuwa limekodiwa na crdb Bank Morogoro karibu na CINE CINEMA building, Kuna mafundi wake pale, Dodoma anafanya kazi ya dry clear, ametega suti za wanene azifue
 
Mahakama ya Kinondoni leo Jumanne imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili apate taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea. Kesi itatajwa 2 Machi 2022.

Pia soma > Paul Makonda ashindwa kufika Mahakamani katika kesi inayomkabili. Kesi yaahirishwa hadi 08 Feb 2022

Shauri hilo limetajwa kufuatia Mahakama hiyo kushindwa kusikiliza hapo awali baada ya shughuli kuingiliana.

----

Akizungumza mahakamani hapo Leo Wakili wa upande wa waleta maombi Nyaronyo Kicheere, ameeleza kwamba wameshindwa kumpata mjibu maombi namba 3 ambaye ni Paul Christian Makonda kwa kuwa Masaki alikokuwa anakaa amekwishahama na namba yake ya simu haipatikani na hivyo kuiomba Mahakama hiyo iwapatie hati ya kumsaka maeneo mbalimbali.

Aidha wameomba kupewa hati za wito ambazo zitapelekwa alipokuwa akifanyia kazi kwa mara ya mwisho, kwenye nyumba aliyokuwa anaishi kwa mara ya mwisho, maeneo anayotembelea mara kwa mara na nyingine iwekwe katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, nyingine ipelekwe bandarini, Kolomije, Misungwi mkoani Mwanza na ya mwisho ipelekwe kwenye gazeti la Kiswahili na la kingereza.

Wakili ameongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutaka mjibu maombi hayo ambaye ni Paul Makonda apate taarifa juu ya uwepo wa kesi hiyo mahakamani.

Kwa upande wake Hakimu wa mahakama hiyo Aron Ryamuya, ameeleza kuwa hoja ya kwenda kubandika hati hizo katika viwanja vya ndege na bandarini ni kinyume cha sheria na ni uchafuzi wa mazingira na badala yake akakubali matangazo hayo yapelekwe kwenye nyumba yake ya Masaki aliyokuwa akiishi, kwenye gazeti na kijijini kwao Koromije pekee.

Kesi hiyo namba 1 ya mwaka 2022, imeahirishwa hadi Jumatatu ya Machi 2, 2022.

Chanzo: EATV
Chochea kuni chochea kuni
 
Back
Top Bottom