Mahakama yazuia ombi la kampuni ya NSK kuifilisi Dangote Cement

Mahakama yazuia ombi la kampuni ya NSK kuifilisi Dangote Cement

Conspiracy in business esp. managing business in emerging markets, there are different ways of changing markets, production points, what if Dangote is going somewhere else to invest,? Business chaos/conflicts can also be created for a good, think deep. you https://jamii.app/JFUserGuide me, then I https://jamii.app/JFUserGuide you harder at last. Awamu ya 5 be careful oooh ogah ogah. Be careful with trans-national ana mult- national business companies
 
Bila shaka hao wahindi wa NSK wakishirikiana na bank ya standard chartered, wanataka mali za kampuni ya Dangote ziuzwe ili wakinunue wao. Ni moja ya strategy wanapenda kutumia ili kupunguza ushindani kwenye soko.
Kwani Dangote angelina kwa wakati kama alivyo kubaliana kiwanda kingefungwaje?

Hapo msiwachafue watu kea shida za Dangote.
 
Dah,ndugu yangu anakosa ajira hivi hivi yaani,inauma sana,mazingira ya uwekezaji nchini kwetu yana shida mahali.

Hapa kwetu mji kasoro meli,viwanda vikubwa kama viwili vimefungwa,ni mazava na cha tumbaku,vilikuwa vimeajiri watu wengi sana hasa kinamama,haya cha mkulazi cha miwa nacho tantalila tu hadi leo hakijaanza kufanya kazi,ndio kwanza miwa yao wanawauzia kiwanda kingine cha sukari cha mtibwa,hadi aibu yaani lengo lilikuwa wazalisje sukari,lakini miwa yao haizalishi sukari inabidi wamuuzie mtibwa angalau wasipate hasara kwenye uwekezaji walioufanya.
Mzava komefungwa hapana sitaki kuamini
 
Ukweli siku zote unachelewa , lakini kwa regime hii ya uwongo uwongo na uzandiki hakuna kitakachofichwa tusikijue.

Soon tutasikia, Mwekezaji alikuwa akiikosesha 'serekale' mapato , huku wakiwa wamekaza shingo.!
Itakuwa kama STAMICO yamebaki magofu tu
 
Pamoja na uwepo wa mada inayohusu kufungwa kwa kampuni ya Dangote hapa nchini iliyoletwa na Mkuu Return Of Undertaker, naomba Moderators muuache Uzi huu kwa maslahi ya mjadala na uelewa.

Kichwa pamoja na maudhui ya uzi wa mtajwa hapo juu ni kuleta habari na kutaka kuaminisha umma kuwa Dangote anataka kufunga kampuni yake kule Mtwara na kuondoa uwekezaji wake hapa Tanzania. Katika kuonesha ukweli huo kumeambatishwa habari ya gazeti la the Citizen la leo.

Kwa msomaji makini ataona na kujua kuwa Dangote ndiye anayepinga kufungwa kwa kampuni yake hapa nchini. Hivyobasi, hana nia ya kuifunga na kuondoka. Yeye ndiye aliyepinga na kufanikiwa kuzuia shauri la kufungwa kwa kampuni yake.

Iko hivi kwenye habari hiyo: Kampuni ya Dangote, kama kampuni nyinginezo, iliingia mkataba wa kuletewa fuel na kampuni ya NSK. Katika kufanikisha hilo, kampuni ya NSK ikachukua mkopo kama mtaji kutoka benki ya Standard Chartered wa bilioni 11.1.

Baada ya kushindikana kulipwa kwa mkopo huo, Standard Chartered ikawashtaki NSK na Dangote. Kufuatia shauri hilo, na katika hali ya kujitetea, NSK akapeleka shauri la kufungwa (winding up) kwa kampuni ya Dangote kwa kushindwa kulipa deni lake kwa kampuni hiyo.

Naye Dangote akawasilisha Mahakamani hapohapo Ombi dogo la kusitisha kwa muda shauri la kufungwa kwa kampuni yake. Ombi lake dogo Dangote ndilo lililotolewa uamuzi kwa kusitisha shauri la kufungwa kwa kampuni yake. Ndiyo kusema, Dangote amefanikiwa kwenye maombi yake.

Kwa kifupi, Dangote ndiye anayepinga kufungwa kwa kampuni yake pamoja na deni linalodaiwa kuwepo dhidi ya kampuni ya NSK. Kwenye mashauri hayo yaliyoripotiwa na the Citizen hakuna mahali Dangote na kampuni yake wameonyesha nia ya kufungwa kwa kampuni hiyo na kuondoka nchini.

Ni vyema kusoma habari kwa makini kabla ya kuandika uelewa ambao wakati mwingine waweza kubeba picha ya kupotosha umma. Dangote ndiye aliyepinga kwa nguvu zake zote kufungwa kwa kampuni yake kwenye mashauri matatu yaliyopo Mahakama Kuu yakihusika kampuni yake, kampuni ya NSK na benki ya Standard Chartered.
Hapa 'likes' zitapungua sana!
 
Tulidanganywa kuwa anafanya service ya week mbili kumbe anakusanya virago vyake aondoke uwekezaji bongo umemshindaView attachment 1640919


Ki- English inaonekana kina mpiga Chenga mleta mada, kwenye hayo maandishi hakuna mahali inapoonyesha kwamba Dangote Cement wanafungasha virago au wana nia hiyo, bali wao wanapinga hiyo winding up order inayo ombwa na Mdeni wao NSK oil .
 
Ki- English inaonekana kina mpiga Chenga mleta made, kwenye hayo maandishi hakuna mahali inapoonyesha kwamba Dangote Cement wanafungasha virago au wana nia hiyo, bali wao wanapinga hiyo winding up order inayo ombwa na Mdeni wa NSK oil .
Mleta mada ni moja watu ambao akili zao amekimbia nazo Lisu kwenda kwa Amsterdam
 
hakuna mkono wa makaburu kweli hapa maana wakaburu bifu za kibiashara wanaziweza saana ili kumiliki soko
 
Siyo huyo tu atakaye fungasha vilago Kwa kushindwa kufanya biashara

Hii inaitwa ni Anguko la kibiashara Duniani na kujengwa upya Kwa Uchumi wa Dunia Kwa mfumo mpya na mashariti mapya ya World Bank,

Miradi mingi ya Serikari itasimama na kote Duniani ispokuwa kwenye Baadhi ya nchi zilizoandaa na kuuleta huo mfumo Duniani,

Hutauza Wala kununua, hii ni Kwa wasomaji wa Biblia pekee,

Wakati Dunia inajiandaa Kwa maambukizi mapya ya Corona ambayo yatakuwa ni tishio na yaliyoongezwa nguvu mara dufu, nchi zote zitalazimishwa Ku lock down nchi zao na msukumo wa kufanya hivyo, utatolewa na WB na usipofanya hivyo Ka nchi kenu kanatemgwa na hakatasaidiwa Kwa chochote, na hutafanya biashara mahali popote

Duniani kote kwenye swala la ajira litazidi kutesa watu na itafikia mahali ofsi nyingi zitafungwa, na maisha haya magumu si hapa Tu Tz Bali ni Dunia kote, tunazidiana kidogo tu kutokana na namna ya chumi zilivyokuwa kabla ya Corona

Mwenye sikio na asikie. Dunia lazima ifikie tamati yake

Acha uongo, dawa ya COVID-19 imeshapatika na chanjo pia.
 
Dangote hawez kushindwa kulipa hio $2m nadhan ni mchongo unachezwa hapa atuachie manyoya bila bugudha
 
Hii NSK kwa nini inakimbilia winding up
Shortsightedness. Dangote employs a lot of people directly and indirectly.
Dangote pays a lot of taxes directly and indirectly.
Which judge in his right mind, without being influenced by stupid people will close such an egg laying goose?
 
Kwa akili ya kawaida tu mtu anaekudai 20 millioni anaweza kweli kwenda mahakamani kutaka uuze hoteli yenye thamani ya billioni tatu kisa deni lake.

Hiyo hela ukienda bank ukaweka 5% ya share equity ya hotel si bank wanakupa tsh 100 million dakika moja tu; unalipa na change inabaki.

Ni matumizi mabaya ya sheria na mahakama; yaani Dangote afunge biashara kwa deni la billioni 11 tsh.

I bet over 90% ya wachangiaji awajasoma ata hiyo habari yenyewe kuona ni namna gani huyo NSK alivyo mpuuzi.
Mkuu mashabiki wa chadema ni moja ya majanga tuliyonayo hapa nchini.

Ni wapumbavu sijapata kuona.
 
[emoji106] Kwanini Serikali ya CCM inawatesa investors?
Mkapa alijitahidi sana kuiamini have dunia kuwa Mambo ya Azimio la Arusha hayatajirudia tena, Kikwete akadumisha mahusiano mema sana na wawekezaji mbalimbali.
Sasa ngwe hii, tunajidanganya sana hatuthamini umuhimu wa uwekezaji.
Hala hatujali Ni watu wetu wangapi wanaoathirika kwa kukosa kazi mara tu wawekezaji wanapotimuliwa.
Endeleeni na tabia mbaya tutaona mwisho wake mwema
Mzee.
Angalia muktadha wa hoja kisha unachangia kwa mtiririko unaoibua hoja au kujibu hoja.

Hii ya kwako anzisha thread mpya tukuwekee facts namna wapinzani wanavyotumika kuwaumiza investors
 
Back
Top Bottom