Mahakama yatupilia mbali Rufaa ya Odinga, yakubali Ruto ameshinda kihalali Urais wa Kenya, leo Jumatatu Septemba 5, 2022

Mahakama yatupilia mbali Rufaa ya Odinga, yakubali Ruto ameshinda kihalali Urais wa Kenya, leo Jumatatu Septemba 5, 2022

nipo hapa Mlimani Law nimebeba mafaili ndio tunamalizia malizia tuje kuwasomea hukumu.

tunaprint jugment muda huu maana kila mtu alilala na flash yake ili maamuzi yasivuje.
 
Hivi ili ionekane ni Demokrasia ndio Odinga anatakiwa Ashinde??

Ila Ruto akishinda sio Demokrasia??.

Hivi nyie wabongo,, Kati ya Uhurodinga na Hustler , nani alikua na nguvu kubwa ya kucheza na Uchaguzi??.

RAIS NI RUTO !!.
Demokrasia sio Odinga au Ruto kushinda, Demokrasia ni kitendo cha kumpa mlalamikaji nafasi ya wazi kwenda mahakamani kujenga facts zake na walalamikiwa kujibu facts hizo..

Hapa kwetu na hata baadhi ya majirani zetu hakuna hiyo nafasi.
 
Kwa Ubunge zipo
 
Hivi ili ionekane ni Demokrasia ndio Odinga anatakiwa Ashinde??

Ila Ruto akishinda sio Demokrasia??.

Hivi nyie wabongo,, Kati ya Uhurodinga na Hustler , nani alikua na nguvu kubwa ya kucheza na Uchaguzi??.

RAIS NI RUTO !!.
Watu wote wanajua Mganga hawezi kuwa Rais Kenya...ila wapo wanaomdanganya..

Hustler ndie the 5th...na anaapishwa tarehe13/092022
 
Hakuna Rais kwa uchaguzi wa August 9, 2022. Mtandao wa IEBC uliingiliwa na wahuni, vituo hewa vilidhihirika. Chebukati ameshindwa kutekeleza majukumu yake, achukuliwe hatua

Ngoma inaanza upya. Na Uhuru Kenyatta ataongeza muda kama Katiba itaruhusu.

Hii ni kwa maoni yangu
 
Mbona unatunanga bila ushahidi😎😎😎😎
 
Polisi waweka kizuizi kinachozuia ufikiaji wa lango la Mahakama ya Juu..
Fb33dp3WIAAc6Ym.jpeg
 
Majaji wakiwasili katika Mahakama ya Milimani kabla ya uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu kesi ya uchaguzi wa urais wa 2022.
 
Uamuzi ni saa sita mchana: Hali ilivyo katika Kaunti ya Nakuru.
 
Kiongozi wa Chama cha Roots Prof. George Wajackoyah miongoni mwa mawakili wengine akiwasili katika Mahakama ya Milimani kabla ya uamuzi wa Mahakama ya Juu kuhusu kesi ya uchaguzi wa urais wa 2022.
 
Back
Top Bottom