Mahakama yatoa amri Paul Makonda atangazwe gazetini na Kolomije kupata taarifa za kesi
Mahakama ya Kinondoni leo Jumanne imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili apate taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea. Kesi itatajwa 2 Machi 2022.

Pia soma > Paul Makonda ashindwa kufika Mahakamani katika kesi inayomkabili. Kesi yaahirishwa hadi 08 Feb 2022

Shauri hilo limetajwa kufuatia Mahakama hiyo kushindwa kusikiliza hapo awali baada ya shughuli kuingiliana.

Tanapol na intelligensia yao wameshindwa kumpata bashite haya ni maaajabu kama chadema wangewaza tu watakuw na kikao cha ndani tayar tanpol wangeishitokeza kitambo kukizuia
 
kama hapatikani unapeleka kwa mwajiri ama nyumbani kwake na hapo nyumbani kama hamna wa kupokea unabandika kwenye mlango wake.
Njia zote zikishindikana, sheria inasema inabidi litolewe tangazo la huo wito kwenye magazeti angalau mawili hadi matatu yanayo sambazwa nchi nzima, so hapo hamna cha ajabu.
  1. Asante sana kwa elimu hii wengi hatukuijua
  2. Vipi kuhusu tangazo linagharamiwa na nani
  3. Na jee haiezekani kutangaza kwenye vyombo vingine kama TV. radio na mbao za matangazo au tangazo likadhaminiwa kwenye matangazo ya mechi nk... kwamfano huenda mtuhumiwa akawa hajui kusoma gazeti akisikia tangazo kwenye runinga au redio ata respond
 
Mahakama ikitaka mchakato ufanyike kwa haraka na upesi ingepanda dau kwamba kwa yeyote atayesaidia taarifa za upatikanaji wake atazawadiwa kiasi fulani cha pesa

Hizo pesa zingelipwa na mshtakiwa mwenyewe, yaani kabla kesi haijaanza kusikilizwa anatakiwa atoe hicho kibunda kwanza
 
Mahakama ya Kinondoni leo Jumanne imetoa amri ya kutangazwa gazetini, nyumba aliyoishi Masaki na au kijijini kwao Kolomije kwa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ili apate taarifa za kesi iliyofunguliwa dhidi yake na Mwandishi wa Habari, Saed Kubenea. Kesi itatajwa 2 Machi 2022.

Pia soma > Paul Makonda ashindwa kufika Mahakamani katika kesi inayomkabili. Kesi yaahirishwa hadi 08 Feb 2022

Shauri hilo limetajwa kufuatia Mahakama hiyo kushindwa kusikiliza hapo awali baada ya shughuli kuingiliana.

Mbona kama kuna jambo linachezwa hii taarifa ya mahakama kwanini hakuwataka polisi wamtafute ni apate taarifa tu kutoka gazetini kuhusu kesi iliyofunguliwa dhidi yake sasa hii haina mantiki yoyote anaweza ku-relux tu ata kama yuko huko Masaki, Imagine kama ni mtu tofuati na Makonda si Polisi wangeambiwa direct wamsake?
 
Jana mbona alikuwa morogoro na wapambe 4 hivi..hana wasiwasi
 
Sijaelewa hii kesi inayomfanya yule Mkuu wa mkoa kiboko wa wauza ngada mh Paulo Makonda aishi kidigidigi kama ni ya jinai au madai?

Ufafanuzi Tafadhali!
 
Kajificha ukweni Njiro, ila haya maisha haya.!!
 
Ukitaka kujua kwa nini magufulists hawampendi samia ni kwa mambo kama haya. Wapwani ndio wafanyaji wakubwa wa madawa ya kulevya.
Mama anaacha aliyekua mtumishi mwakilishi wa rais mkoa wa dar kunyanyasika na kubakia katika hali ya mashaka kwa kazi aliyofanya kupambana na dawa za kulevya. Ni kisasi tu wala sio lingine.
Mkuu acha porojo Wewe,inabidi ifike mahali watu wote watii Sheria ,yaani unataka mama Samia amkingie kifua Makonda kwa makosa aliyojitakia!!?

Napenda Sana utawala wa sheria,au huenda umeandika hapa hujui maana ya rule of law? Utawala wa sheria kazi yake Ni kumwajibisha kila mtu anayevunja sheria za nchi,hivyo acha sheria ushughulike na watu wote wanaohisiwa kukiuka misingi ya utawala wa sheria.

Kama wewe ndo Makonda naomba ujitokeze ukajibu tuhuma zako popote pale ulipo!![emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
 
Polisi ni mtandao mpana sana, kwanini kama makonda ni ngumu kumpata kupokea wito, watumie arrest warant polisi imsake warrant mahali popote
 
Huyu jamaa ndio nilisikia amekimbia nchi kwa kutumia boda ya kenya ama sio huyu , kweli maisha hayana fomula , nakum,buka picha zake anapigiwa saluti na kina mambo saasa huku kavaa kikaputura kifupiii, yani laana hazijawahi kuwaacha watu salama. Malipo ni hapa hapa kabla hujaingia kaburini
 
D4M.jpg
 
Back
Top Bottom