Mahakama yazuia ombi la kampuni ya NSK kuifilisi Dangote Cement

Informative.
 
Da ngote alikuwa anakwepa kodi, na kipengere cha kuajiri watanzania kwa wingi ye akakivunja, akaajri ndugu zake wa uko Bono.

omdoke zake.. eron musk anakuja kuwekeza nchini hivi karibuni..
 
Habari nyingi humu huletwa kwa mrengo wa kupotosha zaidi kuliko kuhabarisha uhalisia wa mambo.

Sababu ikiwa wengi humu wanapenda kuzisikia hizo.

Na kambale wa Jf wanameza sana hizo ndoano.
 
Hii NSK kwa nini inakimbilia winding up
Bila shaka hao wahindi wa NSK wakishirikiana na bank ya standard chartered, wanataka mali za kampuni ya Dangote ziuzwe ili wakinunue wao. Ni moja ya strategy wanapenda kutumia ili kupunguza ushindani kwenye soko.
 
Dah,ndugu yangu anakosa ajira hivi hivi yaani,inauma sana,mazingira ya uwekezaji nchini kwetu yana shida mahali.

Hapa kwetu mji kasoro meli,viwanda vikubwa kama viwili vimefungwa,ni mazava na cha tumbaku,vilikuwa vimeajiri watu wengi sana hasa kinamama,haya cha mkulazi cha miwa nacho tantalila tu hadi leo hakijaanza kufanya kazi,ndio kwanza miwa yao wanawauzia kiwanda kingine cha sukari cha mtibwa,hadi aibu yaani lengo lilikuwa wazalisje sukari,lakini miwa yao haizalishi sukari inabidi wamuuzie mtibwa angalau wasipate hasara kwenye uwekezaji walioufanya.
 
Wenye ushabiki waendelee na ushabiki wao, lakini hiyo haitabadilisha ukweli kuwa TANZANIA INA MAZINGIRA MABAYA SANA YA UWEKEZAJI.

Fikiria mwekazaji mwenye vitega uchumi kadhaa nchi mbalimbali, maisha yake yote hajawahi kulala mahabusu ya Polisi, hata nchini mwake, Tanzania DC ambaye hajawahi kuwekeza hata mradi wa genge la nyanya, kwa ujinga tu, hata bila sababu za msingi, ana uwezo wa kutoa amri, kamata huyo mwekzaji weka ndani, na ikawa.

Pale Morogoro, RCO aliwahi kumweka ndani mkurugenzi wa kiwanda cha tumbaku. Mwekezaji akaamua kufunga kiwanda, baadaye ndiyo serikali ikazinduka na kuanza kumbembeleza sana asifunge kiwanda.

Kuna ujinga mwingi sana nchi hii. Mathalani, sheria inatamka wazi, mamlaka iliyokupa leseni ndiyo pekee yenye uwezo wa kusimamisha shughuli zako, lakini usishangae shughuli zako zinaweza kusimamishwa na mtendaji wa kata, DC au RC. Ni utawala holela, na Rais ndiye aliyesababisha. Maana akiwa nao anaongea vitu vya ajabu sana, vitu vilivyo nje ya sheria, eti hao wana mamlaka yasiyo na mipaka kwa sababu wanamwakilisha yeye!!

Tunawahitaji sana wawekezaji. Makampuni ni taasisi. Hata kukiwa na makosa, huwezi kumparamia tu mkurugenzi au mwekezaji, na kuamru awekwe ndani au asimamishe uzalishaji. Kuna taratibu, na kuna wanasheria wanaowakilisha makampuni, wewe unachomoka na kumweka ndani mkurugenzi. Sipendi kuyatumia maneno mabaya lakini kwa kweli watendaji wengi wa Serikali awamu hii ni washamba na malimbukeni wa madaraka. Wanahisi kwa kupewa cheo fulani basi wao ni binadamu zaidi, na wengine wote ni nusu binadamu walio chini yao.

Kama hakuna watakaopata ujasiri na kumwambia Rais kuwa maeneo haya unafanya vema lakini maeneo haya unafanya vibaya, rekebisha haraka sana, tutajuta sote. Na bahati mbaya watu wanaomzunguka Rais na ambao yeye anawaaminin sana ni watu arrogant lakini ambao practically hawajui chochote kuhusu uchumi, uwekezaji na biashara. Mtu kama Kabudi sidhani kama ana msaada wowote kiuchumi kwa Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Da ngote alikuwa anakwepa kodi, na kipengere cha kuajiri watanzania kwa wingi ye akakivunja, akaajri ndugu zake wa uko Bono.

omdoke zake.. eron musk anakuja kuwekeza nchini hivi karibuni..
Eron musk ndio mzee baba, au anapatikana lumumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…