DOKEZO Mahakama yavunja ndoa ya Davis Mosha na mkewe aliyeishi naye miaka 28, anyimwa mali. Mosha adai kuibiwa $ milioni 1.4 na jaribio la kupewa sumu

DOKEZO Mahakama yavunja ndoa ya Davis Mosha na mkewe aliyeishi naye miaka 28, anyimwa mali. Mosha adai kuibiwa $ milioni 1.4 na jaribio la kupewa sumu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nimejifunza kuna wanawake wanapenda shida. Ukiwapa raha kupitiliza ni matatizo wanasahau walipotoka. Aisee Mosha alivumilia mengi sana. Huyu Mwanamke hajajiharibia yeye tu kajiharibia hadi kwa watoto wake. Wanasema majuto ni mjukuuu atakuja kujua alipoharibu baadae sana. Maana najua mpaka sasa anaamini akienda kudai mgawanyo wa mali ili atamkomoa mumewe. Haya mambo nimeyaona kwenye familia nyingi za wenye hela. Ushauri wangu mapenzi hayalazimishwi. Ukiona mmeshindwana bora muachane. Na pia kwa wanawake mlio katika ndoa: Ni vigumu sana kupata mwanaume anaeweza kukuhudumia na wa kuishi nae bila shida ndogo ndogo kwa karne hii. Kwa hio ukiolewa tulia na jishushe. Mwanaume anaemtesa mke wake anaejishusha ni yule ambaye mke wake amemzidi kila kitu. (mwanaume mwenye inferiority complex)
Shida ya huyo Nancy ni mrogi kwahio alimkamata kwa nguvu huyo Davis Mosha na alikuwa hafurukuti ila baada ya dawa kuisha akaanza kuharibu live 😂😂😂
 
Mheshimiwa Hakimu ameandika hivi:
" The NITTY GRITTY of the matter before me is SOMEHOW not hard to comprehensive. It all started when the petitioner and the respondent GOT ACQUAINTED TO EACH OTHER AFTER A LONG CHASE TRYING TO WIN THE OTHER'S HEART....they decided to surprised the UNIVERSE ....after comprehending that their affection did match and exceeded ONE ANOTHER TO THE HIGHEST DEGREE. The ANGEL OF BLESSING was on their side and bestowed UNTO them THEIR 3 cute children ( amewataja majina). The devil BEING DISGUISED with his CROCODILE smile couldn't let go of their marriage to DOOM by planting weeds in their BLOOM LOVE. He made the decision to hit them with a storm of life threatening ....." Hizi ni paragraph za mwanzo. Total gibberish.

Amandla...
Huyu hakimu ni ana kipaji cha poetry bila shaka 😂😂😂
 
Wanawake Jifunzeni kutafuta mali zenu wenyewe.
Wanapenda sana dezo😂 eti mwanaume sharti anihudumie...Mtu unamuoa ila kushea cost hataki kabisa yani.

Utafte mali kwa nguvu kisha mwisho aje kutaka mgawane pasu kwa pasu wakati hakuna mchango alioweka zaidi ya kutanua mapaja tu na kuongeza wategemezi.
 
Wanawake wakishakaa miaka mingi Kama hiyo kwenye ndoa,huwa hawaoni umuhimu wa mume/ndoa,ubinafsi hutawala nyoyo zao,huu ni ugonjwa mpya kwa wanawake wa tz,ndoa za watu wazima nazo Zina shida kweli siku hizi
Mwanamke ili uishi nae kwa amani kwenye ndoa unatakiwa uhakikishe yuko kwenye pressure most of the time. Ukimpa all of you kilaini tu jua tu baada ya miaka michache atakugeuza zombi wake na kukutaftia replacement mkiwa ndoani humo humo.
 
wamekutana pipa na mfuniko. mosha malaya anapenda sana wanawake. na mkewe anapenda mno uroda.

cc: Mrangi
Mwanaume ukiwa na hela wanawake wa kila aina wanajipanga kwa foleni wakijilengesha ili uwale tu wengine hata hawaitaji pesa zako ila tu wapate fleva ya kutowmbwa na Don Mapesa.

Na kama mnavyojua sisi ni marage ya Mbeya huwa hatuwazi sana mkijilengesha kama mpo njema ni uboho tu.
 
Shida ni kwamba huyu dada alikuwa Malaya kupitiliza huyu Nancy alikuwa anatembea hadi na wafanyakazi wake yani hii ni ushahidi kabisa huyu Nancy alikuwa anatembea hadi na Marafiki wa Mwanaume wake,Mwanaume Akisafiri yeye anapeleka wanaume nyumbani kwa Mume wake anaagiza hadi wadada wa kazi wapike chakula sasa Kuna mtu hapa au uchafu Jamani muacheni Davis wa watu apumzike aishi kwa amani maana Ameshateseka sana kwa huyu mwanamke mwizi kwa hiyo Mungu ameamua kumuondolea gunia la miba kichwani kwakweli na ashukuriwe Mungu kwkuwa hawakumuuua
Huyo malaya ningejua anataka kuniua mi ningemuondoa tu kidizaini akafie mbele huko kwa style ya KGB ile. Namtia pollonium tu kisha na file divorce akauguzwe na malaya wenzie ila akiwa nje ya eneo langu. Miezi 6 mingi lazma atang'ata shuka tu😂
 
Nashengena Boy alimtamani huyo dada kwasababu anang'aa wakati aliyekuwa akimfanya ang'ae ni mume.

Baada ya divorce lazima mng'ao upungue kwa mwanamke hapo ndio boy anapomuacha. wanawake huwa hawafikiri mbali!

kwahiyo sasa hivi huyo dada kwenye nyumba ya ex husband wake kashaondoka au siyo?
Wanawake wa kibongo washamba sana. Akishakuwa na source ya hela anaona ni bora atafte mpenzi wake private wa kumpelekesha ila mumewe anamuona hana maana kwake tena😂.
 
Una ushahidi gani kuwa Hizo Mali walichuma wote?
VIPI kuhusu tuhuma za kuiba Dola 1m na Sumu hapo atastahili?
Au ni dada Yako unamtetea EE? Kwa Mangi hatoboi,mamangi ni brightest sio rahisi uwaingize mjini
Una ushahidi gani alitaka kumuua ,kuiba pesa ,acheni tamaa za mali mke anabaki na haki yake kama mke.

Yaani atake kuua halafu asishtakiwe !?Mpeni haki yake anahusika kweny mali moja kwa moja.

Mosha kaweka hizo kama defensive mechanism sio kweli ni timing madai yote hayana uhalisia eti alitaka kuuliwa😅😅
 
Inawezekana kuwa uko sahihi. Lakini tatizo kubwa katika jamii yetu ni kuona mali yote inayopatikana wakati wa ndoa ni ya mwanaume na anammegea mke wake kama fadhila tu. Kinachosikitisha ni kuwa wanawake wengi wanaamini hivyo pia kwa sababu nao hawathamini mchango wao katika mafanikio ya familia. Hata pale ambapo sheria inasema kuwa ana haki ya kupata mgao katika mali za familia wengi wanaishia kusema kuwa watamuachia Mungu hasa kama aliyekuwa mume wake ni tajiri au mtu mwenye nguvu katika jamii. Hapa mnamlaumu mwanamke kuwa kuwa ana tamaa kama vile kuwa na tamaa ni dhambi. Huyo mume wake asingekuwa na tamaa angepata huo utajiri? Wanaume wangapi wamepata mafanikio kwa sababu mwanamke ana tamaa ya maendeleo ikiwa pamoja na mali? Huyu mwanamke anaitwa malaya wakati aliyekuwa mume wake sio tu ana mipango ya kando na hata mahakama imekiri kuwa amezaa na angalau mmoja wao. Unafik na double standards zenu zinaudhi kwa kweli.

Amandla...
Double standards zipi bwana wee. Mwanaume mpaka anapozaa nje ya ndoa jua mke hajielewi ameshindwa kumu handle mumewe ama ni mkorofi. Michepuko hutokea sababu ya wanawake kutowajibika ipasavyo na ndoa.
 
Hakuna mtu mwenye pesa anaweza kuvumilia shida. Kama hauna pesa hauwezi kuelewa hii kauli. Dada yangu kama unataka unyenyekewe kwenye ndoa kama malaika. Tafuta mume masikini na umhudumie kila kitu umpe mpaka hela ya bia. Na kuahidi hata ndugu zake watakutetea ukikosea. Tatizo wanawake wengi mnachukulia uzuri wenu una thamani. Thamani ya binadamu yeyote duniani ni kiasi cha disposable income anachokimkliki. Mwanamke kama hauna hela kubali kuwa mnyonge. Usishindane na mumeo kwa kumkomoa. Wewe na mumeo ni vitu viwili tofauti. Yeye ndio anakuhudumia kila kitu. Na uwezo wake wa kukuhudumia ndio unaosababisha wanawake wenzako wamsumbue. Maisha yana sheria zake. Maisha ni kuchagua nimeshaelezea hapo juu uchague kutokana na maisha unayotaka. Sikubaliani na mwanaume anaetembea na mahawara huku hatimizi majukumu yake kama mume.
Kiufupi tofauti ya maskini na mwenye uwezo ni number of choices. Tajiri anachagua ale nini kwa wakati upi ila kapuku anakula kilichopo kwa wakati uliopo. Maskini hana la kufanya zaidi ya kuvumilia.
 
Unaongea nadharia dada yangu unachokitaka hakipo hapa duniani. Na ndio maana wanawake wengi hawaolewi. Kwa sababu wanataka pesa na kunyenyekewa kwa pamoja. Hivyo vitu havipo na havitakaa viwepo. Hakuna mtu atakaekupa pesa na heshima kwa pamoja. Ukiwa na mtazamo huo lazima utakosa mume labda utafute mwanaume ambaye hana hela. Lakini mwanaume mwenye mtazamo huu atasumbuliwa kila siku na wanawake wakililia awaoe. Na mwanamke mwenye mtazamo huu akipata mwnaume mwenye hela anaolewa chap kwa haraka. Unang'ang'ania viapo vya ndoa wakati wachungaji, masheikh na mapadri wanakumbatia matajiri. Unashindana na mumeo una uwezo wa kulipa ada ? Au kuihudumia hiyo nyumba ? Jishushe tu na jifanye mjinga watoto wakishakuwa na Umri ukienda mume atajirudi angalau. Lakini hauwezi kushindana na mtu mwenye hela. Kama unataka Utu tafuta wa size yako. Kuna dada mmoja alikuwa hajatulia akaja kupata mwanaume mwenye nia ya kumuoa. Alikuwa na uwezo mkubwa kifedha akaja kuachana nae kisa alifumania sms za kimapenzi. Hiyo ilikuwa mwaka 2008, mwezi wa saba mwaka huu anatimiza 37. Hana ndoa na bado yupo kwao, yule jamaa ana mke na ameshaoa. Na huyu dada amekuwa kimada kila akihitaji hela anaenda kwa yule ex-wake kubatuliwa. Anamfanyia vituko mke wa jamaa lakini mke anamwambia tu kuwa "wewe ni hawara hauwezi kuwa mke". Dada mpaka leo anajutia maana mke ndio anaitwa Mama Tarimo yeye kabaki kuwa kihawara chenye tamaa ya hela 😂 😂 😂 😂 😂 😂 . Huyu mke wa Tarimo ndio anajua nini maana ya kuwa mke.
Mkuu unashusha nondo hadi nataka kumuita waiter akuongeze 3 kwa heshima yangu kwako.
 
Mfanyabiashara Davis Mosha ameacha na mke wake wa ndoa aliyeishi naye kwa miaka 28 amekwenda kufoji nyaraka za kampuni hukumu imetolewa mke hajapewa urithi hata pini.

Masikini ya Mungu Huyu Mkewe ndiye alikuwa muhasibu wa kampuni zote za huyu mfanyabiashara kwa miaka 20.

Majaji wetu hukumu kama hizi ni za ukandamizaji, mawakili tunaomba msaidie kama hii hukumu ni halali na mahakama zetu zinatoa haki nimeona uonevu mtupu humu Pesa imenunua haki.

Je hii ni sawa?

==========
MAAMUZI YA MAHAKAMA
  • Ndoa kati mlalamikaji na mlalamikiwa imevunjwa na talaka imetoka.
  • Hakuna mali zilizopatikana kwa pamoja kwenye ndoa.
  • Uangalizi wa mtoto Daniela Davis Mosha unakuwa chini ya mlalamikaji(Baba)
  • Mdaiwa anapewa ruhusa ya kuwa na mtoto kipindi cha likizo na siku yenye nafasi kwa mtoto
  • Mdaiwa amekatazwa kutumia jina la mlalamikaji Davis Mosha na amerejeshewa majina yake ya awali
  • Kila mmoja atabeba gharama za kesi

View attachment 2912748View attachment 2912749View attachment 2912750View attachment 2912751View attachment 2912752View attachment 2912753View attachment 2912754View attachment 2912755View attachment 2912756View attachment 2912757View attachment 2912758View attachment 2912759View attachment 2912760View attachment 2912761View attachment 2912762View attachment 2912763View attachment 2912764View attachment 2912765View attachment 2912766View attachment 2912767View attachment 2912768
Acha umbeya wewe. Ndo maana umepost kama Anonymous ili usije ukashushuliwa.

Yaani ulivyokuwa umekabwa na umbeya kooni mpaka umeshindwa kutulizana na kupangilia hizo picha kwa usahihi. Unatuchosha tu kusoma document iliyopangiliwa ndivyo sivyo... yaani unatoka ukurasa 13 unakuja ukurasa wa 11 vurugumechi tupu kisa kukabwa na umbeya.

Kwanini nakuita mbeya?

Soma hiyo huku ukurasa wa 14, aya ya mwisho na muendelezo wake kwenye ukurasa wa 15. Naiweka hapa kwa manufaa ya wote:

1708918093587.png


Kama hujui Kiingereza alichoandika Mh. Hakimu hapo ni kwamba mwanamke hakuomba mgawanyo wowote wa mali, na wala hakuleta ushahidi wowote wa kuonesha kwamba kuna mali za ndoa. Mali alizoonesha ni mali za kampuni. Kampuni sio ndoa. Mali za kampuni haziwezi kugawanywa katika shauri la talaka. Kwamba mwanamke kama anataka mgao wa mali za kampuni basi afungue shauri la madai la kawaida.

Sasa cha muhimu ni hicho cha mwanamke kutodai mgawanyo wowote wa mali, halafu wewe ambaye siye uliyepewa talaka unawashwa na mali hizo.
 
Mnaweza kuishi pamoja lakini msichume pamoja.
Wasomi wote wanajua hilo.
Watu ambao hawakufanikiwa kusoma na hawana maarifa ndio huwaza kwa namna yako

Wewe unazungumzia usomi na maarifa, je! Tukienda kidini ni sawa kunyimwa haki yake huyo mke wa marehemu! Ila kwakua wewe si Muislamu, na huujui Uisilamu na sheria zake hata majibu utakayonipa hayatakua na uhalali wowote
 
Ni Mtoto wa Mosha ndiyo, mfanyakazi alikosea meseji badala ya kumtumia Nancy kuwa Zoezi la kumuua Mtoto limekamilika anaua usiku na MTO, akawa anaomba pesa, akakosea akamtumia Mama wa Mtoto
aisee,asante kwa huu ubuyu maana story ilitembea sana ila watu walikuwa wanaficha wahusika anatajwa tuu rachel temu
 
Mnaweza kuishi pamoja lakini msichume pamoja.
Wasomi wote wanajua hilo.
Watu ambao hawakufanikiwa kusoma na hawana maarifa ndio huwaza kwa namna yako
Katika hali yoyote ile hilo suala halipo,mali ambao mke kazikuta ndio hazimuhusu ila yote yaliyotokea punde baada ya ndoa basi anahusika .

Hali inayoweza kujitokea kama mume anaendesha mali za kifamilia yaani kama biashara ya familia ya mume ,ila bado kweny kipato cha mume mke atahusika isipokuwa mali za biashara nzima

Rejea mke wa Mrema kupata mgao kidogo baada ya mumuwe kufariki wala ndoa haina muda sana.
 
Back
Top Bottom